Neville Meena ametutusi kuita Tanganyika nchi ya "KUFIKIRIKA"

hili halipingiki kuwa Tanzania ni nchi ya kufikirika na sihivyo hata kusadikika inawezekana kabisa
 
Neville Meena tuombe radhi wale wote tuliozaliwa TANGANYIKA kwa kuiita nchi yetu tulimozaliwa eti ni ya KUFIKIRIKA eti tu kwa kuwa wewe umezaliwa TANZANIA. Umemtusi hata Rais wa awamu ya kwanza Hayati Mwalimu Nyerere na wale wote walioshirikiana nawe kuikomboa Tanganyika mikononi mwa wakoloni. Makala yako katika gazeti la Mwananchi leo jumapili ulikotaja kuwa kwako Tanganyika ni nchi ya kufikirika haikustahili kuchapishwa. Nawasilisha kwa wana JF wenzangu.
ni ya kufikirika ndiyo. kwani ipo?
 
Mnaopinga na ku-support hoja kabla hautjaenda mbele namoba mnitajie SIFA za NCHI (kipande cha ardhi) KUITWA NCHI ni zipi. Tukishaelewa SIFA za nchi then Tunaweza kujibu kama Tanganyika ni nchi au ni nchi ya kufikirika?

Tusi argue kama mahayawani.
 
Et mtoa mada hebu jitetee kwa kuwaonyesha wanaokupinga ilipo Tanganyika. Si wewe unaiona? bas kata mzizi wa fitina na taja mipaka yake.
 
Mnaopinga na ku-support hoja kabla hautjaenda mbele namoba mnitajie SIFA za NCHI (kipande cha ardhi) KUITWA NCHI ni zipi. Tukishaelewa SIFA za nchi then Tunaweza kujibu kama Tanganyika ni nchi au ni nchi ya kufikirika?

Tusi argue kama mahayawani.
Naomba hayo uyafanye mwenyewe na kama huelewi busara ni kutochangia mada. Usitupe kazi tukufundishe afu ndo tuchangie? noooo we jifundishe ukijua njoo tulonge ukikwama basi tena.
 
Neville Meena hana kosa lolote kwani ameongea ukweli wake. Kimsingi yeye anaitambua Tanzania na sio Tanganyika.
Suala hili linavurugwa kabisa na katiba yenyewe ambayo haiitamki Tanganyika bali Tanzania Bara. Sasa Tanzania Bara ni nchi gani kihistoria?
 
Hata TANZANIA BARA nayo niyakufikirika. Tanganyika ilitawaliwa, ikapigania uhuru na ikapata uhuru. Sasa hiyo Tanzania Bara imeibukia wapi kama sio ya kufikirika pia???
 
Kweli Unaumaaaaaaaaa.

Lakin ukweli siku zote unasimama.

Hongera Neville meena
 
yuko sahihi kabisa sema labda wewe ukilaza unakusumbua, kwanza inakubidi ujue sifa ya kuwa nchi ni nini!! kwasasa Tanganyika ni nchi ya kufikirika tu yaani ukubali au ukatae!!

Ndugu yangu Mimi nimezaliwa Tanganyika Nyie mwapenda kuita (Tanzania bara). Kwangu mimi Tanganyika si nchi ya kufikirika kwa sababu Tanzania kama hujui imeungwa ungwa kwa nchi mbili nazo ni Tanganyika na Zanzibar. Sasa hiyo Tanzania unayoisema wewe ni ipi. Siku zote mktaa kwao ni mtumwa. Kamwe hatuwezi kuibeza Tanzania kisa eti Tumezaliwa baada ya Muungano hilo haliwezekani daima.
 
Ni msaka tonge tu Meena na ujue kalishwa Yamini na Chama Twawala sio bure hawezi kutoka povu.
 
Karibu nchi yangu Tanganyika,Kwangu mimi hii Tanzania ndiyo ya kufikirika,haijulikani ilipata uhuru lini na hivyo ipo ipo tu! Haina hata mashujaa walioipigania hivyo kwangu mimi haina thamani yoyote
 
yuko sahihi kabisa sema labda wewe ukilaza unakusumbua, kwanza inakubidi ujue sifa ya kuwa nchi ni nini!! kwasasa Tanganyika ni nchi ya kufikirika tu yaani ukubali au ukatae!!


Which means Tanzania nayo ni nchi ya kufikirika (maana ukitoa ama Tanganyika au Zanzibar basi Tanzania haipo).
 
Neville Meena tuombe radhi wale wote tuliozaliwa TANGANYIKA kwa kuiita nchi yetu tulimozaliwa eti ni ya KUFIKIRIKA eti tu kwa kuwa wewe umezaliwa TANZANIA.

Umemtusi hata Rais wa awamu ya kwanza Hayati Mwalimu Nyerere na wale wote walioshirikiana nawe kuikomboa Tanganyika mikononi mwa wakoloni. Makala yako katika gazeti la Mwananchi leo jumapili ulikotaja kuwa kwako Tanganyika ni nchi ya kufikirika haikustahili kuchapishwa.

Nawasilisha kwa wana JF wenzangu.

kishawasahau weNZAKE WOTE WALIODHURIKA WAKIPIGANIA TANGANYIKA ! KWELI CHEO NI DHAMANA .
 
Neema huyu si mnajua fika kabisa mtu ambaye yuko ccm kipindi kile mwangosi kauwawa na majambazi ccm alikuwa akijipendekeza sana kwa waziri nchimbi kwa wakati ni danguro la njaa huyu
 
Neema huyu si mnajua fika kabisa mtu ambaye yuko ccm kipindi kile mwangosi kauwawa na majambazi ccm alikuwa akijipendekeza sana kwa waziri nchimbi kwa wakati ni danguro la njaa huyu

tangu kipindi hicho nilimdharau sana huyo jamaa !
 
Back
Top Bottom