Ujanja ndio Akili

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Ngoja nikwambie kitu. Hii dunia huwa ina siri kubwa sana, na kamwe usimwamini mtu hata kama anakuongozaga ibada sehemu ya kusali. Hii dunia ina watu wajinga na wajanja, wajinga ni asilimia tisini na wajanja ni asilimia kumi.

Kwenye hao kumi pia wametofautiana. Asilimia saba ni wale ambao hawataki kabisa kupelekeshwa na asilimia tatu ni wale ambao wanawapelekesha wajinga wa asilimia tisini wanavyotaka wao.

Unaweza kuwa msomi mkubwa, una maPhD yako ya kumwaga lakini ukifika mahali fulani unakuwa miongoni mwa wajinga. Mzee wa miaka hamsini ama sabini hata akiniambia ana PhD wala simuogopi kwa sababu pia anawezekana kuwa miongoni mwa wajinga.

Maofisini mwetu hao wazee ndiyo wanasumbua sana. Dunia ya sasa hivi kuiongoza haitakiwi uwe na elimu kubwa sana, ila unatakiwa kuwa mjanja wa kujua mambo. Watu wenye elimu kubwa wanazidi kudidimia chini, wale wajanja wanazidi tu kusonga mbele.

Leo si ajabu ukamuona kijana mwenye digrii anasota mtaani huku kijana wa darasa la saba anakula bata sana na mafanikio kibao. Kwa nini? Ni kwa sababu maisha ya sasa hivi, kuna wakati ili ufanikiwe unatakiwa kuwa mjanja.

Ukimuona mtu ana elimu yake halafu mjanja, muheshimu sana. Watu wengi wenye elimu huwa wapumbavu mitaani. Tunawaona, wanahisi elimu inaweza kuwa mkombozi wa kila kitu, kumbe kuna mahali ukifika, elimu yako unaiweka kwenye kistuli, halafu unaingia wewe kama wewe. Tunataka tuone kichwa chako bila ile digrii huwa inakuwaje?

Wasomi wengi ukiwaondolea Diploma, Digrii ama PhD zao wanakuwa wajinga, hawawi wajanja. Kuna kipindi niliwahi kusema kwamba nchi ikiwa na wazee wengi, haiwezi kuendelea hata kidogo, yaani tutakuwa tunapiga hatua tano mbele na kumi kupiga nyuma.

Ukimwangalia Doto Magari, hana elimu ila ni mjanja tu wa mtaani, kupitia ujanja wake, anatengeneza pesa, kupitia ujanja wake, leo ametuacha mbali tunajiita wasomi. Ukimwangalia Mwijaku, ni msomi mkubwa ila amefika sehemu, ule usomi wake ameuweka pembeni.

Kuna mwingine atasema yule chawa, lakini ndiyo anaishi kwa kupitia uchawa wake. Kuna yule mshikaji wa Buster Rhymes, naye alikuwa chawa, akaenda na uchawa mwisho wa siku naye akaanza kutengeneza pesa, na ngoma nyingi akaanza kushirikishwa.

Hii dunia inatakiwa kuwa na akili. Dunia inawatengenezea pesa wajanja na kuwaacha wenye elimu. Ili mambo yako yasonge, inatakiwa kwanza uwe umezungukwa na wajinga wengi. Nchi kama Nigeria ni vigumu kuingoza kwa sababu watu wengi wamesoma na ni wajanja.

Hapa kumbuka jambo moja. Unaweza kusoma na ukawa mjinga. Kwa Nigeria, watu wamesoma halafu ni wajanja. Wao wanaidhihirishia dunia kwamba ni wajanja na hawawezi kuwa wajinga hata siku moja, ndiyo maana ile nchi kuiongoza ngumu sana.

Watu wengi wenye nguvu kwenye dunia hii, wanawatumia watu wachache tu kupeleka taarifa kwa wajinga, zikishafika kwa hao wajinga, na kwa sababu ni wengi, basi wanafanikiwa kwa kile wanachokitaka.

Kila mtu huwa mjinga mahali fulani na mjanja mahali fulani. Ila kuna watu wanakuwa wajinga mahali pote na wajanja mahali pote. Hii dunia ukitaka kuiongoza, cha kwanza unatakiwa kuwa mjanja. Wazungu wanatupiga gepu hapo tu.

Wao wamesoma halafu ni wajanja, sisi hatujasoma kama wao, halafu tuna ujinga mwingi. Leo ni rahisi tu kumuona John anamchukia Juma kwa sababu tu si mtu wa dini yake. Hawa watu wakishachukiana, wale wajanja kupitia chuki hizo, wanazigeuza kuwa mtaji na kupiga pesa.

Wajanja wanaamua tu kumwambia Edward kwamba utaanza kuitwa Majeed, tutakupeleka madrasa, utasoma, utaijua kurani, utajifunza mengi kuhusu dini hiyo kwa kuwa kuna mahali tunataka tukutumie kuhakikisha tunafanikiwa kwenye mambo yetu, na kweli wanamtumia.

Kila mtu unayemuona duniani hapa, hasa mtu mkubwa anatengenezwa. Kuna wachungaji wa kutengenezwa, kuna mashehe wa kutengenezwa. Kuna wajanja waliamua tu kuwatengeza ili baadaye wafanye mambo yao. Kuna kitu kikubwa hapa kimejificha.

Zamani hii mbinu walikuwa wanaitumia sana CIA. Wanamtengeneza mtu kama shehe, anakuja msikitini, anaswali, mnakuwa naye hata kwa miezi sita, mnamuona mwenzenu, na kwa sababu mna umasikini, yule mtu wakati wa mfungo wa Ramadhani akiwapa tende tu kila siku, sasa mnaona kama nabii ameshuka, kumbe yupo kwa mpango fulani, baada ya kukamilisha kazi yake, yule shehe haonekani tena. Anapeleka ripoti mahali fulani kuhusu nyie.

Si kwa hao tu. Watu wanamtengeneza mpaka mchungaji. Unaona matangazo mchungaji mkubwa anakuja kutoka Marekani, huyo mchungaji noma. Zinatengenezwa clips za uongo, anaonyeshwa anavyokemea mapepo, watu mnamuamini, mchungaji anakuja nchini, anatangaza neno, kumbe nyuma ya pazia wapo wajanja kadhaa, wamefanya hilo kwa ajili ya manufaa yao.

Wajanja wanaanzisha ajenda za kuhusu machoko, halafu wanakupa wewe mjinga mmoja pesa nyingi kutangaza sera zao, na kwa sababu ni mjinga, halafu masikini, unajikuta ukiingia kwenye mitego yao. Wanakwambia hatuwezi kuwasaidia kama hamsapoti hiki kitu. Hapo wamekaa wajanja fulani, wanataka mambo yao yaende sawa, kwa kutumia akili zao, pesa zao, wanaanza kukupelekesha wewe bila kujua.

Wajanja wengi wanapatikana kwenye hizi taasisi za kishetani. Ukijifanya mjanja kutaka kuwashtukia, wanakumaliza. Wakikuona una akili sana na ushawishi, wanakuteka, unapelekwa mahali ambapo tayari mtu kama wewe amekwishatengenezwa, ukifikishwa huko kumbukumbu zako anapewa huyo, unauawa halafu maisha yako anaanza kuishi mtu mwingine mwenye mfanano wako.

Mjanja kabla ya kumuingia mjinga, kwanza anaangalia una uhitaji gani. Anasimamia kwenye uhitaji wako, mwisho wa siku anapitisha ajenda zake kupitia wewe. Michael Jackson alikuwa mmoja wa wajinga, watu wakamtumia kupitisha ajenda zao, mwisho wa siku anakuja kugundua ilikuwa too late, mwisho tu alibaki kusema Sony ni mashetani.

Wakoloni walipokuja Afrika waliona kabisa kwamba sisi ni wajinga, walihitaji vitu vingi kutoka kwetu, na kwa sababu tulikuwa na dini zetu, kitu cha kwanza ilikuwa ni kuziua na kutupa dini zao. Wakafanikiwa, tukawapa vioo, dhahabu halafu wao wakatupa vitabu vyao vya dini, vikatutisha sana.

Unavisoma vitabu hivyo unaambiwa mitume yote ya zamani ilikuwa ni ya Kizungu ama Kiarabu. Kwa maana Mungu hakutaka kabisa kutuangalia watu weusi, yaani hata kupitia vitabu vyao vikaonyesha kwamba watu weusi ni takataka, yaani Mungu huyuhuyu tunayemuabudu aliona mitume wote wanatakiwa kuwa Wazungu na Waarabu.

Dunia ina siri kubwa sana. Kuna siku niliwaambia kuna watu wanamjua Mungu wa kweli ni yupi, inawezekana huyo Mungu unayemuabudu si Mungu wa kweli. Kuna siri ambazo zimefichwa sana. Hizi siri ukitaka kuzichimbua, viongozi wa dini wanakwambia usichimbue, unamkosea Mungu.

Kuna mtu aliniuliza: “Mhaya, kwa nini unamzungumzia Mungu wa watu? Wenu yupo wapi?”

Akiwa na maana kwamba unasoma Biblia unakutana na Mungu wa Israel, unasoma unakutana na Mungu wa Kiarabu. Yaani unaambiwa Waarabu walifanya hivi na vile, inamaana hawa Wazungu na Waarabu walikutana na Mungu wa kweli, sisi tukashindwa kukutana naye na kuanza kumwabudu Mungu wao? Hayo maswali jijibu mwenyewe tu.

Hii dunia imezungukwa na wajanja sana. Hawa wajanja wanaitawala dunia kwenye nyanja mbalimbali, elimu, biashara mpaka dini. Na niliwahi kukwambia kwamba hata siku zetu za kuabudu walizipanga wao. Yaani wao na miungu yao wakakupangia siku za kuabudu.

Ukisoma vitabu vya dini, vinawazungumzia wao tu na miungu yao, haiwazungumzii watu weusi. Ukiuliza nabii fulani na mitume, unaambiwa walikuwa Waarabu ama Wazungu, Waafrika wapo wapi?

Haohao watu wakaweka vitu vyeusi tu ndiyo vinakuwa vibaya. Shetani hachorwi kama Muarabu ama Mzungu, lazima awekewe ngozi nyeusi. Unasikia tu mchawi anavaa kaniki nyeusi akiroga. Mtu akizikwa kwa sababu anakwenda kwa Mungu, tunamingirisha kwenye sanda nyeupe. Yaani mchawi...kaniki nyeusi....sanda nyeupe.

Malaika wote unaowajua wewe, ukichorewa unaonyeshwa ni Wazungu...hakuna malaika mweusi. Vitu vyote vibaya vina rangi nyeusi, na vyote vizuri vina rangi nyeupe. Vitu vya hatari ambavyo si salama, rangi nyeusi, ila vile salama vyote ni rangi nyeupe.

Mavazi ya watu wanaoabudu shetani huwa meusi, hawavai meupe. Yaani hii rangi yetu ilianza kubaguliwa kuanzia kwenye hvyohivyo vitabu.

Leo ukimchora Yesu mweusi ama mitume, watu watakushangaa, ila ukimchora shetani mweusi, hata yule Saidi wa Mbagala atakuona upo sahihi. Yaani tayari hata sisi tayari wajanja washatupatia kwa kutukubalisha kwamba vizuri ni vyeupe, vibaya ni vyeusi.

Ukimchora shetani mweupe tu...ndugu yangu utatafutwa...ila ukimchora mweusi...mbona freshi tu, utaambiwa ndiyo ngozi yake.
 
Chuki dhidi ya Waarabu na Wazungu haiwezi kukusaidia, na wala haina mantiki.

Wapo Wafrika ni wakatili hao kuliko hata unaodhani.

Mwanadamu ni mwanadamu tu. Kwani wa ngozi nyeusi na wa ngozi nyeupe tofauti nini?

Mbona hata sie weusi tunatofautiana rangi - kuna weusi tii, maji ya kunde, chocolate, nk.

Kiasili mwanadamu asiyemcha Mungu na kumwamini kwa dhati ni mbinafsi na mbaguzi, bila kujali anatoka Ulaya, China, Afrika au Marekani, bila kujali imani, dini, hali ya kifedha nk.

Bottomline: mwanadamu ni yuleyule.

Thank God for the true religion that transcends all these social, political, economic, geographical and even religious stereotypes.
 
Huu uzi ungekuwa mzuri kama ungekuwa specific, mimi nimeusoma wote , umeanza vizuri kabisa lakini ukachanganya na udini , (ukabagua hadhira) mtu alikuwa anausoma kwa amani tu ili ajifunze wewe ukachanganya tena na maswala ya dini, sasa hadi tunashindwa ni kipi tudiscuss maana ushachanganya topics. Jifunze kuwa specific.
 
Chuki dhidi ya Waarabu na Wazungu haiwezi kukusaidia, na wala haina mantiki.

Wapo Wafrika ni wakatili hao kuliko hata unaodhani.

Mwanadamu ni mwanadamu tu. Kwani wa ngozi nyeusi na wa ngozi nyeupe tofauti nini?

Mbona hata sie weusi tunatofautiana rangi - kuna weusi tii, maji ya kunde, chocolate, nk.

Kiasili mwanadamu asiyemcha Mungu na kumwamini kwa dhati ni mbinafsi na mbaguzi, bila kujali anatoka Ulaya, China, Afrika au Marekani, bila kujali imani, dini, hali ya kifedha nk.

Bottomline: mwanadamu ni yuleyule.

Thank God for the true religion that transcends all these social, political, economic, geographical and even religious stereotypes.
Jamaa huwa anaharibu nyuzi zake kwa chuki zake tu hata kama ana hoja ya msingi ataanza kuleta mambo hayaeleweki tena.
 
Ungekuwa na akili ungejua kubalance kwa nyuzi zako kadhaa huko nyuma.

Sasa kama wasomi wajinga na maprofessor uchwara wasio na faida yaani washamba ni watu wa kwenu..

Hamna ujanja nje ya kukariri ndio mmeifikisha nchi hapa kwa kifupi hamna jipya wala hamna cha maana ,zaidi ni sifa tu za kishamba .

Moja ya jamii za kishamba ni nyie na elimu haina jipya maana ipo kweny vichwa vya wendawazimu....Mtaongozwa na CCM wazee wa lumumba wale elimu kidogo ila ujanja mwingi.
 
Umeanza vizuri katikati hapo ndio umeharibu kuanza story za kwenye kahawa kuwa tuliyemuona leo si makamo wa Rais ni saut tu imeigwa na mtu kavaa mfano wa sura yake
 
Ungekuwa na akili ungejua kubalance kwa nyuzi zako kadhaa huko nyuma.

Sasa kama wasomi wajinga na maprofessor uchwara wasio na faida yaani washamba ni watu wa kwenu..

Hamna ujanja nje ya kukariri ndio mmeifikisha nchi hapa kwa kifupi hamna jipya wala hamna cha maana ,zaidi ni sifa tu za kishamba .

Moja ya jamii za kishamba ni nyie na elimu haina jipya maana ipo kweny vichwa vya wendawazimu....Mtaongozwa na CCM wazee wa lumumba wale elimu kidogo ila ujanja mwingi.
Wewe na Kabila lako mmeifikisha Nchi wapi?

Punguza makasiriko nanii
 
Makasiriko gani ? Wakati nyie washamba ndio maana nchi haiwezi kuendelea ...Hao maprofessor wenu ushamba mwingi na akili za kizamani.

Huo husomi wenu mmefanya mapinduzi gani ,ni kwamba nyie washamba na tunawaona mabayo tu hamna jipya .

Ndio maana hamjui kujiongeza na ujinga wenu hata mambo ynayoendelea duniani hamjua mpo kama wewe.
 
Ngoja nikwambie kitu. Hii dunia huwa ina siri kubwa sana, na kamwe usimwamini mtu hata kama anakuongozaga ibada sehemu ya kusali. Hii dunia ina watu wajinga na wajanja, wajinga ni asilimia tisini na wajanja ni asilimia kumi.

Kwenye hao kumi pia wametofautiana. Asilimia saba ni wale ambao hawataki kabisa kupelekeshwa na asilimia tatu ni wale ambao wanawapelekesha wajinga wa asilimia tisini wanavyotaka wao.

Unaweza kuwa msomi mkubwa, una maPhD yako ya kumwaga lakini ukifika mahali fulani unakuwa miongoni mwa wajinga. Mzee wa miaka hamsini ama sabini hata akiniambia ana PhD wala simuogopi kwa sababu pia anawezekana kuwa miongoni mwa wajinga.

Maofisini mwetu hao wazee ndiyo wanasumbua sana. Dunia ya sasa hivi kuiongoza haitakiwi uwe na elimu kubwa sana, ila unatakiwa kuwa mjanja wa kujua mambo. Watu wenye elimu kubwa wanazidi kudidimia chini, wale wajanja wanazidi tu kusonga mbele.

Leo si ajabu ukamuona kijana mwenye digrii anasota mtaani huku kijana wa darasa la saba anakula bata sana na mafanikio kibao. Kwa nini? Ni kwa sababu maisha ya sasa hivi, kuna wakati ili ufanikiwe unatakiwa kuwa mjanja.

Ukimuona mtu ana elimu yake halafu mjanja, muheshimu sana. Watu wengi wenye elimu huwa wapumbavu mitaani. Tunawaona, wanahisi elimu inaweza kuwa mkombozi wa kila kitu, kumbe kuna mahali ukifika, elimu yako unaiweka kwenye kistuli, halafu unaingia wewe kama wewe. Tunataka tuone kichwa chako bila ile digrii huwa inakuwaje?

Wasomi wengi ukiwaondolea Diploma, Digrii ama PhD zao wanakuwa wajinga, hawawi wajanja. Kuna kipindi niliwahi kusema kwamba nchi ikiwa na wazee wengi, haiwezi kuendelea hata kidogo, yaani tutakuwa tunapiga hatua tano mbele na kumi kupiga nyuma.

Ukimwangalia Doto Magari, hana elimu ila ni mjanja tu wa mtaani, kupitia ujanja wake, anatengeneza pesa, kupitia ujanja wake, leo ametuacha mbali tunajiita wasomi. Ukimwangalia Mwijaku, ni msomi mkubwa ila amefika sehemu, ule usomi wake ameuweka pembeni.

Kuna mwingine atasema yule chawa, lakini ndiyo anaishi kwa kupitia uchawa wake. Kuna yule mshikaji wa Buster Rhymes, naye alikuwa chawa, akaenda na uchawa mwisho wa siku naye akaanza kutengeneza pesa, na ngoma nyingi akaanza kushirikishwa.

Hii dunia inatakiwa kuwa na akili. Dunia inawatengenezea pesa wajanja na kuwaacha wenye elimu. Ili mambo yako yasonge, inatakiwa kwanza uwe umezungukwa na wajinga wengi. Nchi kama Nigeria ni vigumu kuingoza kwa sababu watu wengi wamesoma na ni wajanja.

Hapa kumbuka jambo moja. Unaweza kusoma na ukawa mjinga. Kwa Nigeria, watu wamesoma halafu ni wajanja. Wao wanaidhihirishia dunia kwamba ni wajanja na hawawezi kuwa wajinga hata siku moja, ndiyo maana ile nchi kuiongoza ngumu sana.

Watu wengi wenye nguvu kwenye dunia hii, wanawatumia watu wachache tu kupeleka taarifa kwa wajinga, zikishafika kwa hao wajinga, na kwa sababu ni wengi, basi wanafanikiwa kwa kile wanachokitaka.

Kila mtu huwa mjinga mahali fulani na mjanja mahali fulani. Ila kuna watu wanakuwa wajinga mahali pote na wajanja mahali pote. Hii dunia ukitaka kuiongoza, cha kwanza unatakiwa kuwa mjanja. Wazungu wanatupiga gepu hapo tu.

Wao wamesoma halafu ni wajanja, sisi hatujasoma kama wao, halafu tuna ujinga mwingi. Leo ni rahisi tu kumuona John anamchukia Juma kwa sababu tu si mtu wa dini yake. Hawa watu wakishachukiana, wale wajanja kupitia chuki hizo, wanazigeuza kuwa mtaji na kupiga pesa.

Wajanja wanaamua tu kumwambia Edward kwamba utaanza kuitwa Majeed, tutakupeleka madrasa, utasoma, utaijua kurani, utajifunza mengi kuhusu dini hiyo kwa kuwa kuna mahali tunataka tukutumie kuhakikisha tunafanikiwa kwenye mambo yetu, na kweli wanamtumia.

Kila mtu unayemuona duniani hapa, hasa mtu mkubwa anatengenezwa. Kuna wachungaji wa kutengenezwa, kuna mashehe wa kutengenezwa. Kuna wajanja waliamua tu kuwatengeza ili baadaye wafanye mambo yao. Kuna kitu kikubwa hapa kimejificha.

Zamani hii mbinu walikuwa wanaitumia sana CIA. Wanamtengeneza mtu kama shehe, anakuja msikitini, anaswali, mnakuwa naye hata kwa miezi sita, mnamuona mwenzenu, na kwa sababu mna umasikini, yule mtu wakati wa mfungo wa Ramadhani akiwapa tende tu kila siku, sasa mnaona kama nabii ameshuka, kumbe yupo kwa mpango fulani, baada ya kukamilisha kazi yake, yule shehe haonekani tena. Anapeleka ripoti mahali fulani kuhusu nyie.

Si kwa hao tu. Watu wanamtengeneza mpaka mchungaji. Unaona matangazo mchungaji mkubwa anakuja kutoka Marekani, huyo mchungaji noma. Zinatengenezwa clips za uongo, anaonyeshwa anavyokemea mapepo, watu mnamuamini, mchungaji anakuja nchini, anatangaza neno, kumbe nyuma ya pazia wapo wajanja kadhaa, wamefanya hilo kwa ajili ya manufaa yao.

Wajanja wanaanzisha ajenda za kuhusu machoko, halafu wanakupa wewe mjinga mmoja pesa nyingi kutangaza sera zao, na kwa sababu ni mjinga, halafu masikini, unajikuta ukiingia kwenye mitego yao. Wanakwambia hatuwezi kuwasaidia kama hamsapoti hiki kitu. Hapo wamekaa wajanja fulani, wanataka mambo yao yaende sawa, kwa kutumia akili zao, pesa zao, wanaanza kukupelekesha wewe bila kujua.

Wajanja wengi wanapatikana kwenye hizi taasisi za kishetani. Ukijifanya mjanja kutaka kuwashtukia, wanakumaliza. Wakikuona una akili sana na ushawishi, wanakuteka, unapelekwa mahali ambapo tayari mtu kama wewe amekwishatengenezwa, ukifikishwa huko kumbukumbu zako anapewa huyo, unauawa halafu maisha yako anaanza kuishi mtu mwingine mwenye mfanano wako.

Mjanja kabla ya kumuingia mjinga, kwanza anaangalia una uhitaji gani. Anasimamia kwenye uhitaji wako, mwisho wa siku anapitisha ajenda zake kupitia wewe. Michael Jackson alikuwa mmoja wa wajinga, watu wakamtumia kupitisha ajenda zao, mwisho wa siku anakuja kugundua ilikuwa too late, mwisho tu alibaki kusema Sony ni mashetani.

Wakoloni walipokuja Afrika waliona kabisa kwamba sisi ni wajinga, walihitaji vitu vingi kutoka kwetu, na kwa sababu tulikuwa na dini zetu, kitu cha kwanza ilikuwa ni kuziua na kutupa dini zao. Wakafanikiwa, tukawapa vioo, dhahabu halafu wao wakatupa vitabu vyao vya dini, vikatutisha sana.

Unavisoma vitabu hivyo unaambiwa mitume yote ya zamani ilikuwa ni ya Kizungu ama Kiarabu. Kwa maana Mungu hakutaka kabisa kutuangalia watu weusi, yaani hata kupitia vitabu vyao vikaonyesha kwamba watu weusi ni takataka, yaani Mungu huyuhuyu tunayemuabudu aliona mitume wote wanatakiwa kuwa Wazungu na Waarabu.

Dunia ina siri kubwa sana. Kuna siku niliwaambia kuna watu wanamjua Mungu wa kweli ni yupi, inawezekana huyo Mungu unayemuabudu si Mungu wa kweli. Kuna siri ambazo zimefichwa sana. Hizi siri ukitaka kuzichimbua, viongozi wa dini wanakwambia usichimbue, unamkosea Mungu.

Kuna mtu aliniuliza: “Mhaya, kwa nini unamzungumzia Mungu wa watu? Wenu yupo wapi?”

Akiwa na maana kwamba unasoma Biblia unakutana na Mungu wa Israel, unasoma unakutana na Mungu wa Kiarabu. Yaani unaambiwa Waarabu walifanya hivi na vile, inamaana hawa Wazungu na Waarabu walikutana na Mungu wa kweli, sisi tukashindwa kukutana naye na kuanza kumwabudu Mungu wao? Hayo maswali jijibu mwenyewe tu.

Hii dunia imezungukwa na wajanja sana. Hawa wajanja wanaitawala dunia kwenye nyanja mbalimbali, elimu, biashara mpaka dini. Na niliwahi kukwambia kwamba hata siku zetu za kuabudu walizipanga wao. Yaani wao na miungu yao wakakupangia siku za kuabudu.

Ukisoma vitabu vya dini, vinawazungumzia wao tu na miungu yao, haiwazungumzii watu weusi. Ukiuliza nabii fulani na mitume, unaambiwa walikuwa Waarabu ama Wazungu, Waafrika wapo wapi?

Haohao watu wakaweka vitu vyeusi tu ndiyo vinakuwa vibaya. Shetani hachorwi kama Muarabu ama Mzungu, lazima awekewe ngozi nyeusi. Unasikia tu mchawi anavaa kaniki nyeusi akiroga. Mtu akizikwa kwa sababu anakwenda kwa Mungu, tunamingirisha kwenye sanda nyeupe. Yaani mchawi...kaniki nyeusi....sanda nyeupe.

Malaika wote unaowajua wewe, ukichorewa unaonyeshwa ni Wazungu...hakuna malaika mweusi. Vitu vyote vibaya vina rangi nyeusi, na vyote vizuri vina rangi nyeupe. Vitu vya hatari ambavyo si salama, rangi nyeusi, ila vile salama vyote ni rangi nyeupe.

Mavazi ya watu wanaoabudu shetani huwa meusi, hawavai meupe. Yaani hii rangi yetu ilianza kubaguliwa kuanzia kwenye hvyohivyo vitabu.

Leo ukimchora Yesu mweusi ama mitume, watu watakushangaa, ila ukimchora shetani mweusi, hata yule Saidi wa Mbagala atakuona upo sahihi. Yaani tayari hata sisi tayari wajanja washatupatia kwa kutukubalisha kwamba vizuri ni vyeupe, vibaya ni vyeusi.

Ukimchora shetani mweupe tu...ndugu yangu utatafutwa...ila ukimchora mweusi...mbona freshi tu, utaambiwa ndiyo ngozi yake.
Wajanja hatuandikagi kitabu kwa thread isee..
Only 1 paragraph inatosha.
 
Makasiriko gani ? Wakati nyie washamba ndio maana nchi haiwezi kuendelea ...Hao maprofessor wenu ushamba mwingi na akili za kizamani.

Huo husomi wenu mmefanya mapinduzi gani ,ni kwamba nyie washamba na tunawaona mabayo tu hamna jipya .

Ndio maana hamjui kujiongeza na ujinga wenu hata mambo ynayoendelea duniani hamjua mpo kama wewe.
Nimekuuliza wewe na Kabila lako mmefanya nini hapa Nchini, unaleta porojo au unaona aibu kutaja kabila lako la kina Kinjeketile Ngwale
 
Sasa nyie si ndio mnajisifu ni wasomi na ujinga wenu.!!

Wale maprofessor wenu wana nn cha maan !?

Usomi na ushamba havikai sehemu moja ,hizo nyadhifa mlizopewa hamna kitu mmefanya .

Kama wewe ulivyo mshamba hata uchambuzi wako unakuwa unakuwa wa kijinga ,yaani unaonekana mshamba kutwa kushambulia uislamu .
 
Kuunganisha usomi na personal archivement unakua haupo sawa unless unakua umekariri kasumba za kizamani,Mambo ya pesa ni ishu ya opportunities na opportunity zipo kwa ajili ya yeyote awe amesoma sana ama ngumbaro, na pesa inakaa kwa yeyote anaeweza kuitafuta na kuilea bila kujali levo yake ya elimu.
 
Back
Top Bottom