Kinyonga na Maajabu ya Rangi

Mtuache

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
251
638
Habari wana jamvi,

Hivi ulishawahi kujiuliza kinyonga anawezaje kujibadilisha rangi?

Majibu ya Kwa Nini, Kitu gani na Kivipi Kinyonga anaweza kubadilika rangi haya hapa.

Kama wewe ni mpenzi wa kusoma bila kuchoka shuka na mimi hapa taratibu. Kama kawaida yangu huwa ninaandika sayansi zile za ndani-ndani sana lakini kwa lugha rahisi.

Iko hivi...
Kila kiumbe kina ngozi, ngozi ya kiumbe fulani hutofautiana na kiumbe kingine kulingana na Seli za ngozi ya kiumbe husika, Binadamu, kwa mfano, ana Seli zinaitwa Melanocytes kwenye ngozi ambazo husaidia kuunda aina Fulani za Seli ziitwazo Melanin kwa ajili ya kuipa rangi nyeusi au Kahawia ngozi ya Binadamu.

Kinyonga anazo Seli nyingi kwenye ngozi yake!

Seli zote kwenye ngozi ya kinyonga hubadilika kulingana na mwanga utakaomulika kinyonga, na aina fulani ya hormone au kemikali ya kichocheo ambayo kinyonga atakuwa nayo kwa mda huo.
Seli hizi kwa pamoja huitwa "Chromatophores"

Hili neno limeundwa na maneno kama "Chroma" au Chromo yaani Rangi na "Phore" yaani punje au Pigment.
Hizi Phore huitwa hivi kwa sababu ni punje ambazo zina uhusiano na mwanga (photo). Wanaofahamu "Chromatography" wanajua kuwa ni Sayansi ya kutenganisha na kutambua rangi.

Unaweza kusema Kinyonga ni "Chromatographer" wa asili.

Sasa hizi Chromatophores za kwenye ngozi ya kinyonga huwa zipo za aina nyingi, kumbuka Binadamu anazo tu Melanin kutoka kwenye Melanocytes ambazo huwa ni Nyeusi au Kahawia.

Kinyonga anazo "Melanophore" ambazo ni Nyeusi au Kahawia, hizi ni sawa na zile zilizo kwenye ngozi ya Binadamu. Kinyonga anazo pia seli nyingine zinaitwa "Iridophores" hizi hutoa rangi ya blue na kijivu.

Kinyonga huwa na seli nyingine kwenye ngozi zinaitwa "Erythophores" hizi hutoa rangi Nyekundu.
Na pia kuna "Cianthophore" hizi hutoa rangi ya Njano.

Hapo tumemaliza kitu gani kinasababisha abadilike rangi, "Ni kwa sababu ngozi yake ina seli mbalimbali zinazoweza kuunda pigments zenye rangi tofauti kwa nanma anavyotaka"

Kama uko tayari, tunaweza kusonga mbele kujua sasa anawezaje kuziongoza rangi hizi kuchanganyika na kuunda muonekano wake?

Iko hivi...
Kwenye kila kiumbe kuna aina ya kemikali tunaziita vichocheo vya mwili au hormone, hizi hutengenezwa kwenye mwili kwa muongozo wa Ubongo kulingana na mazingira aliyomo kiumbe fulani.

Mfano Binadamu akiwa kwenye baridi mwili hujua kuwa kuna namna unatakiwa kutengeneza ngozi ijilinde na baridi. Ndipo inaweza kutolewa taaria mwili kuunda vipele kwa kuziba Vinyweleo ili joto lisipungue

Au katika mazingira ya kuogopa mwilini automatic unaweza kuunda vipele kwenye ngozi kumaanisha ubongo umechukulia tukio lililopo kuwa la kudhoofisha mwili. Katika mazingira mengine mtu mweupe sana akiwa kwenye hofu ngozi yake huwa nyekundu.

Na kwa kinyonga ipo hivyo, ubongo wa kinyonga unaweza kutoa taarifa kwenye seli za mwili wa kinyonga ambazo taarifa ikipokelewa itaenda kusumbua seli za ngozi, badala ya kuunda vipele au kuamsha vinyweleo, kwa kinyonga huwa ni kuunda aina nyingine ya Rangi.

Kwa nini?
Kwa sababu ya seli za Rangi mfano nyekundu huwa zina uhusiano na kichocheo cha mwili kinachohusu hofu.
Alafu kichocheo cha mwili kinachohusu Furaha na afya njema huwa na mahusiano na seli za kijani.

Hivyo kinyonga akiwa ametulia zake kwenye mazingira hana stress mara nyingi huwa kijani, na akisumbuliwa huanza kugeuka kuwa rangi ya Udongo, kuja Njano mpaka nyekundu kama atapata hofu kabisa.

Hizo ni hormone za mwilini, kama unavyiweza kutishia Binadamu akatoa haja ndogo na kutetemeka,
Kwa kinyonga huwa zile hisia zinasumbua seli za kwenye ngozi yake.

Kama ambavyo mtu anaweza kupata mshutuko akahisi upande mmoja umekufa ganzi na damu ni kama vile hazifiki, Pia na kwa Kinyonga iko hivyo.

Unaweza kumtia hofu lakini vile vichocheo vya hofu vikaenda baadhi ya sehemu za mwili na pengine vikaenda vichocheo vya kujihami, na pengine vikaenda vichocheo vya kuhisi joto limepanda na pengine vikaenda vichocheo vya mwili kupoa ghafla.

Matokeo yake utaona anakuwa na Rangi mchanganyiko. Hapo unakuwa umemvurugia mfumo wa fahamu, mfumo wa upumuaji, Chakula, mzunguko wa damu na hata mfumo wa kufikiri.

Sasa kwa Nini anaweza kubadilika rangi hata kwa maamuzi yake? Hiyo ni kawaida yake.

Ndio maana huwa nasema wanyama wanafanya Photosynthesis. Japo wasomi wa mchongo wataendelea kuikataa hii.

Katika kuchakata mwanga na mionzi ya Jua, Rangi Nyeusi huwa inasharabu (Absorb) mionzi na mwanga pamoja na Joto, wakati rangi Nyeupe huwa anaakisi (reflect).

Kinyonga akihisi joto la mwili wake ni dogo huwa akili inatoa taarifa kwenye vichocheo vya ngozi kuunda Melanin zenye rangi nyeusi au Kahawia zile zinazoitwa Melanophore kwa ajili ya kuvuta au kufyonza Joto na mionzi ya Jua kwa aajili ya kujiongezea joto mwilini.

Na akitataka kupunguza Joto au kujikinga na Mionzi mikali, automatic ubongo utachakata taarifa ya kuunda pigments zenye rangi ya uweupe kwa ajili ya kuakisi mwanga na Mionzi.

Wakati mwingine kinyonga hubadilika rangi kuendana na mazingira kwa ajili ya kujificha, au kuwatisha viumbe wengine, hii inarudi kule kwenye kujihami na hisia za kuwekeana hofu kwenye jamii.

Hubadilika rangi pia kujaribu kubadili "Chemical Bonding structure" ya seli kwenye ngozi yake kwa ajili ya kujitibu magonjwa mbalimbali au vidogo. Hili nililisema kwenye makala ya Photosynthesis kuwa hata Mionzi ya Jua inasaidia kutibu magojwa kwa Binadamu.

Pia Kinyonga kuna mazingira huitaji oxygen kidogo kwenye mwili wake, hivyo hujigeuza kuwa rangi ya kijani ili afanye Photosynthesis ua kutumia Carbondioxide kama ilivyo mimea. Mara nyingi akifanya hivi huweka mchirizi mweupe kwenye ngozi kwa ajili ya kupunguza idadi ya Mionzi kwenye mwili.

Imeandikwa na Cekam Cekam's.

1684230307730.jpg
 
View attachment 2623865
IMG_20220509_104149.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom