Neville Meena ametutusi kuita Tanganyika nchi ya "KUFIKIRIKA"

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
206
Neville Meena tuombe radhi wale wote tuliozaliwa TANGANYIKA kwa kuiita nchi yetu tulimozaliwa eti ni ya KUFIKIRIKA eti tu kwa kuwa wewe umezaliwa TANZANIA.

Umemtusi hata Rais wa awamu ya kwanza Hayati Mwalimu Nyerere na wale wote walioshirikiana nawe kuikomboa Tanganyika mikononi mwa wakoloni. Makala yako katika gazeti la Mwananchi leo jumapili ulikotaja kuwa kwako Tanganyika ni nchi ya kufikirika haikustahili kuchapishwa.

Nawasilisha kwa wana JF wenzangu.
 
yuko sahihi kabisa sema labda wewe ukilaza unakusumbua, kwanza inakubidi ujue sifa ya kuwa nchi ni nini!! kwasasa Tanganyika ni nchi ya kufikirika tu yaani ukubali au ukatae!!
 
Neville Meena ndo yupi?ndo huyu nayemuonaga pale QC akija kusaini hela kwa Manji kila mwisho wa mwezi au namfananisha?
 
Neville Meena tuombe radhi wale wote tuliozaliwa TANGANYIKA kwa kuiita nchi yetu tulimozaliwa eti ni ya KUFIKIRIKA eti tu kwa kuwa wewe umezaliwa TANZANIA........
sasa aombe msamaha kwa lipi? UONGO UKO WAPI HAPO?
Basi tutajie ni sifa zipi zinazofanya nchi yetu iitwe Tanganyika!
 
yuko sahihi kabisa sema labda wewe ukilaza unakusumbua, kwanza inakubidi ujue sifa ya kuwa nchi ni nini!! kwasasa tanganyika ni nchi ya kufikirika tu yaani ukubali au ukatae!!

Wewe hata kusoma huwezi? Soma tena Title!!!
 
Msameheni yawezekana kalamu imeteleza ,,,,,, huyo ni mtu wa pwani anadhihirisha maneno yake ya kinywa chake mpaka kalamu imeteleza,,,,,,
 
Tanganyika kuwa nchi ya kufikirika liko wazi.

mto mada umesoma shule gani mkuu?
 
Tanganyika si ya kufikirika, bado ipo.
Watu kibao wanaitambua, mfano Medical Council of Tanganyika, Tanganyika Law Society, Tanganyika Farmers Association, n.k.
Ni nchi yenye mikoa 25 kwa sasa, mawaziri wasio wa mambo ya Muungano hushughulikia mambo ya Tanganyika tu(nyie mwaiita Tanzania bara, wkt kwa kusema bara mnaiondoa Mafia na ukanda wote wa Pwani toka Tanga hadi Mtwara kuwa si sehemu ya nchi ya Tanganyika!)
 
Tanganyika ni Nchini Fikirika!? mnajidanganya kweli. Tanganyika ipo ila imefunikiwa shuka la Tanzania, Nchi fikirika kwa sasa ni Zanzibar maana inajitahidi itambulike kama Chini kokote duniani imeshindikana kwa sababu ya ukoloni mambo leo unaoitwa Muungano chini ya shuka Tanzania.

Hili shuka Tanzania lazima liongolewe na Zanzibar irudishiwe uhuru wake kamili. Zanzibar ibaki kama zanzibar, Tanganyika kama Tanganyika na Muungano ambao kimsingi ni shirikisho ubaki pale ukiwa na mamlaka zake na taasisi zake zilizo chini ya Shirikisho.

Umewahi wapi kuona Rais wa chini upande mmoja wa chini ana mamlaka kamili upande mwingine wa Nchi mamlaka yake ya mipaka kwa zaidi ya 80% [JMK] Au umewahi wapi kuona Rais wa nchi hana mamlaka kwa Usalama na uchumi wa chini yake? [Dr Shein] Hivi Dr Shein lini ametoka Nje ya Zanzibar kuhudhuria japo economy forum japo iliofanyika Tanganyika (almaarufu Tanzania bara) sembuse hizo za Ulaya na Bara America. Au huwa anahudhuria lakini wananchi hatujui?

Siku sio nyingi sana Tanganyika itarudi, na nyie mnaosema ni fikirika ntayameza maneno yenu.
 
red = wewe ndo inabidi utuombe radhi kwa kukosea kuandika neno KUFIKIRIKA na badala yake umetukana kwa kuandika neno KUFIRIKA


Mkuu: Point taken. Nilikwisha gundua hilo kosa kwenye heading nikajaribu kusahihisha ikashindikana kwenye JF mobile. Niwaombe radhi kwa wote waliokwazika na kosa hilo.

Baada ya kusema hivyo narudi kwenye mada kuwa Tanganyika si ya kufikirika. USSR ilipovunjika nchi zilizokuwepo kwenye muungano zilirudi kwenye uhai wao kwa majina yao yale yale. Nchi ya kufikirika(imaginary)ni kwamba haijawahi kuwepo kabisa.

Neville Meena anasema yeye kazaliwa Tanzania na kwa sababu hiyo kwake Tanganyika haijawahi kuwepo. Na waliozaliwa Iliyokuwa Tanganyika anawambiaje?
 
Mkuu: Point taken. Nilikwisha gundua hilo kosa kwenye heading nikajaribu kusahihisha ikashindikana kwenye JF mobile. Niwaombe radhi kwa wote waliokwazika na kosa hilo. Baada ya kusema hivyo narudi kwenye mada kuwa Tanganyika si ya kufikirika. USSR ilipovunjika nchi zilizokuwepo kwenye muungano zilirudi kwenye uhai wao kwa majina yao yale yale. Nchi ya kufikirika(imaginary)ni kwamba haijawahi kuwepo kabisa. Neville Meena anasema yeye kazaliwa Tanzania na kwa sababu hiyo kwake Tanganyika haijawahi kuwepo. Na waliozaliwa Iliyokuwa Tanganyika anawambiaje?

It was just a light touch lakini context au maudhui ya thread safi. mie nimezaliwa Tanganyika mji mkongwe wa Singida
 
Tanganyika si ya kufikirika, bado ipo.
Watu kibao wanaitambua, mfano Medical Council of Tanganyika, Tanganyika Law Society, Tanganyika Farmers Association, n.k.
Ni nchi yenye mikoa 25 kwa sasa, mawaziri wasio wa mambo ya Muungano hushughulikia mambo ya Tanganyika tu(nyie mwaiita Tanzania bara, wkt kwa kusema bara mnaiondoa Mafia na ukanda wote wa Pwani toka Tanga hadi Mtwara kuwa si sehemu ya nchi ya Tanganyika!)

Kama kikwete ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kule zenji wana Rais wao, wewe unaedai Tanganyika ni nchi Rais wenu anaitwa nani?. Kama hakuna nyie ni wa kufikirika tu!
 
Tanganyika ilikufa tangu mwaka 1964, limebaki jina tu. Hivi wewe ukipewa jina la Babu yako aliyekufa inamaanisha kwamba huyo babu yako yu hai kwasababu tu ya hilo jina linalotajwa? Naunga mkono Tanganyika ni nchi ya kufikirika.
 
Ni kweli hii nchi TANGANYIKA ni ya kufikirika maana haipo tena. tuombwe radhi kwa lipi.
 
Kama kikwete ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kule zenji wana Rais wao, wewe unaedai Tanganyika ni nchi Rais wenu anaitwa nani?. Kama hakuna nyie ni wa kufikirika tu!

Nyie hamjui mambo haya.
Muungano ulipoanza, ilikubaliwa ziwepo serikali 2 na marais wawili, Zenji iwe na Rais wake na serikali yake, na Rais wa Serikali ya Muungano ndo awe pia Rais wa Nchi ya Tanganyika.

Na jambo hilo halijawahi kubadilishwa.
Kisichokuwepo kwa sasa ni serikali ya Tanganyika, ambapo jukum hilo la serikali limo mikononi mwa Serikali ya Muungano.
Nchi ya Tanganyika ipo, na mipaka yake iko dhahiri, na inaitawala nchi ya Zanzibar kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni,
ikiiachia mamlaka kidogo tu ya ndani.

Kama Nchi ya Tanganyika haipo, wazanzibar wanataka kuvunja Muungano na nani waliyeungana nae?
Waliungana na Tanzania ambayo haikuwepo?

Msinambie Zanzibar aliolewa na Tanganyika, kisha mtoto Tanzania alipozaliwa, babake Tanganyika akafa, kisha mtoto Tanzania akamrithi mjane ambaye ni mama yake na kumfanya mkewe, hivyo leo Zanzibar anadai talaka toka kwa mwanae badala ya mumewe ambaye leo mnamuita marehemu Tanganyika!

Mnanishangaza sana.
 
Na bendera yetu ina rangi 3, njano kijani na nyeusi.
Tena sisi tulijitawala km taifa la Tanganyika kwa miaka karibu mi3, wenzetu walijitawala kwa miezi mi3, tukatoa mahari, tukajitwalia mke, hd leo!
 
yuko sahihi kabisa sema labda wewe ukilaza unakusumbua, kwanza inakubidi ujue sifa ya kuwa nchi ni nini!! kwasasa tanganyika ni nchi ya kufikirika tu yaani ukubali au ukatae!!



Mkuu. Kuniita "kilaza" unakosea maana hunifahamu. Neno "kilaza" halikuwepo katika msamiati kwa sisi tuliozaliwa Tanganyika. Neno kilaza ni la kizazi chenu mnaonunua mitihani kuanzia primary mpaka chuo kikuu. Sisi tulifanya mitihani ya standard twelve na fourteen iliyotungwa kule Cambridge Uingereza na kusafirishwa kwa shirika la ndege la Uingereza liloitwa BOAC na baadae ilirudishwa huko huko kwenda kusahihishwa. Mitihani ya chuo kikuu ilikuwa ni ya University of Lomdon. A bit of history for you son!
 
Back
Top Bottom