Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 229
- 544
Siku za hivi karibuni hasa hasa kuanzia kipindi cha awamu ya tano ya "mwamba" ajira serikali zimekuwa ngumu sana hata kwa zile kada zinazo ajiri watu wengi kwa wakati mmoja kwa mfano nursing, daktari, walimu, kwenye majeshi n.k
Katika kufuatilia kwa ukaribu swala hili utetezi wa walioko kwenye vitengo husika (Utumishi) ni kwamba waombaji wamekuwa wengi sana sababu ambayo kwa "nje nje" inaonekana ni kweli
Lakini jaribu kufuatilia watu wanaopata hizo ajira utagundua kuwa hiyo sababu inatumika kuwachuja watu wasiojulikana, wasio na chochote, wasio na network yaani wapo wapo na vyeti vyao labda na uwezo wao ambao hawana sehemu ya kuuonyesha
1. Kama wewe huna kadi ya kijani ya chama cha kijani, endelea kusubiri Mwenyezi Mungu ashushe rehema zake
2. Kama wewe na wazazi wako hamna nyaya nyaya zilizounganika unganika na watu walioko kwa serikali wakubwa wakubwa au wadogo wadogo lakini wanaojua milango ya ofisi wanaohusika na ajira, kazana kufunga na kuomba usubiri miujiza
3. Kama wewe una kadi ya kijani ya chama cha siasa cha kijani halafu sio chawa na unajifanya unasimamia misimamo na hutaki kufuata wanachotaka wakubwa zako, nenda kakanyage mafuta ya Mwamposa usubiri miujiza
Tafuta watu unaowaamini hasa vijana walioko vyuoni kwa sasa waulize kwanini kuna trend kubwa sana ya vijana wa vyuo kujiunga na UVCCM na hawaachi kulipa ada za uanachama kielektronic? Ni kweli wanapenda siasa na wanapenda sera za chama hicho au kuna something behind? Kama anakupenda atakupa majibu sahihi
Vijana wa humu, ajira za serikali siku hizi haziendi kwa mtu tuu! Unaambiwa zinaenda kwa watu ambao tayari wapo kwenye data base yao na mwenyekiti wa Taifa (sio mwenyekiti "mkubwa" hapana, wa wadogo) ana nafasi kubwa ya kusema nani aende na nani asiende baada ya kupokea ripoti kwa wasaidizi wake anaowafahamu
Fuatilieni ajira za ualimu na kada ya afya zilizotoka mara ya mwisho angalia profile ya waliopata
Fuatilia wakati ule wa sensa angalia aina ya watu waliopata ile kazi
Najua kuna watu watakuja na mitazamo yao kuhusu hiki nilichoandika pengine na wengine wanaweza kudhani mimi ni mmoja wa wanaotaka "kuwashawishi" vijana kujiunga huko nilikotaja, lahasha! Najaribu kuwafumbua macho tuu!
Kuna wahitimu wa nursing, Doctars, Walimu wa mwaka 2015, 2016 na GPA zao nzuri tu za degree na diploma zao wako mtaani na wakati huo huo kuna wahitimu wa kozi kama hizo hizo wa mwaka 2019,2020, 2021 wako na check number zoa wanakula maisha serikalini. Ni vigezo gani hutumika kuwachuja hawa?? Fanyani ufuatiliaji mdogo tu mtajua ni kwanini
Mwisho
Tatizo hili la "ubaguzi" kwenye ajira haliwezi kumalizwa bila jobseekers kuonyesha hisia zao hadharani kwamba hili linakera
Vijana wa nchi hii amkeni!!!! Mmelala usingizi wa pono!!!
Kina Mwl. Nyerere, Mzee Mugabe, Mandela na wengine wote unaowajua waliopigania haki kutoka kwa wakoloni walifanya harakati hizo wakiwa vijana wabichi kabisa with the age of bellow 30!!
Waliweza kutetea haki zao kutoka kwa wakoloni wazungu pamoja na "udogo" wao, nyie sasa hivi mmeendekeza betting, mapenzi, mpira na ubishoo mkisubiri hao hao wanaowatenga wawatetee