Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 2023) Nairobi- Kenya tarehe 05 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Kimataifa kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23) unaofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Nairobi nchini Kenya tarehe 05 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Kimataifa wakati wa Wimbo wa Umoja wa Afrika (AU) na ule wa Taifa wa Kenya ukiimbwa mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Nairobi nchini Kenya tarehe 05 Septemba, 2023 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23) Nairobi nchini Kenya tarehe 05 Septemba, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23) Nairobi nchini Kenya tarehe 05 Septemba, 2023.
Kweni sisi Wapinzani mazingira hayatuhusu?Huyo Odinga wanamuendekeza sana ameketi hapo safu ya mbele kama nani?
Suala sio upinzani hapa najadili faida za hizi summits zisizoisha mwaka mzima... walikua Kwenye mkutano kama huu ulaya... mara rasilimali watu mara EAC mara SADC mara AU... sijui maziwa makuu... mara economic forums na upuuzi mwingine mwingi... hizi talk shops zimeisaidia nini Afrika?Kweni sisi Wapinzani mazingira hayatuhusu?
Nilikuwa nafikiri unamuongelea Raila OdingaSuala sio upinzani hapa najadili faida za hizi summits zisizoisha mwaka mzima... walikua Kwenye mkutano kama huu ulaya... mara rasilimali watu mara EAC mara SADC mara AU... sijui maziwa makuu... mara economic forums na upuuzi mwingine mwingi... hizi talk shops zimeisaidia nini Afrika?
As former Prime minister of Kenya!Huyo Odinga wanamuendekeza sana ameketi hapo safu ya mbele kama nani?
Bottom line: waafrika tuna mambo ya hovyo sana aisee... mwaka mzima hawa viongozi wanazurula kwenye summits tu zisizowasaidia chochote zaidi ya kwenda kufedheheka kama yule rais wa Cameroon aliyejamba mbele za watu!