Hii ni kwajili ya mashabiki wa Fid Q na muziki wa Hip Hop tu

Saad30

JF-Expert Member
May 26, 2020
1,815
3,637
Habari wakuu,

Naomba kunanza na Track hii ya Fid Q ft Juma nature, SIRI YA MTUNGI.

Naandika mistari ya hii ngoma nitakapoishia atendelea mwingine hadi track kuisha, kisha mkuu mwingine anaweka track tunapita nayo.

Song: Siri ya mtungi
Fid Q ft Juma Nature

Verse no: 1
Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo//Skua na umuhimu kihivyo//stimu zikanipa elimu ya BIKO.

Kimaandiko,kimistari fans wana-sream nik-rap//skuamini kama nnaZari hadi nilipo ibuni Hip Hop

Wanapagawa na baadhi ya mambo nayoyajua//pia nina uwezo kufanya mpaka madawa yakaugua.

Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa team mabitozi//achana na power window sjui rimz za dimpoz

Haileti bingo mshiko star ishi simple//sanaa iko hivyo sometimes hukataa kukaa ulipo

Wanao dharau hujiletea matatizo//hawajui kama wadau hupendelea kukuona hivyo?

Bonge la star donge la njaa hauna kitu//jikombe ugongwe mtaa ukuone hauna inshu.

Ukishindwa kujiandaa// jiandae kushindwa mjinga utaachwa unashangaa kumuona martin kadinda

Usmart anaotinga//majumba mandinga
Je hizi tracks za harakati ni ujinga?
 
Hapana... nguvu ya mamba ni maji

na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati

sio kipaji kama Kubanda eti unachana kigumu

kisa track ikivuma sana kwenye chati haidumu

Amani kwa chachage na Makuwadi wa soko huria..

baba asante kwa utafiti na zawadi ya almasi ya bandia

Nyumbani nasikiliza dunia ya Marijani

najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?

labda kubisha na wakinitisha najihami..

inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani

Pole MAPROSOO umefanya umetubu..

WazeE ni wahuni hadi soo waay back before Sugu

Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu

na mbwa mwitu wenye siri.. ili bepari umuabudu

kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu..

huo ni utumwa pia

Unafanya vijana wanaumia..

Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..
 
Hiphop urudi ,naona sahv mziki unaotamba ni wa kuhamasisha ushg tu

Ova
 
Chorus

Siri ya mtungi aijuaye kata
Komaa kaza kisha utapata ×2

Siri ya mchezo naijua mimi tu
Na hakuna mwingine ×2
 
Tofauti ya biashara na Siasa ikila hasara inaweza buma

wakati Siasa kila mara ukiwa unang'ara ujue kuna.. kinara

anayeunda msafara wa wanaojituma

na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna

Kidumu chama cha masela Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,

tuone kufuru za wenye hela

Tanzania ni demu wa mtungo wanamuiita cha wote

hangover, anaikimbia kwa kupiga mtungi saa zote

Mkubwa anazuga atasolve matatizo ya nchi yake

na gari bovu.. halisukumwi kwa kukaa ndani yake

Maendeleo ni ile ndoto mwekezaji ashaipuuza..

je Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza?

hakuna Uhuru wa kweli msidanganywe na illusion

na daily tunafeli sababu ya political institutions

civilization imeadvance sasa wanatuua economically..

hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free

Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu

kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu

Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua?

zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua?
...................
 
Hii ngoma inaitwaje?
 
Wamejivisha U-Noah safina zao zikatoboka

Wakajivisha U-Musa fimbo zao hazikugeuka nyoka

Sasa wanaujaribu umungu mtu kuamua leo nani atatoka??

Chorus.......
 
Back
Top Bottom