New Targets: Slaa na Raia Mwema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

New Targets: Slaa na Raia Mwema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 5, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kama dalili zinazoendelea zitakuwa ni zile zile zinazotarajiwa basi gazeti la Raia Mwema na Dr. Slaa wameanza kumulikwa kwa kurunzi kali zaidi. Raia Mwema kwa kuanza kuchukua nafasi ya magazeti yenye kuthubutu zaidi na taarifa za kina za uchunguzi na uchambuzi usiokuwa na kigugumizi. Kwa mara nyingine Jenerali anaanza kutupiwa macho kwani inaonekana ameanza kurudisha makali yake kwa timu aliyoikusanya... so stay tuned.

  Baada ya kudokezwa kuwa Dr. Slaa anaweza kupendekezwa na chama chake kuwa mgombea wa Urais mwakani a new strategy imeanza kutengenezwa yenye kukumbushia jinsi Mrema alivyokuwa neutralized. Mbinu hii ni ile ile ya kuchafua, kupandikiza hofu, na zaidi ya yote kuquestion utimamu wa mtu... Dr. Slaa ameonja kidogo makali ya CCM political machinery lakini kama kweli Chadema wanafikiria hivyo mtashangaa mashambulizi yajayo!! He better brace himself kwani CCM wanajua kabisa JK vs Slaa itakuwa an uphill battle!
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  ..... beg to differ, itakuwa kama kumsukuma mlevi!
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Nani anayesukuma na kusumwa, I suppose you meant anayesukumwa (a.k.a Mlevi) ni JeiKei
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hakika Chadema wakimsimamisha Slaa, watakuwa wamecheza. huyu jamaa is a right person kuiongoza hii nchi.

  Halafu pia nilisikia kuna hoja imetolewa kuwa ingefaa mgombea urais anayefikisha 3% ya kura katika uchaguzi mkuu aoutomatically aingie bungeni. Nafikiri hii ni pendekezo zuri. Hata akina lipumba tutapata mchango wao lakini ninavyowajua CCM watang'aninia viti maalumu matokeo yake wanajaza bungeni ma rubber stamp kibao kutuongezea mzigo wa kuwahudumia tu.
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dawa ya kuwashinda hawa majangili ni ku-pre empty uovu wao ili wakija nao hapa tuwe tunawashangaa tu. Naona ni wajibu wetu sote kuhakikisha kuwa maoni ya wengi yanapewa nafasi,
   
 6. k

  kigugumizi Member

  #6
  Nov 5, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana nilisema kuwa "Chadema Kuteketezwa"
  Leo Mwana kijiji amekuja na jipya la Raia Mwema na Dr. Slaa.

  Taarifa za kina ndani ya Chama hicho kinadai, kuwa Dr. Slaa bado hajaridhia kugombea Urais licha ya kupata msukumo mkubwa kutoka kwa wananchi. Dr. Slaa ambaye ni Kiongozi makini kuliko wote Tanzania , bila hofu atamsumbua sana JK 2010 ikiwa ataridhia maombi ya wananchi.

  Amejitokeza mara kadhaa kukiri kuwa hana mpango na Urais. Wala hiyo siyo mkakati wake, watu wa karibu yake wanasema kuwa bado na kiu na Ubunge.

  Raia mwema bado ina lack jambo moja, inaandika habari kitaaluma zaidi, target yake ni middle class. wakati mwana Halisi kama udaku wa kisiasa inaeleweka na kila Mtanzania.

  Tusubiri - Nadhani Zito anafaa sana kwa 2010 kwa Chadema!
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Patachimbika mwakani ikiwa ni kweli
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Nov 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  siku chache zijazo mtaanza kuona haya..
   
 9. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Labda dr atagombea kuongeza kura cha CHADEMA lakini sidhani kama hata yeye anaamini kwa structure hii iliyopo kama anaweza kupata kura nyingi na kutangazwa mshindi.

  Nasema hivyo [kupata kura nyingi nakutangazwa mshindi] nikijua kuwa ni vitu viwili tofauti, hasa nikikumbuka uchaguzi wa 1995 kule Zenji CUF walipongezwa kwa kupata kura nyingi na CCM wakapongezwa kwa kushinda.

  Lakini pia sioni mkakati wa chadema unaokiplekea kufikiri kitashinda uchaguzi wa rais wa rais 2010,bado mtandao wao vijijini ni mdogo sana, na huko ndiko wapiga kura wengi waliko na ni vigumu kujenga mtandao wa kuaminika kisiasa katika kipindi cha mwaka mmoja tu.
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  km ni kweli ntaingia mtaani 2010 kumpigia debe slaa na chadema nyumba hadi nyumba
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Nov 5, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Anafaa nini ubunge au uraisi!!!!!
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kama ni katika kuboresha RUZUKU ya CHADEMA kwa kura za URAISI sawa. Dr Slaa na agombee tu. Uphill battle ya kweli inaweza kuwepo 2015 kwa kuwa CCM wamejichafua na kuchafuana sana
   
 13. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  mkuu inabidi hiyo shughuli uaze sasahivi,chama kinahitaji kuwa na mizizi muda mrefu tu kabla ya uchaguzi,chama kiwe na wanachama wake kabla hata ya uchaguzi kuliko kutegemea kampeni za wakati wa uchaguzi ambao kwa kweli huwa ni muda mfupi sana kutegemea kuweka mizizi ya ukweli ya kutafuta ushindi,opereheni sangara naona ikiendelea italeta mafanikio makubwa tu
   
 14. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani umri wa Zito haumruhusu kugombea urais. Pia na kwakuwa chama chake walimwangusha kutokugombea U/Kiti hawezi pia kupendekezwa kwenye kitu kikubwa zaidi.
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  Nov 5, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kupungua kwa ngvu za MwanaHalisi, kufifia kwa Uadilifu wa Tanzania Daima, kuibuka upya kwa magazeti ya Nipashe na ndugu zake, na pia Kurudi katika Chati kwa Jenerali, ndilo Tishio jipya katika siasa za hapa nyumbani Tanzania.

  Siasa za CCM , zimejaa uharamia na uharifu wa kila na namna, wakizitumia vizuri mamlaka mbalinbali ambazo ziko chini ya Raisi ni raisi kwao kuhujumu harakati halali za kisiasa, ila kila kosa atakalo lifanya JK kutaka kuwaziba midomo Jenerali/Raia Mwema na kamanda Dr W. Slaa ndipo pale atakaongeza umaarufu wa kisiasa wa mahasimu wake sambamba.

  Jenerali ni mahili wa kukwepa vihunzi vya kisiasa huku akijilinda kwa kila gharama kuchafuta na dhana mbalimbali za kifisadi au mafisadi, huku akijiweka kando na baadhi ya marafiki zake na yeye kubaki kua safi.
   
 16. N

  Natasha Ismail JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Dr, Father, baba padri, paroko Slaa,

  Pamoja na kwamba mimi si mwanachama wa chama chako wala chama chochote hapa nchini nakushauri usikie maombi ya wananchi na ukubali kugombea urais 2010. Nakuahidi kukupigia kampeni nyumba hadi nyumba bila malipo kwani naamini unaweza. Naamini hautatuangusha. May Allah guard you amen
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  Nov 5, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Dr Slaa ndio mtu stahili kwa kuingoza nchi hii, baada ya kufikishwa hapa na hawa marafiki na siasa zao za kujuana na kupendeleana, nchi hii inataka mwanasiasa mwenye mrengo usio wa katikati, hakuna kuuma na kupuliza.
   
 18. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2009
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  km ni kweli ntaingia mtaani 2010 kumpigia debe slaa na chadema nyumba hadi nyumba

  nakuunga mkono na mguu, tutakua wote. ila akiwa zito sikusaidii. dogo huyo simuamini hata kidogo
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Dr Slaa alipata kura kiasi gani jimboni kwake mwaka 2005?
   
 20. M

  Masatu JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Dr Slaa hafai kuwa Rais na hii ni kwa sababu urais ni zaidi ya kufyatua mabomu Mwembayanga.

  Juhudi zake jimboni si za kubeza hata kidogo hata hivyo urais sio tu hawezi bali hapati na hasa ukizingatia chama atakachogombea si chama cha siasa ni genge la wabangaizaji wa mjini tu
   
Loading...