Licha ya kuwa na vyuo na graduates wengi wa IT hapa Tz kwanini hakuna maajabu wanayofanya?

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,842
Wengi (sio wote)

Uzi huu wala sina nia ya kuwaponda bali naweka tu awareness ya hali halisi, off course watabe wa IT wapo waliohitimu vyuo ila ni.wachache sana ukilinganisha na wengi ambao ni amateurs ila tu kinachowabeba ni magamba (vyeti)

- IT, computer science, computer engineering, cyber security, data science, n.k kuna vyuo vinatoa hizi fani na wahitimu wapo wengi lakini sioni cha ajabu walichofanya hadi sasa.

Wengi huishia kujua kutumia internet bure ya vpn kwa kujaribu mafaili yaliyotengenezwa na wanaijeria, kuweka mods kwenye games, kushusha software / games / window zilizochakachuliwa, kucheza fifa kwenye ps, kupiga window, kudownload muvi kwa torrents, na vitu vingi ambavyo kiufupi creativity inayohusika ni ndogo,,, yaani happ anajiona anajua kila kitu kwenye pc, wakati kiuhalisia ni beginner.

Naona kuna graduates kibao sana wa haya mambo ila wengi huishia kusubiri kuomba ajira, kuhusu creativity, uvumbuzi ama ku innovate vitu naona bado sana.

Hata yule mtz alieuza system yake ya gesi kwa bilioni 50 sio graduate wa IT, alisomea mambo ya uhasibu ila alikuwa anafanya IT kama ujuzi binafsi.

Edit;

Wengi wanauliza nafanya shughuli ipi,

maelezo >> haya hapa <<
 
Wanajua ku burn CD
Hapo hakuna creativity yoyote maana watu tayari washaumiza vichwa kutengeneza hizo software za ku burn cd, wanao burn cd huwa ni watumiaji wa software ambayo imesharahisishwa kutumika, hakuna creativity yoyote hapo!! hata mtoto wa miaka sita especially kama anajua kiingereza unaweza kumfundisha kwa siku moja tu maana software imerahisisha matumizi
 
Ukiwa na muda usisite kupita kwenye huu uzi, utapata majibu yote👇

Mkuu wewe chuo umesoma Nini na umefanya kitu Gani mpaka sasa? Au hujasoma
Mimi ni fundi seremala, elimu niliishia form 4, kwenye mambo ya pc naweza kujiweka level ya mtumiaji wa kawaida na nashukuru lugha ya malkia hainipigi chenga.

vitu vya kawaida vilivyorahisishwa kwa kufata maelezo kama kupiga window, kuagiza vitu online, kusafisha ndani pc, kutengeneza sites kwa html / css, kushusha movies, kushusha software zilizochakachuliwa, kuchakachua modem, nk. Wala havinipi shida yoyote.

Shida inapokuja kuna IT wengine naona hata vitu basic kabisa vinawapiga chenga hadi nakosa majibu ya kinachofundishwa huko chuoni.

Kuna mhitimu wa kozi hizi alinunua pc mpya, ile ya zamani kuna mteja alitoa pesa aichukue, nikawa namshangaa ananyonya vitu kidogo kidogo vya pc ya zamani ili ahamishie kwenye pc mpya, nilimwambia afungue pc aweke hard disk ya laptop ya zamani kwenye pc mpya and vice versa, aliniambia hayo mambo hayajui, ilibidi nimsaidie vitu hivi basic kabisa akaishia kunishangaa sana.
 
Wanaweza kuchungulia kwenye akaunti zako za benki na kukomba Salio lako lote. Angalia wasije wakakukomoa.
 
- IT, computer science, computer engineering, cyber security, data science, kuna vyuo vinatoa hizi fani na wahitimu wapo wengi lakini sioni cha ajabu walichofanya hadi sasa

Naona kuna graduates kibao sana wa haya mambo ila wengi huishia kusubiri kuomba ajira, kuhusu creativity, uvumbuzi ama ku innovate vitu naona bado sana.

Hata yule mtz alieuza system yake ya gesi kwa bilioni 50 sio graduate wa IT, alisonea mambo ya uhasibu ila alikuwa anafanya IT kama ujuzi binafsi.
Tuanze na wewe kwenye kada yako umefanya Nini ama mmefanya Nini Cha kuishtua dunia ama mmeishia kukariri tu bila ya ku innovate yenu binafsi. Je ya hao mliyoyasoma mkapata karatasi zenu unadhani wao waliyajuaje walisomea wapi,Kama mgunduzi wa umeme alisomea wapi umeme ama gari?

Ama umeshiba na kisalali slip chako ambacho hakifiki $10000 ,unayo beibi woka,na ka three bedroom,na mbususu Kali unakula unajiona Kama wewe ndiye mjanja mno hapa duniani. Yaani Kama hapo Ni ego ndiyo inayokusumbua.

Baada ya stori kwa kukujibu kwa normal mind njoo Sasa niingie deep tujadili swali lako positively.

Nikujulishe kuwa tafiti nyingi mno zinategemea viwanda viwadhamini hao jamaa wafanya research na kuweza Kuja na innovation ya kuisdia dunia mfano yule dogo wa mpesa.

Pia kwa nchi zetu hizi masikini watu huwa tunasoma ili tuweze kujipatia living only yaani basic needs ndipo tunakuja kusubiria Ajira Mana unakuta wazazi Ni peasant,mama ntilie,wamachinga,wenye maduka ya kawaida ya kujipatia kula na kulala,wafugaji wa kawaida.

Unakuja kulinganisha na huko duniani mtt anazaliwa yeye anawaza kujulikana Mana kila kitu kipo kwao mkuu.

Ishu kubwa elewa ili mind ifanye innovation inabidi iwe katika Hali ya ku relax smt na hardship ,so inategemeana na kila mtu kuwa anakuwa motivated.

Elimu yetu pia ha encourage Innovation Bali katika kufaulu kupata alama za juu kabisa darasani na ndioiyo mindset tokea naseri Mana unasikia kuwa fulani Yuko vizuri amekuwa wa kwanza na sio kuwa akavumbua kitu fulani.

Kwa harakaharaka nimeishia hapo,hayo mengine inabidi niumize kichwa.

Ila elewa your or life is highly backed up with our own history or background mkuu.

Zaa watt mmoja akakulie USA,mmoja tz mmoja sauzi,mmoja uk,mmoja Saudi or uarabuni,.mmoja China Japan, mwingine India ama Indonesia na wa mwisho kabisa akakulia Kijiji chochote hapa Tanzania. Baada ya kuwa wamekuwa wakubwa above 35yrs wakutanishe waambie wote Ni watt wako ndio utajua Kama hujui.

Kama Kuna sehemu nime attack your ego,psyche and amygdala brain potezea kuwa strong emotionally.
 
Mimi ni fundi seremala, niliishia form 4 lakini kwenye mambo ya pc nipo nipo na nashukuru lugha ya malkia hainipigi chenga.

Hivi vitu vya kawaida kupiga window, kuagiza vitu online, kusafisha ndani pc, kutengeneza sites kwa html / css, kushusha movies, kushusha software zilizochakachuliwa, kuchakachua modem, nk. Wala havinipi shida yoyote, si haba kwangu.

Shida inapokuja kuna IT wengine naona hata kupiga window kunawapiga chenga hadi nakosa majibu
Wewe inaonekana una nature ya hizo Mambo ,na hapa ukipewa maujuzi kidogo utaenda mbali mno utakuja kuandika history kuwa alikuwaga seremala sahivi Ni it director American or world bank. Check Kama umri unaruhusu na uwezo wa mfukoni zama school ama somea online hizo kozi za it Ni PC yako tu umekaa ndani na internet unamaliza.
 
- IT, computer science, computer engineering, cyber security, data science, n.k kuna vyuo vinatoa hizi fani na wahitimu wapo wengi lakini sioni cha ajabu walichofanya hadi sasa.

Wengi huishia kujua kutumia internet bure ya vpn kwa kujaribu mafaili yaliyotengenezwa na wanaijeria, kuweka mods kwenye games, kushusha software / games / window zilizochakachuliwa, kucheza fifa kwenye ps, kupiga window, kudownload muvi kwa torrents, na vitu vingi ambavyo kiufupi creativity inayohusika ni ndogo,,, yaani happ anajiona anajua kila kitu kwenye pc, wakati kiuhalisia ni beginner.

Naona kuna graduates kibao sana wa haya mambo ila wengi huishia kusubiri kuomba ajira, kuhusu creativity, uvumbuzi ama ku innovate vitu naona bado sana.

Hata yule mtz alieuza system yake ya gesi kwa bilioni 50 sio graduate wa IT, alisonea mambo ya uhasibu ila alikuwa anafanya IT kama ujuzi binafsi.
Mleta Uzi , fanya analysis ya kutosha ili uje na vielelezo vilivyo kamilika, 👆hichi ulicho kiandika , kina mapungufu mengi Sana
 
Wengi (sio wote)

- IT, computer science, computer engineering, cyber security, data science, n.k kuna vyuo vinatoa hizi fani na wahitimu wapo wengi lakini sioni cha ajabu walichofanya hadi sasa.

Wengi huishia kujua kutumia internet bure ya vpn kwa kujaribu mafaili yaliyotengenezwa na wanaijeria, kuweka mods kwenye games, kushusha software / games / window zilizochakachuliwa, kucheza fifa kwenye ps, kupiga window, kudownload muvi kwa torrents, na vitu vingi ambavyo kiufupi creativity inayohusika ni ndogo,,, yaani happ anajiona anajua kila kitu kwenye pc, wakati kiuhalisia ni beginner.

Naona kuna graduates kibao sana wa haya mambo ila wengi huishia kusubiri kuomba ajira, kuhusu creativity, uvumbuzi ama ku innovate vitu naona bado sana.

Hata yule mtz alieuza system yake ya gesi kwa bilioni 50 sio graduate wa IT, alisomea mambo ya uhasibu ila alikuwa anafanya IT kama ujuzi binafsi.
Wasomi wote wa bongo wa fani zote wanasoma History tu hivyo usitegemee maajabu.
 
Wewe inaonekana una nature ya hizo Mambo ,na hapa ukipewa maujuzi kidogo utaenda mbali mno utakuja kuandika history kuwa alikuwaga seremala sahivi Ni it director American or world bank. Check Kama umri unaruhusu na uwezo wa mfukoni zama school ama somea online hizo kozi za it Ni PC yako tu umekaa ndani na internet unamaliza.
Unajua kitu ambacho nimegundua ni kwamba hata kwenye matumizi ya kawaida ya pc hapa bongo mtu anaweza kuonekana master hapa tz.

Mtu kavuja jasho na kaumiza kichwa kuchakachua window / game / software na kuiweka mtandaoni ili watu wadownload watumie bure, hapo sisi tunao download tunafata maelekezo yake kutumia hizo software bure wala hatuumizi kichwa, lakini mbongo anaweza kukuona bonge la mtaalam 😂😂

Binafsi kipimo changu cha IT alieiva ni creativity ya kubuni vitu, ku modify vitu, n.k. kadri apendavyo, hapa nazungumzia developers na programmers wazoefu wanaosababisha mambo sio sisi wazee wa kupakua.

Binafsi kwa vitu nafanya kiukweli hata baadhi ya IT wananiona konki lakini nashangaa maana nami huwa ni mtumiaji tu wa vilivyoandaliwa kwajili ya matumizi.
 
Kuna muda unakutana na foreman site za ujenzi Ni la saba Ila anajua vitu vya kitalaamu adi keep ujue. Huwezi mdanganya kitu ,sema tu mkiingia kwa karatasi anakimbia. Anafanya kwa kukariri sema Ile why hanayo
 
Hata kwa darasa la saba wengi tu ni hawa wajenzi wanaotujengea nyumba, nimewahi kwenda sehemu flani kuna ujenzi unaendelea wapo wanafunzinwa field kwenye vitendo bado wabichi sana wanafindishwa na hao hao darasa la saba, wanafunzi wengi walikuwa nondo kwenye makaratasi lakini kiutendaji ilibidi wawe wanafunzi upya.
 
Wapo watabe wa it ni wachache kuliko wanao iangusha tasnia
Na hawapewi nafasi,

Sijui hao IT wa Tanesco wanapokea mishahara ya kazi zipi, hivi imeshindikana kujaza umeme moja kwa moja baada ya kununua luku kwenye simu ? haya mambo ya kuingiza token yananishangaza.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom