New Track:Siri ya Mchezo-FID Q feat Juma Nature

Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,882
10,193
Rapper FID Q jana ametoa track yake ya tatu itakayokuwa kwenye album yake ijayo Kitaalojia track inaitwa Siri ya Mchezo akiwa amemshirikisha Juma Nature ,Producer aliyetengeneza ni Ben Mwamba

SIRI YA MCHEZO LYRICS
Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na umuhimu kihivyo… stimu zikanipa elimu ya Biko/ Kimaandiko
… kimistari.. hadi fans wanascream nikirap../ sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop/
Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa #teamMabiiitoz /
Achana na power window.. sijui rimz za dimpoz/
haileti bingo, mshiko? Star ishi simple/ sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa
.. hauna kitu/
jikombe ugongwe…mtaaa ukuone hauna ishu/

ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/
Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za harakati ni ujinga?/
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji/ na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..sio kipaji kama Kubanda eti unachana kigumu/ kisa track ikivuma sana kwenye chati haidumu /
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA../ baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../ najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na wakinitisha najihami../ inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/
''Pole MAPROSOO'' ( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu.. / WAZEE ni wahuni hadi soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu/ na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../ huo ni utumwa pia/Unafanya vijana wanaumia../
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..


CHORUS: ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza.. kisha utapata/ x 2
Siri ya mchezo naijua mimi.. tu.. na hakuna mwingine x 2


VERSE 2:
Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara inaweza buma/ wakati SIASA kila mara ukiwa unang'ara ujue kuna.. kinara/ anayeunda msafara wa wanaojituma na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna/ KIDUMU CHAMA CHA MASELA… Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,/
tuone kufuru za wenye hela/
TANZANIA ni ' demu wa mtungo ' wanamuiita CHA WOOTE/'' HANGOVER .. ''anaikimbia kwa kupiga ' " mtungi " saa zote /Mkubwa anazuga atasolve… matatizo ya nchi yake/ ''na gari bovu..'' halisukumwi kwa kukaa ndani yake/
MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza../ je Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza? /
hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion/
na daily tunafeli sababu ya POLITICAL institutions/
CIVILIZATION imeadvance sasa wanatuua economically../
hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free/
Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu/
kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/
Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua..?
zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua?
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka/
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA/
Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua nani leo atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????
 

Attachments

  • Siri ya Mchezo-Fid Q ft Juma Nature.mp3
    9 MB · Views: 779
fareed ni nyoko! zma nyimbo zote wikendi ni huu tu ngoja niudownload. mwanangu kibra kwa chorus. hip hop is back
 
Fareed hajawah kukosea. Haya mashairi ni mazito sana. Itamchukua miaka hata 20 kwa diamond au msanii wa rnb kuandka angalau verse moja tu yenye uzto kama huu
 
Jinsi siku zinavyozidi kwenda FID Q anazidi kuimprove,i hope hii album itakuja kuwa "The best Hip Hop Album in Tanzania
 
ni noma but kulinda heshima isije kubainika katafsiri
 
Ngoma kali ila punch lines nyingi amechukua ktoka kwenye ngoma zake mbali ambali ambazo alisharecord
 
me nimeiona moja ile ya madawa kuugua. Nyingne ipi don?

Civilization imeadvance sasa wanatuua economically,
Hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free - ni punchline aliitumiwa kwenye ngoma flan alishirikishwa na Beezy zamani kidogo. Humo anakwambia 'Usimpe Nyama ngumu ya nyati kibogoyo kumpima woga'.
Zipo nyingi amechukua lakini ngoma imetulia sanaa.
 
Jinsi siku zinavyozidi kwenda FID Q anazidi kuimprove,i hope hii album itakuja kuwa "The best Hip Hop Album in Tanzania

Mstari wa Fid Q ninaoukubali mpaka kesho ni kwenye umbo namba 8 ;anasema "kivipi nimkazie jicho wakati binti kasimama!" huu mstari una tafsiri tatu..nani anaweza kuzidadavua?
 
give us the meaning!

Kivipi nimkazie jicho wakati binti kasimama?
maana zake izi hapa bob
1- Kivipi nimle tu kwa macho wakati demu mwenyewe ni mzuri?(demu kasimama maana yake demu mrembo)
2- kivipi niishie namtazama tuu wakati binti kashasima,hapa binti kama alikuwa anatembea then akasimama..so inabidi amfuate amtokee.
3- kivipi nitamkaza kwenye jicho wakati binti kasimama(hapa jicho ni sehemu ya haja kubwa,,,kumuingilia demu kinyume na maumbile sharti hainame,,,akisimama inasumbua ndio maana Fid anauliza 'kivipi'.....
 
Kivipi nimkazie jicho wakati binti kasimama?
maana zake izi hapa bob
1- Kivipi nimle tu kwa macho wakati demu mwenyewe ni mzuri?(demu kasimama maana yake demu mrembo)
2- kivipi niishie namtazama tuu wakati binti kashasima,hapa binti kama alikuwa anatembea then akasimama..so inabidi amfuate amtokee.
3- kivipi nitamkaza kwenye jicho wakati binti kasimama(hapa jicho ni sehemu ya haja kubwa,,,kumuingilia demu kinyume na maumbile sharti hainame,,,akisimama inasumbua ndio maana Fid anauliza 'kivipi'.....

Kha wewe mastomach ni noma jamaangu! Hiyo maana namba tatu sikuwahi kuiwaza asilani. Hip Hop ni zaidi ya kughani kwa lisauti ligumu kama lile jamaa la chongo, K. PINA
 
Back
Top Bottom