Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

2005 Sikumpa Kura Yangu JK; 2010 Sikumpa Kura Yangu JK. Kwa Sababu JK Ni Chekibobu. Siwezi Kutoa Kura Yangu Kwa Chekibobu. Bora Nife Tu, Kuliko Kutoa Kura Yangu Kwa Chekibobu. Chekibobu Hastahili Kuwa Rais wa TZ. Ndiyo Maana Tuna Matatizo Mengi Kwa Sababu ya Huyu Chekibobu JK.

Ni kweli kabisa .Hana tofauti na akina Ndama Mtoto wa Ng'ombe , etal
 
Mi ningekuwa na uwezo ninge Force ibadilishwe bwana lakini bado nachechemea,, lakini naamini kati ya watu watakao shiriki kuibadilisha katiba hii ni mimi, na wewe Rafiki

Kenya waliandamana sana kudai katiba mpya. Nakumbuka katika moja ya maandamano hayo, somebidy Prof. Ghai (mzungu au mhindi) alikuwa amevaa T-Shirt iliyoandikwa "Why hire a Lawyer if I can buy the Judge". Kwa maana nyingine, tunahitaji Wa-TZ kuanza kudai katiba kwa maandamano ya amani, migomo baridi hasa kususia mikutano ya wanasiasa wakubwa, na kupiga kampeni ya nguvu ili watu waelewe kwa nini tunataka katiba mpya na watuunge mkono.

Nafikiri hii ndiyo iwe strategy ya kwanza, tukiungwa mkono wa wabunge wote wa upinzani. Najua hamasa ipo. Tukumbuke Mawaziri walipozomewa baada ya bajeti ya pili ya serikali ya Kikwete! Slogan "KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI". Tuwaombe wananchi wawasusie wabunge wao ambao hawataunga mkono hii move.

Dr. Slaa anzia hapo. Tutakuunga mkono.
 
Katiba itabadilishwa tu siku si nyingi sana. tena asipoangalia mabadiliko yatakuja kama ambavyo hakutarajia mabadiliko ya uchaguzi huu
 
Je unajua kuwa Chenge amesaini katiba inayotumika sasa? Alikuwa ni mwanasheria mkuu wa serikali. Na ushaidi hupo hapo chini. Na wakati huohuo anataka kutumia katiba ya sasa kumpa uspika, wakati nyie mnadai kuwa ni fisadi.




Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________

1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
_____________
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA YA MWAKA 1977
(Toleo hili la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977,
limezingatia na kuweka pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Katiba
ya Muungano tangu ilipotungwa mwaka 1977 hadi tarehe 30 Aprili, 2000.
Dar es Salaam, A.J.
CHENGE
1 Novemba, 2000 Mwanasheria Mkuu

 
Atake asitake mabadiliko huwa hayazuiliki, katiba mpya tutapata no matter how long
 
Watanzania si waoga kiasi hicho lkn ni wajinga kwa kukosa elimu ndio ikawa hawawezi andamana wala kudai haki na wakiandamana wenzao wakauliwa wengine huchekelea mfano ni mauji ya wapemba mwaka 2001. Watanzania wengi walifurahia sasa wacha yafike na nyie si hamuelewi?
 
We need initiators wa hii tuna facts za kutosha na rahisi kueleweka kwa wananchi. Kwangu mimi imesha kuwa general answer kwa kila anaeuliza kuhusu matatizo ya uongozi wa tz. Ebu nisaidieni ni nani anafaa kati NGOS, CHAMA CHA SIASA au an indivial. Maana serikali iliyopo ndo wanufaikaji na hii katiba iliyopo sio rahisi ku support postive changes
 
Inasemekana Katika maswali ambayo humuudhi Muheshimiwa Jakaya mrisho kikwete, ni pamoja na Swala la Katiba ya Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania...

Ameshasikika ,marachache akisema kubadili katiba si maendeleo ya nchi huku akijua kuwa Katiba ndiyo inayo Bana maendeleo ya nchi,,

Tazama Zambia, Tazama Rwanda,, Nchi hizi mbili zilikuwa na rushwa na ufisadi wa kutupwa,, lakini Maraisi wake wameamua kujikubali kuwa lazima Wananchi waumie kwa kuwabana na sheria ngumu zinazo leta maendeleo ya nchi ili baada ya maendeleo hayo kupatikana watafurahia maisha

Wananchi wengi tunaishi kwa kukosa besic needs kwa kiwango kile kinachotakiwa,,,

Katiba hii inatakiwa ibadilishe jamaniniiii

Kubadili katiba ili alete maendeleo hawezi labda kuongezaa kipindi cha tatu!!
 
Hivi kwanini tusi washawishi Watanzania tuungane Tanzania Nzima Kudai Katiba mpya?
Tuungane kuidai Katiba mpya

Ni kuwa tembea mitaani kisha uwaulize watu mia moja je wamewahi kuiona ama kuisoma Katiba?
Nadhani jibu litakuwa hapana.
So tusikimbilie kubadili kitu ambacho hata kilichomo ndani hatukijui.
Kwanza elimu itolewe juu ya hii katiba ya sasa na tuelezwe mapungufu yake then tuanze mikakati.
 
Woga chanzo chake ni ujinga. Hata hao CCM na vibaraka wao polisi wanajua wanaweza kutisha tu, ikizidi wanaweza kuuwa jozi moja tu ya watu kabla dunian nzima haijawaangukia kama tani ya mchanga. Dunia ya siku hizi hakuna serikli yeyote- hasa hizi omba-omba- ikafanya mauaji itakavyo. Ndiyo maana watu wasemapo waandae maandamano ya amani wasikia sauti kali za kuwatisha kutoka polisi, kwa vile wajua wakiandamana wataweza kuvunja ule uzio wa woga waliouweka! Ni tisha tisha tu ya kudanganya wajinga. Lakini iko siku mtu mmoja atajitutumua na kutamka ' Ah,Mfalme yuko uchi' hiyo siku iko karibu sana kutokana na ubabe wao. Na hpo nipo uzio wa woga utakatwa.
 
kwa nini hataki kubadili katiba? ukweli si rahisi kabisa watawala kukubali kubadili katiba itakayoaccomodate vyama vyote vya siasa.

kubadili katiba kunahitaji pressure na nguvu isiyo ya kawaida.

kwa msemo huu wa kikwete ni sawa na kuwaambia wapinzani hawapo na HAWAWEZI!!!!

moja ya mbinu ilikuwa kususia uchaguzi mpaka NEC na katiba vibadilishwe, lakini vyama vyetu vya siasa vikiongozwa na walafi na waroho wa madaraka kama akina LIPUMBA NA SLAA walijua wataingia ikulu! tu!!! HIKI KITUKO CHA KUFANYA CHAGUZI KATIKA MAZINGIRA HAYA NA BADO MKAITA KURA NI HAKI!!! NI KITUKO CHA KARNE NYINGI ZIJAZO!!!!!
 
Watanzania tulikuwa tumepata nafasi pekee ya kumpata kiongozi ambaye anegtupatia katiba ya kisasa sambamba na matakwa ya millenium hii. Unfortunately majambazi wametuharibia bahati yetu hiyo na kuturudisha kwenye ujima.

Nashindwa kuwaelewa watu wanaosema President wa watu Slaa akubaliane na ujambazi huo. Ningemshauri anyamze kwa kipindi lakini akumbuke kuwa watanzania wengi wanahitaji uongozi wake kuliko kipindi chochote katika 15 iliyopita; watu wanataka uhuru wao halisi wakilindwa na Katiba yao, siyo huu wa bandia ambapo katiba inawalinda wakubwa tu. Slaa asikubaliane na hiyo dhana potofu kuwa akubali matokeo ya uonevu eti kwa faida ya amani.

"Those who sacrifice liberty for security deserve neither!!!"
 
Back
Top Bottom