Neno "watanionaje" ndio linawafanya graduates wengi kuchagua kazi

Yohana469

JF-Expert Member
Feb 16, 2021
302
448
Habarini wanaJF,

nakumbuka kauli ya mgombea uraisi wa UKAWA 2015 Ndugu Edward Lowasa alotamka kuwa tatizo la ajira tusipokuwa makini litakuja kuwa bomu, sasa ni rasmi kauli yake imetimia. Kwa sasa ajira kwa wahitimu ishakuwa ngumu, tena baada miaka miwili au mitatu litakuwa kubwa zaidi. Kama ni bomu tunasema bomu la maangamizi yaani nyuklia. Wahitimu wengi watakuwa mitaani hawajui nn chakufanya.

Sasa ni wakati wahitimu kushtuka kujua wakati wa kuchagua kazi umekwisha ulikuwa kipindi hicho JK yupo madarakani,huyu bwana mkubwa ukichagua kazi kiukweli utakufa na njaa hata hela ya vocha utakosa.

Nimeshuhudia vijana wengi wahitimu wapo nyumbani hawaelewi kesho yao. Ukimuuliza anakwambia hakuna ajira, ukimwambia tufanye kazi hii anakwambia jirani au m2 fulani akiniona itakuaje yaani kama anaona aibu. Sasa m2 hafikirii huyo m2 anayemwonea aibu ana msaada gani kwake, hata akipata tatizo hawezi msaidia.

Yaani mhitimu yupo radhi ahame mkoa aende mbali na mkoa ili akafanye kazi ngumu aepuke aibu, wakati pale karibu akitumia fursa vizuri ataweka akiba na kujiajiri kwa sababu atakuwa hana majukumu mazito.

Sasa ni wakati wa kushtuka na kutokuchagua kazi na usimwonee aibu m2 ambaye hana msaada kwako .
 
Tatizo tumewaacha watu ambao kazi zao ni kubuni policy za kuongeza ajira na kuwatwika wananchi wenyewe kwamba ndio makosa yao.

Hizo kazi hata za kutokuchagua mkuu ni kwamba hazipo. Kujiajiri is for the few (inahitaji discipline wala sio elimu).

Kwahio ingekuwa rahisi kila mtu kujiajiri wote watoke huko walipo tuingie mtaani tujiajiri. Nchi yenye asset kama hii inageweza ku-create mifumo ya kusomba majority kufanya kile cha kufanya kulingana na skills zao, zile percent ndogo ndio zinge-create vitu vya kuajiri watu (sio kila mtu aingie mtaani na kufanya kitu).

Kwanza itafika wakati wa competition na "bigger fish eating a small fish.", hayo maduka yote ya mtaani yatashindwa ku-compete na wachache wenye mitaji na economy of scale, Pile it High, Sell it Cheap.
 
Tuliandaliwa kuajiriwa ila suala la kujiajiri ni uthubutu wa mtu mmoja mmoja
Tuliandaliwa kuajiriwa ila suala la kujiajiri ni uthubutu wa mtu mmoja mmoja

Tuliandaliwa kuajiriwa ila suala la kujiajiri ni uthubutu wa mtu mmoja mmoja
Mkuu tukisema tuliandaliwa kuajiriwa unajidanganya, fanya kitu kutokana na mazingira yaliyopo. Hakuna m2 alitegemea kama bwana mkubwa angeicontrol nchi namna hii kipindi anakabidhiwa madaraka 2015 November, kama hali iko hv lazima uende kutokana hali halisi, ndo cha msingi.
 
Mimi nipo upande wako
 
Ukishakua mtu mzima ukaachana na drama za ki-teenager na fake life utagundua kuishi kwa kuangalia flani atanionaje akinikuta nafanya kazi fulani ni element za immaturity

Sio kwamba nawa diss wanaochagua kazi hapana. Binafsi ni kiri kwamba ni mmoja wa watu ambao wanachagua kazi ila kwa criteria tofauti na hizo, hua nazingatia mazingira ya kiusalama ya hiyo kazi, uhalali, na maslahi kulingana na complex ya kazi husika

Nishafanya kazi ngumu zenye maslahi madogo ambayo ilinifanya niumwe, pesa niliyopata nikaishia kujiuguza hakuna cha maana nilichofanya

Nishawahi kwenda machimboni kuchimba dhahabu ilikua kila wiki lazima msiba utokee, mtu kufukiwa na gema au kulipukiwa na baruti ilikua kawaida

So katika mazingira hayo mtu akiniambia nachagua kazi it is fine for me, kwasababu siku ukiumwa msaada wake ni pole tu

Ila kuchagua kazi kwa kigezo kua flani atanionaje (nje ya hivyo vigezo hapo juu) hilo kweli ni tatizo
 
Uliwai kumwambia graduate fanya hii kazi nayeye akaona inafanyika na kuna resources zote za kufanyika akakwambia hivyo fulani atanionaje.

Huu ujinga wa kuandika kila kinachokuja kichwani ni ushamba sana.

OK, na wasio graduate wasio na kazi nao hawana kazi kwasababu wanasema fulani atanionaje??
 
πŸ†ƒπŸ†ƒπŸ…ΈπŸ†‰ πŸ…» πŸ…ΉπŸ…ΈπŸ† πŸ…½πŸ…Έ πŸ…ΆπŸ…»πŸ…» πŸ…ΈπŸ†‚πŸ†‚πŸ†„πŸ…΄ πŸ†‚πŸ…Έ πŸ†ƒπŸ…½πŸ†‰πŸ…½πŸ…Έ πŸ†ƒπŸ†„ ......πŸ†ƒπŸ†ƒπŸ…ΈπŸ†‰ πŸ…½πŸ…Έ πŸ…²πŸ†πŸ…½ ....πŸ…½ πŸ†„πŸ…»πŸ†ƒπŸ…ΈπŸ…½ πŸ…ΈπŸ…½πŸ…²πŸ†πŸ…΄πŸ†‚πŸ…΄
 
Watu ambao huwa mnapenda Kuwataka ( Kuwaambia ) hawa ( sisi ) Graduates kuwa wasichague Kazi na wafanye Kazi yoyote ( zozote ) kuna muda nawadharau na kuwaona hamna Akili ( yaani ni Wapumbavu ) wa Kifikra.

Hivi hawa Graduates mlipoteza muda wenu pamoja na Rasilimali Fedha zenu Kuwasomesha ( Kozi za Fani mbalimbali ) kwa Gharama Kubwa ndani na nje ya Nchi ili waje kufanya hizo Kazi zenu zozote?

Ni kwanini mnaacha Kujadili Mfumo mbovu wa Elimu ya Tanzania usiomuandaa Graduate kuwa pro active na kumtaka awe Tegemezi kwa Ajira za Maofisini huko Serikalini na Sekta binafsi? Kuna Graduate anayependa au kufurahia kuwa Jobless kama mnavyowaona? Mliofanikiwa acheni Unafiki kwa Kuona Wasomi wenzenu hawajitumi au hawapendi Kazi.

Sasa kama Wazazi kumbe huwa mnajua kuwa Watoto wenu ( zenu ) wanaweza Kufanya Kazi ( Ajira ) zozote hata za Kubeba Zege au Kumenya Viazi vya Chips kwanini tokea zamani hamkuwaambia wajikite huko ili wasipoteze muda wao wa Kusoma kwa miaka mingi huko Shuleni na Vyuoni?

Hivi Serikali ya Tanzania, Sera zake pamoja na Taasisi za Kibenki zingeweka Utaratibu wa Kuwakopesha Graduates kwa Riba nafuu leo wengi Wao wasingeweza Kujiajiri na Kulipunguza kwa Kiasi kikubwa tatizo la Ajira? Rasilimali za Tanzania zikitumika vyema zinaweza Kulipunguza hili tatizo ila Watanzania wengi tumejaa Unafiki na Kujisahau kwakuwa wengine walishafanikiwa na kuona Maisha wameshayapatia na shida Kwao itakuwa ni Historia.

Kwa sasa naomba niishie hapa Kwanza.
 
Kwa kifupi tu ni kwamba course nyingi haziwaandai per se watu kwenda mtaani kujiajiri na labda concept nzima ya β€œkujiajiri” haieleweki kwa watu wengi. The β€œhow to” ni shughuli pevu.

Ninawafahamu ndugu kadhaa walisoma sijui Sociology, Political Science, IT, Laws etc ila wapo tuu wanatafuta kazi tangu 2017. Kuna mmoja yeye alishtuka na kufungua Mgahawa wake na sasa anasogea mdogomdogo

Wengine wao wanasubiri ajira hata za TZS. 250,000/- kwa mwezi
 
Uliwai kumwambia graduate fanya hii kazi nayeye akaona inafanyika na kuna resources zote za kufanyika akakwambia hivyo fulani atanionaje.

Huu ujinga wa kuandika kila kinachokuja kichwani ni ushamba sana.

OK, na wasio graduate wasio na kazi nao hawana kazi kwasababu wanasema fulani atanionaje??
wapo
 
Kwanza hakuna bomu lolote litakalolipuka kutokana na wahitimu, wahitimu wengingi ni waoga balaa, kamwe hawawezi jitokeza barabarani hata kwa maandamano ya amani kuiomba serikali kuwafikiria, kama mtu anaogopa kufanya kazi fulani ili asionekane na fulani ni bora afe tu kwa njaa maana hana faida.
 
Tatizo tumewaacha watu ambao kazi zao ni kubuni policy za kuongeza ajira na kuwatwika wananchi wenyewe kwamba ndio makosa yao.

Hizo kazi hata za kutokuchagua mkuu ni kwamba hazipo. Kujiajiri is for the few (inahitaji discipline wala sio elimu).

Kwahio ingekuwa rahisi kila mtu kujiajiri wote watoke huko walipo tuingie mtaani tujiajiri. Nchi yenye asset kama hii inageweza ku-create mifumo ya kusomba majority kufanya kile cha kufanya kulingana na skills zao, zile percent ndogo ndio zinge-create vitu vya kuajiri watu (sio kila mtu aingie mtaani na kufanya kitu).

Kwanza itafika wakati wa competition na "bigger fish eating a small fish.", hayo maduka yote ya mtaani yatashindwa ku-compete na wachache wenye mitaji na economy of scale, Pile it High, Sell it Cheap.
Kuna watu wamejitoa katika kutekeleza majukumu yao halafu waathirika ndio wanaotupiwa mzigo wa lawama.
 
Tatizo ni kwamba watu ambao mlikwishapata kazi either kwa kuajiriwa or kujiajiri huwa mnaona kama graduates wengi walio mtaani ambao ni jobless kwamba hawana maana..NONSENSE..
 
Back
Top Bottom