Neville Meena ametutusi kuita Tanganyika nchi ya "KUFIKIRIKA"

Czechoslovakia or Czecho-Slovakia (Czech and Slovak: Československo, Česko-Slovensko) was a sovereign state in Central Europe which existed from October 1918, when it declared its independence from the Austro-Hungarian Empire, until 1992. From 1939 to 1945, the state did not de facto exist because of its forced division and partial incorporation into Nazi Germany, but the Czechoslovak government-in-exile nevertheless continued to exist during this period. In 1945, the eastern part of Carpathian Ruthenia was taken over by the Soviet Union. On 1 January 1993, Czechoslovakia peacefully split into the Czech Republic and Slovakia.
 
Neville Meena tuombe radhi wale wote tuliozaliwa TANGANYIKA kwa kuiita nchi yetu tulimozaliwa eti ni ya KUFIRIKA eti tu kwa kuwa wewe umezaliwa TANZANIA. ...
Kweli hili linaweza kuwa tusi!
 
Ninavyofahamu jina TANZANIA ni acronym ya majina mawili ya TANGANYIKA na ZANZIBAR yaani: TANZANIA = TANganyikaZANzibarNIA.
 
Nashangaa mnavyomshambulia aliyeanzisah uzi huu, Tanganyika ipo maadamu Tanzania ipo. Kwani katika mkataba wa Muungano inasomekaje? Zanzibar waliungana na nchi hewa? no Tanganyika haijafa maadamu kwenye mkataba wa muungano inasomeka kuwa Tanganyika imeungana na Zanzibar huwezi kuufuta ukweli kwa maneno mepesi ya kisiasa twendeni na facts jamani
sasa aombe msamaha kwa lipi? UONGO UKO WAPI HAPO?
Basi tutajie ni sifa zipi zinazofanya nchi yetu iitwe Tanganyika!
 
What is new kwenye hilo? He was right. Yes ya kufikirika. Ulitaka asemeje ungetusaidia kwa hilo au ungesahihisha kauli yake ingekuwa vema sana ili uwezo kutusaidia na wengine. Inabidi umfuate Mtikila muwe wote.
 
Nafikiri Neville Meena hajui kiswahili vyema na ukweli ni kwamba anatakiwa kuomba radhi umma wa Watanganyika;
UFAFANUZI
Nchi ya KUFIKIRIKA maana yake ni kwamba hiyo nchi haijawahi kuwepo kwenye uso wa dunia kitu ambacho sio kweli maana uingereza ilitoa uhuru kwa Tanganyika mwaka 1961 na baadae kuwa JAMHURI YA TANGANYIKA. Tanzania ilikuja baadae kabisa
Kwa hiyo Meena amekurupuka kwenye mada yake na anatakiwa awe makini kama mwandishi wa habari kabla ya kudiscuss issues sensitive kama hizi
 
Tanganyika ni Nchini Fikirika!? mnajidanganya kweli. Tanganyika ipo ila imefunikiwa shuka la Tanzania, Nchi fikirika kwa sasa ni Zanzibar maana inajitahidi itambulike kama Chini kokote duniani imeshindikana kwa sababu ya ukoloni mambo leo unaoitwa Muungano chini ya shuka Tanzania.

Hili shuka Tanzania lazima liongolewe na Zanzibar irudishiwe uhuru wake kamili. Zanzibar ibaki kama zanzibar, Tanganyika kama Tanganyika na Muungano ambao kimsingi ni shirikisho ubaki pale ukiwa na mamlaka zake na taasisi zake zilizo chini ya Shirikisho.

Umewahi wapi kuona Rais wa chini upande mmoja wa chini ana mamlaka kamili upande mwingine wa Nchi mamlaka yake ya mipaka kwa zaidi ya 80% [JMK] Au umewahi wapi kuona Rais wa nchi hana mamlaka kwa Usalama na uchumi wa chini yake? [Dr Shein] Hivi Dr Shein lini ametoka Nje ya Zanzibar kuhudhuria japo economy forum japo iliofanyika Tanganyika (almaarufu Tanzania bara) sembuse hizo za Ulaya na Bara America. Au huwa anahudhuria lakini wananchi hatujui?

Siku sio nyingi sana Tanganyika itarudi, na nyie mnaosema ni fikirika ntayameza maneno yenu.

Ndugu umeenda shule ukafika japo darasa la 7? Maneno uloyasema ni aibu kubwa, eti Zanzibar ndio ya kufikirika na sio tanganyika, tanganyika ipo kwa unavojidanganya! Duh! Haya hebu twambie katiba ya ya tanganyika imewekwa wapi? Rais wa tanganyika yuko wapi? Serikali ya tanganyika iko wapi? Wimbo wa taifa wa tanganyika uko wapi? Basi naomba angalau unitajie location ya bunge la tanganyika! Sasa ndo kaa ufikirie nani wa kufikiriwa, maana zanzibar ni semi-autonomous lakini tanganyika ni Zero-autonomous zaidi ya kutumia jina la Tanzania.
 
By the way, huyo anaekwenda katika economy forum anajulikana kama ni rais wa Taifa liitwalo Jamhuri ya watu wa Tanzania, hawajui kama kuna rais wa Tanganyika, hebu ntajie rais wa tanganyika anaitwa nani, sijawahi kumsikia rais wa JMT akiwa addresed as the president of tanganyika. Na unaonekana wewe mtu wa vijijini, kwani ulifikiri kikwete peke ake ndo anaenda ulaya na marekani? FYI President Amani Abeid Karume pamoja na kama zanzibar haina sovereignty lakini anatandikiwa Red carpet na anakuwa anatambulikana kama the president of Zanzibar, hata hao mliowauzia kigamboni akina Bush walikuwa wanamwita the Presudent of Zanzibar! Naomba unitajia jina la THE PRESIDENT OF TANGANYIKA, mi naona bora huyo Neville aombe radhi, na alikuwa aseme Tanganyika sio kitu cha kuingia akilini kabisa kwa sababu hakipo!
 
Hivi Tanzania na kabla ya Tanganyika ilikuwa inajulikana kwa jina gani? litafutwe liwe mbadala kwanza maana haya majina mawili yanatia kichefuchefu kwa kuleta vurugu; tutaishia kuenzi fikra na majina yaliyaanzishwa enzio pasikuwepo na faida yoyote!!!!!!!.
 
Hapo mwisho umejijibu mwenyewe! Tanganyika inatumia jina la Tanzania kuitawala Zanzibar!!!
Ndugu umeenda shule ukafika japo darasa la 7? Maneno uloyasema ni aibu kubwa, eti Zanzibar ndio ya kufikirika na sio tanganyika, tanganyika ipo kwa unavojidanganya! Duh! Haya hebu twambie katiba ya ya tanganyika imewekwa wapi? Rais wa tanganyika yuko wapi? Serikali ya tanganyika iko wapi? Wimbo wa taifa wa tanganyika uko wapi? Basi naomba angalau unitajie location ya bunge la tanganyika! Sasa ndo kaa ufikirie nani wa kufikiriwa, maana zanzibar ni semi-autonomous lakini tanganyika ni Zero-autonomous zaidi ya kutumia jina la Tanzania.
 
Tanganyika si ya kufikirika, bado ipo.
Watu kibao wanaitambua, mfano Medical Council of Tanganyika, Tanganyika Law Society, Tanganyika Farmers Association, n.k.
Ni nchi yenye mikoa 25 kwa sasa, mawaziri wasio wa mambo ya Muungano hushughulikia mambo ya Tanganyika tu(nyie mwaiita Tanzania bara, wkt kwa kusema bara mnaiondoa Mafia na ukanda wote wa Pwani toka Tanga hadi Mtwara kuwa si sehemu ya nchi ya Tanganyika!)

Haya uliyoandika ndio yanathibitisha kuwa Tanganyika ni nchi ya kusadikika....kuna mambo ya zanzibar na mambo ya muungano tu......kuna serikali ya zenji na serikali ya JMT tu......sasa iweje wizara ndani ya JMT eti inashughulikia mambo ya bara tu.......which is bara here? Rais wake....katiba yake....bunge lake?
 
Chilubi Tatizo lako kubwa ambalo hata huyo meena analo ni kuwa hamjua maana ya kufikirika. Wewe nafikiri kuwa Zanzibar ni nchi eti kwa vile tu ina katiba bendera na Wimbo wa Taifa. Ukweli unabaki pale pale tu kuwa endelea kufikiri kuwa zanzibar ni nchi lakini ki uhalisia sio nchi. Nchi gani ambayo haiwezi kujiamulia masuala yake ya kiuchumi? haiwezi kusimamia masuala yake ya amani na usalama? hiyo ni nchi fikirika tu wala sio nchi halisi. Kwenda USA akaitwa Rais wa zanzibar haimaanishi kuwa ni Rais wa Nchi. Ili kuitawala Zanzibar Tanganyika imebidi kuvaa Gamba la Tanzania ambalo tunataka livuliwe ili na Zanzibar liwe taifa huru lenye uwezo wa kujiamualia mambo yake. Leo hii zanzibar haina uwezo wa kuamua nani awe Rais wa Muungano, nguvu hiyo wanayo watanganyika maana Rais wao ndio rais wenu wa Muungano. Tanganyika sio ya kufikirika ipo na hata hiyo katiba ya Muungano ya Tanganyika ila iliongezewa vifungu ya kuibana Zanziar iwe chini ya Tanganyika kwa gamba Tanzania. kwanini katiba ya zanzibar haikutumika kuwa ya Muungano badala yake ikatumika ya Tanganyika? Chilubi tafakari kabla ya kuchangia mada
 
Tatizo la waandishi wetu hawajali kutumia maneno sahihi yeye meena kakurupuka tu na kuandika kufikirika bila kujua maana na ndio maana linaleta shida.Laiti angejua maana asinge litumia angetafuta neno ambalo lingefaa kuwa hapo
 
Tanganyika si ya kufikirika, bado ipo.
Watu kibao wanaitambua, mfano Medical Council of Tanganyika, Tanganyika Law Society, Tanganyika Farmers Association, n.k.
Ni nchi yenye mikoa 25 kwa sasa, mawaziri wasio wa mambo ya Muungano hushughulikia mambo ya Tanganyika tu(nyie mwaiita Tanzania bara, wkt kwa kusema bara mnaiondoa Mafia na ukanda wote wa Pwani toka Tanga hadi Mtwara kuwa si sehemu ya nchi ya Tanganyika!)

wanasheria, wafamasia na wote wa tasnia mbalimbali ktk ushirika wao hawataweza kuburuza umma wa watu ambao wanaweza kuamua kukataa kufungwa na maamuzi ya kikoloni ya kukusanywa ktk kitu kinachoitwa tanganyika....kigoma yetu si tanga na wala si nyika...ni kigoma!!!...kazi itakuwepo... mwenye kujua... (hata akiwa si "joni kisomo" ) hawezi kushabikia kuvunjika kwa muungano, na kuja kwa tanganyika.... atajua dhahiri kabisa katika makabila zaidi ya mia na ushee lazima kuna yatakayo taka haki ambayo zanzibar ilipewa ya kuamua mustakbala wake...tafakari...tahadhari
 
Nevile MEENA ni kichwa now I understand kwa nini alipewa tuzo ya heshima.
 
Back
Top Bottom