New York, Marekani: Rais Samia ashiriki Mkutano kuhusu athari za Mabadiliko ya TabiaNchi

UKISIKIA UJINGA ULIOTOPEA NDIO HUU HAPA

Na Bollen Ngetti

WAKATI mwingine huhitaji hata elimu ya msingi kutambua kiwango cha ujinga wa mtu. Ni kheri anayeficha ujinga wake kwa kukaa kimya maana hutoelewa ni mjinga au ana akili sawa sawa.

Ninafuatilia kwa karibu sana safari ya Rais Samia Suluhu Hassan katika mtaa wa Brettonwood, New York nchini Marekani ambapo kama viongozi wengine duniani wameenda kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Umoja wa Mataifa. Katika Mkutano huu wakuu wa nchi hukutana kujadili mustakabali wa usalama wa dunia katika medani zote.

Rais Samia ameamua kupiga ndege wawili kwa jiwe moja tofauti na wenzake. Kabla ya kuondoka nchini tayari wafanyabiashara na wawekezaji ndani ya nchi walitangulia kwa gharama zao ili kutumia uwepo wa Rais wao kukutana na wawekezaji wa duniani kuwashawishi kuja kuwekeza Tanzania kwa kuzingatia kwamba tumeamua kufanya kazi na sekta binafsi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi.

Wakati baadhi ya Marais waliofika New York wakipumzika mahotelini kusubiri Mkutano Samia yuko bize kukutana na makundi mbalimbali ya wawekezaji kuwataka waje Tanzania kushirikiana na sisi kujenga nchi yetu. Hongera sana.

Ujinga wetu umechomoza pale ambapo baadhi yetu tunamsifia Raia wa Zambia kwenda New York kwa kupanda ndege ya abiria na ujumbe wa watu wachache. Tena wengine wakikoleza uongo eti kasafiri na watu watatu kisa, wamepiga picha ya watu waliowahi kutoka kwenye ndege. Jinga kabisa! Kwamba Samia kasafiri kwa halaiki ya watu kuponda raha! Huu ndio ujinga uliovuka mawingu.

Kwanza niwaambie wapuuzi hao kwamba kwa mara ya kwanza Rais kutoka Tanzania kufikia Hoteli ya kawaida ya The Pierre akiacha Hoteli za Nyota tano walizofikia wenzake. Lakini pia badala ya kusafiri na dege letu Air Bus mama yetu akasafiri na ndege ya Emirates na ujumbe wa watu wachache mno.

Kwa wasiofahamu msafara tuliouona sehemu kubwa na wanausalama wa Marekani ambao ndio wanamlinda kiprotokali za kiusalama. Tatizo wajinga wakiona ngozi nyeusi nasi wanajua ni wazaramo tu. Wale ni Wamarekani weusi na wakwetu hawazidi hata 8. Tuache ushamba wa kusifia Rais wa nchi nyingine tukiponda wa kwetu. Ni ujinga na Wazambia wanatushangaa!

Ziara ya Samia New York ni zaidi ya Mkutano wa UN. Tutegemee matunda mengi ya kibiashara baada ya safari yake hiyo maana anakutana na wakubwa wa dunia na "kuwatongoza" waje kupanua ajira nchini. Anafungua Tanzania kidunia tofauti na ziara za kutoka Mufindi kwenda Geita, kazi anayofanya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na ujumbe wake.

Kama Watanzania jukumu letu ni kumuunga mkono Rais wetu, kumtia shime, kufanya kazi kwa bidii kwa juhudi na maarifa ili kufikia malengo yaliyowekwa.

Nimefurahi hata alivyokutana na Mange Kimambi kuonesha kuwa hana chuki wala kisasi kwa mtu yeyote. Hivi ingekuwaje JPM ndiye angekutana na Mange? Si binti wa watu angekuwa "mshikaki" on the spot? Tuache ujinga tujenge nchi yetu.
#MguseMamaNinuke
 
Mama anazidi kukubalika duniani yupo tayari kuwa Rais wa ile United States of Africa
Kama Kuna uwezekano huo naunga mkono hoja kuwa Rais Samia Suluhu Hassan awe Rais wa United States of Africa, ili Tanzania iongozwe na Rais kutoka Upinzani.
 
Mkutano wa UNGA hauna faida yoyote kwa mwananchi yeyote Dunia nzima... Elewa kwanza hilo.
Unafaida kubwa sn agenda yamsingi inayo enda kuzungumziwa pia ni uharibifu wa hali ya hewa Duniani hilo tu linagusa kila mtu katika huu ulimwengu wa fuju jua hilo kwanza.
 
Nyinyi washamba wa Chato ifike muda sasa mkubali yule mungu wenu ametwaliwa na Mungu wa kweli, na sasa tunakwenda na mama mpaka 2030.
Mwananchi anapata manufaa gani kwenye mkutano wa UNGA na mingine ya pembezoni?.... Dadavua tu hiyo Mada, hayo mengine uliyoandika waachie wanaoshabikia siasa za majitaka!
 
Mwananchi anapata manufaa gani kwenye mkutano wa UNGA na mingine ya pembezoni?.... Dadavua tu hiyo Mada, hayo mengine uliyoandika waachie wanaoshabikia siasa za majitaka!
Unafaida kubwa sn agenda yamsingi inayo enda kuzungumziwa pia ni uharibifu wa hali ya hewa Duniani hilo tu linagusa kila mtu katika huu ulimwengu wa fuju jua hilo kwanza. Ukame wewe huoni, joto ulioni na nk.
 
Tunaambiwa amefanya mazungumzo na Rais wa Comoro na wa Sudani ya kusini. Ama kweli tuna safari ndefu!
Tena hizo ni nchi muhimu sana kwetu kibiashara.

Comoro kuanzia nyanya, vitunguu, nyama na kila kitu vinatoka Tanzania.

South Sudan ni Taifa changa linahitaji import kwa karibu kila bidhaa.

Kumbe humu wamejaa watu wajinga wanaodhani Rais wetu anaweza kukaa na Rais wa Korea ili tuweze kuuza Software Seoul?
 
Unaongea kishabiki badala ya kujenga hoja itakayoleta Tz endelevu
Washamba wa sukumagang mnajulikana tu kwa mawazo yenu ya kijima.International exposure ni jambo muhimu kwa kiongozi wa nchi. Huko anakutana na maraisi wenzake wengi kwa urahisi zaidi na kunabiloshana mauzoefu ya kuongoza nchi.
 
Washamba wa sukumagang mnajulikana tu kwa mawazo yenu ya kijima.International exposure ni jambo muhimu kwa kiongozi wa nchi. Huko anakutana na maraisi wenzake wengi kwa urahisi zaidi na kunabiloshana mauzoefu ya kuongoza nchi.
Wew Kibaraka wa mabeberu usie na aibu
 
Back
Top Bottom