Juma Nature ndio best storyteller wa muda wote Bongo. Wasanii wachanga mnao-rap jifunzeni kwa Juma Nature

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,522
7,370
Kwenye muziki wa hiphop bongo hakujawahi kutokea msanii mwenye nguvu kama Juma Nature.

Juma Nature aliingia kwenye muziki akaukuta umejaa umarekani mwingi na akaubadilisha mchezo kabisa. Silaha yake kubwa ilikuwa ni storytelling.

Ipo wazi Juma Nature ndio bingwa wa storytelling kibongobongo. Alianza na story ya kigheto ghetto mpaka simulizi za ex wake Sinta. Na alivutia kwa sababu alitumia ucheshi na lugha za uswazi.

Kwa sasa muziki wa bongo unafanya vizuri kwenye waimbaji ila upande wa rap ni kama umekufa. Kwa sasa hawezi simama rapa akachana nchi ikastuka.

Shida kubwa marapa wa sasa wamewekeza kwenye mistari konde yani ufundi wa kugeuza geuza mashairi na wengine wameingia kwenye trap wanajikuta kina Dababy au Migos hakuna localisation.

MCs wadogo jifunzeni kwa Juma Nature aliingia kwenye game na silaha yake kubwa ilikuwa kuelezea story haswa za uswazi. Aliisimamisha mitaa akawa jina la mchezo.

Jifunzeni storytelling... hakuna mwanadamu anayeweza kuukwepa mtego wa story kila binadamu anapenda kusikia visa mbalimbali.

FA alitupa kisa cha aliyekufa kwa ngoma... Profesa akatuletea mwanasiasa muongo muongo kwenye ndio mzee... Ngwea akatupa story za ghetto lake.... J Mo akatupa mawili matatu kuhusu mabalaa ya mvua na jua...Nature ndio aliua kabisa akatusimulia Mzee wa Busara, Drama za Sinta. Mtoto Iddi nk

Hii ndio siri pekee nataka niwape vijana wadogo mnaoingia kwenye muziki wa hiphop kama mnataka kutengeneza pesa...Hakikisha unachokiandika hata yule beki tatu anaeosha vyombo nyumbani anaweza kuvutiwa na kukiimba.

Maisha ya binadamu ni hadithi.

Lakini msiandike story kama mtu anasoma kitabu cha Shigongo. Andaeni content zenye ubunifu wa kimuziki. Hii ndio siri ya Juma Nature kuubadili mchezo na akaibeba Temeke mabegani, Storytelling.

Akitokea storyteller wa rap kuna pesa yake nyingi sana ya kubadilisha maisha yako na family yako.
 
Kwa sasa amna anaeweza kutoa kazi nchi ikashituka vipi kuhusu =Rapcha-Lissa

Kwa upande wangu MCs na storyteller bora kuwahi kutokea bongo ni Dizasta Vina
Rapcha anajitahidi ila bado anajitafuta, Lissa ilikuwa ni story nzuri lakini bado haikuwa na ubunifu wa kitofauti. Rapcha akikaza anaweza kuwa bora anao mkono mzuri wa kuandika.

Dizasta mimi uwa namuweka kwenye upande wa Mrisho Mpoto sijui kwa nini uwa mnamuweka kwenye kundi la MCs. Kwanza story zake zipo so direct yani hadithi njoo uongo njoo utamu kolea.
 
Nyimbo za storytelling ni kali sana.. hata dogo Rapcha alipotoa Lissa unaona kabisa watu walikua wamemiss hivyo vitu.. ngoma ikapata reception nzuri.
Storytelling ndio namna pekee watu hawawezi kuresist sanaa yako. Watu wanapenda story ndio maana wabongo wanashinda Instagram wanapenda story.
Nafikiri Rapcha atakuwa amejifunza.
 
Back
Top Bottom