Neno maalbino | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno maalbino

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Gamariel, Nov 26, 2009.

 1. Gamariel

  Gamariel Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  jamani naomba mnisaidie kiswahili fasaha juu ya wingi wa neno albino. Mara nyingi watu wamekuwa wakiwaita walemavu wa ngozi maalbino jambo ambalo kwa mtazamo wangu naona kama sio sahihi. Mfano mtu mwenye ngozi nyeupe huitwa mzungu na wingi wake huitwa wazungu, mtu mwenye ngozi nyeusi huitwa mwafrika na wingi wake huitwa waafrika. sasa kwanini albino asiitwe waalbino kwa wingi wake? nisaidieni
   
 2. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tumwite Mwalbino labda ndo wingi wake utakuwa Waalbino! Ni mawazo tu.
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Albino ni neno la kiingereza. Kiswahili chake ni zeruzeru, ingawa kwa sasa watu wanaamini ni jina linalodhalilisha (sijui ni kwa nini!). Neno zeruzeru kama ambavyo nimekuwa nikisikia linatumiwa halina wingi (angalia: "yule zeruzeru ni mkorofi" au "zeruzeru hawa ni wakarimu").
   
 4. m

  macinkus JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kuna maneno mengi ya kiingereza yanatumika badala ya kiswahili kuonyesha u-mambo leo kwa mfano nguo ya kutungua dukani inaitwa "ready made". Nyerere alieleza kwamba hata kwa kiingereza, umamboleo upo kwa kuacha neno la kiingreza na kutumia la kigeni na alitoa mfano wa mswahili kuitwa "rat catcher" kwa mkamata panya na mzungu anayefanya kazi hiyo hiyo kuitwa "rodent officer"! Nadhani ni ustaarabu zaidi kuwaita zeruzeru "albino".

  macinkus
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Kwa uelewa wangu mdogo wa lugha, mimi nadhani maalbino ndio uwingi wa albino.
   
 6. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Sio kweli mtu mwenye ngozi nyeusi anaitwa Mwaafrika, je na mmarekani mweusi utamwita mwaafrika, au ukienda india kuna wahindi weusi hao nao ni waafrika.?
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hii inapnyesha dhahiri kuwa hii lugha yetu ina mapungufu. kwa nini wapende kuitwa albino? zeruzeru linadhalilisha vipi? wakati mwingine ni kujikweza tu kusiko na maana, ila tukubaliane nao tu. tuwaite maalbino
   
 8. nzalendo

  nzalendo JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,875
  Likes Received: 2,680
  Trophy Points: 280
  kiswahili cha albino ni ''tupinkele'' ;-----baraza la kiswahili liko wapi?
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  'Tupinkele'! Inawezekana, ingawa binafsi sijawahi kusikia likitumiwa na wazungumzaji wa kiswahili wa Tanzania kumaaninsha 'albino'. Mara chache sana nimesikia likitumika kumaanisha wageni!

  Au ni neno jipya limebuniwa na BAKITA kuchukua nafsi ya zeruzeru ambalo halitumiki?
   
 10. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,364
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Acha uongo wewe,sio wote wenyengozi nyeupe huitwa wazungu,mbona wahindi,waarabu wote wanangozi nyeupe lakini hatuwaiti wazungu,hata wachina hatuwaiti wazungu?
   
 11. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,535
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Kuna njia mbalimbali kuonyesha uwingi katika sarufi ya Kiswahili.

  Watu hutajwa mara nyingi kwa maneno yanayoonyesha mwanzoni "M" kwa umoja na "WA" kwa uwingi. Lakini si maneno yote kwa watu yaliyopo katika kundi hili.

  Kuna maneno yanayoonekana kama maneno yenye asili ya kigeni na haya yamo kwenye kundi tofauti. Umoja hauna "M" mbele lakini uwingi huonekana kwa "MA"

  Mifano: daktari - madaktari; profesa - maprofesa, dereva - madereva
  Hivyo ndivyo albino - maalbino

  (swali la neno sahihi tuache kando. Hili ni idara ya msamiati halafu msamiati na sarufi ni mikono tofauti ya elimu ya lugha)
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Dec 6, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Maneno mengi yalibadilishwa jinsi ya kuwaita walemavu miaka ile ya '80' kama sikosei.

  Wataalam wa lugha na wapigania haki waliona kuwa Kumwita mtu kwa kupitia ulemavu wake ni kumdhalilisha, mfano neno Kilema (Vilema) ni mtu aliyepata ulemavu baada ya kuzaliwa (hakuzaliwa mlemavu).

  Mf:
  Badala ya kutumia neno Kilema tunashauriwa kuumia neno Mlemavu.

  K/Vipofu= M/Walemavu wa mcho, (asiye ona).

  K/Visiwi = M/Walemavu wa kusikia, wasio weza kusikia.

  K/Vilema (K/Viungo) = Mlemavu wa Viungo.

  Zeruzeru = Wenye ulemavu wa Ngozi (Albino).

  Ushauri ni kwamba tuwaite vile wenyewe wataona kuwa ni sawa.
   
 13. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mazeruzeru, au
   
 14. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Alibino sio neno la kiswahili, kwahiyo huwezi kupata neno fasaha lakiswahili kupata wingi wake!
  Labda utafsiri kwanza: Zeruzeru
  Hakuna wingi wa neno zeruzeru, ni sawa na neno mbuzi au Ng'ombe (maneno haya hayana wingi)
   
Loading...