Je, unajua kwamba Adam na Hawa walikuwa watu weusi?

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
805
807
Habari Jf nataka kuwajua kama madailivyo kuhusu adamu na hawa ahsant twende na mimi pamoja

ADAM NA HAWA WALIKUWA WEUSI AU WEUPE?

Kujibu swali hili na kwa kutaka kujua au kuthibitisha uvumi kwamba Adam alikuwa mtu mweusi, inabidi turudi kwenye tafiti nyingi zilizofanyika kuhusu DNA ya mtu mweusi.

DNA ni kifupisho cha "DeoxyriboNucleic Acid" ambayo ni jina la Kiingereza la molekuli kubwa ndani ya seli za viumbehai wote. Kwa Kiswahili huitwa "Asidi DeoksiriboNukleini" (kifupi: ADN) au 'Asidi Kiinideoksiribo. DNA hubeba vinasaba (jeni), yaani ni hii molekuli ambayo inatawala seli za viumbehai na kuamua tabia, mwonekano, jinsia, na hata aina ya damu ya viumbe vyote.Yaani kwa mfano ukitaka kuthibitisha kama mwanao ni damu yako kweli,unakwenda kupima vinasaba au jeni ya DNA.

Utafiti wa kina sana wa kisayansi unaonyesha kuwa mwanamke mweusi (Mwafrika) ndiye binadam wa pekee ambaye ana DNA ya kipekee inayoweza kutoa kila rangi ya binadamu duniani!Yaani anaweza akazaa mwafrika, albino, mzungu, mwarabu n.k.Jeni yake ni ya kipekee!

DNA ya mwanamke wa kiafrika inapopitia mabadiliko ya kimaumbile(mutation),binadamu wa rangi zote wanapatikana.Aina hii ya "gene"(jeni) ya vinasaba inaitwa "Eve Gene",yani jeni ya Eva,na haipatikani popote pale zaidi ya hapa kwetu Afrika.

Alafu kwa wale wasiojua, GENE (jeni)ni ruwaza ya kemikali ndani ya seli ambayo hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbehai kutoka kwa wazazi wake.

Sasa naomba mtu akane hili alafu anithibitishie kuwa Adamu na Hawa hawakuwa watu weusi na hawakuwepo hapo bondeni Mesopotomia (Edeni)

Tambueni ukweli kwamba wazungu walitunyang'anya imani yetu,na chimbuko lake, na kuifanya kuwa ya kwao!

Adamu na Hawa walikuwa watu weusi.

#IloveAfrica
#AfricaIsPowerful
#FaithBeganInAfrica
#AlkebulanIsPower
 
SIO HAO TU HATA MKE WA NABII MUSA ALIKUWA MTU MWEUSI (SIPORA) MAMA YAKE GERSHOMU MTOTO WA KWANZA WA MUSA

MTU NI MTU AWE MWEUSI AU MWEUPE NI MTU TU

DIFFERENT COLOUR ONE PEOPLE

USIPAGAWE MUNGU HANA UBAGUZI STAY COOL, STAY SAFE
 
SIO HAO TU HATA MKE WA NABII MUSA ALIKUWA MTU MWEUSI (SIPORA) MAMA YAKE GERSHOMU MTOTO WA KWANZA WA MUSA

MTU NI MTU AWE MWEUSI AU MWEUPE NI MTU TU

DIFFERENT COLOUR ONE PEOPLE

USIPAGAWE MUNGU HANA UBAGUZI STAY COOL, STAY SAFE
Hii kitu ipo kwako lakini siyo kwa mzungu.
Mzungu kwake color matters most. Atakupa heshima kulingana na rangi, ubaguzi kwao upo siku zote wanaficha ficha tuu ila hawamkubali mtu mweusi kamwe, sijui kunanini wana kiogopa toka kwa mtu mweusi.
 
Hio dini inayomtambua Adam na Hawa imetokea wapi ? (Bali kule ilikotokea watasema walikuwa ni mataifa gani)

Another way tafuta kwenye hio Dini yako inaposema mataifa yalitokea vipi na yalitokea wapi (utaona kwamba watunzi walikuwa wanavutia kwao)

Ukija historically species yetu mabaki yake yapo Olduvai Gorge - Tanzania hivyo asili yao ni hapa Tanzania..., Ila ukitumia facts kwamba sisi ni muunganiko wa cells zilizokuja kuwa multicellular by happenstances basi chanzo ni cell tu kama wewe ulivyoanzia kwenye sperms mbili
 
Ehe.

"Eve's Gene" ni neno la kisayansi? au Ndio hivyo tena, mambo ya Wazungu na kutupotosha?
 
Back
Top Bottom