Photosynthesis: Ulemavu

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Tulioanza pamoja sehemu ya kwanza tuliona maana ya Photosynthesis bila kuikariri kama kitendo kinachofanyika na mimiea tu, bali hata viumbe wengine na hasa wanyama kama Binadamu. Katika maoni ya wadau wengi tuligundua watu kutotaka kuhama kwenye dhana ya neno Photosynthesis kama wengi walivyojifunza kwenye mitaala ya elimu za shuleni, wakijaribu kusema nitumie neno lingine kwa ajili ya wanyama. Sio kweli, mimi nitaendelea kusema wanyama wanafanya Photosynthesis ikiwemo Binadamu.

Ambao hawajataka kuelewa au kubadilika namna ya walivyosoma hapo awali, wataelewa huko mbeleni sisi walio tayari kupata "jambo jipya" kupitia kujifunza tuendelee...

Katika sehemu ya kwanza niliainisha namna Binadamu anaweza kufanya Photosynthesis; sio kuunda chakula chake, bali kuunda baadhi ya seli za mwili wake kwa kutumia mwanga na Mionzi ya Jua. Niliongelea sana sana kwenye ngozi ya Binadamu ambayo huwa na seli za Melanocyte ambazo zikichomwa na mionzi ya Jua huunda moja ya matokeo ambayo ni Kemikali inayoitwa Melanin. Hii Melanin ndio huipa ngozi rangi nyeusi au maji ya Kunde.

Mtu mweusi anayo Melanin ya kutosha sana, na pia Melanocyte inapokuwa na uwezo wa kuunda Melanin za Kahawia (Brown) mtu huwa na Rangi ya Maji ya kunde, mara nyingi kama Melanin zipo za kutosha mtu huyu huwa na Nywele Nyeusi ngumu na macho Meusi.

Kwenye jicho kuna kile ki-duara katikati ambacho kina ki-tundu katikati yake, kile ki-duara huwa kinatanuka na kusinyaa kuweza kupunguza au kuongeza ki-tundu kilicho katikati yake, hii husaidia jicho kutofautisha mwanga mkali (mwingi) na mwanga hafifu (machache) Kile ki-duara katikati ya jicho kinaitwa Iris.

Kwa mtu wa kawaida– mwenye Melanin kwa kiwango sahihi– kile ki-duara kinabidi kiwe Cheusi au rangi ya Ugoro. Kwa watu weusi kinakuwa cheusi, na baadhi ya watu wa maji ya kunde kinakuwa Brown; Rangi ya ugoro au udongo mkavu.

Photosynthesis sio tu kwenye ngozi, bali hata kwenye macho kuweza kuona na kuunda picha (Image au vision) tunatumia mwanga wa Jua, kuweza kutofautisha Rangi za vitu tunafanya "Photo-Spectroscopy", kuweza kuwa na Iris inayotanuka na kusinyaa kuruhusu mwanga mwingi au kidogo upenye kwenye lenzi, Picha mtu anayoona kwenye jicho inapokelewa kwenye Retina kwa kuchakata mwanga (Photo-synthesize) kuweza kuunda mawimbi ya umeme kupita kwenye Neva ya Optic mpaka kwenye ubongo, kote huko kuna Melanin na Melanocyte.

Unaweza kuona kwa nini nasema wanyama kama Binadamu wanafanya Photosynthesis.
Kwa swala hili la "Spectrum Analysis" na Kuweza kuona kutumia macho nitakuja kuliongelea huko mbeleni.

Niliwaambia kwenye sehemu ya kwanza kuwa "Weusi au maji ya Kunde ndio rangi sahihi za ngozi ya Binadamu anayeishi na mwenye asili ya Dunia hii, hizo nyingine ni ama Ulemavu, Sumu, Mazingira Magonjwa, Hybrid au Mutation" Leo tuongelee kwa ufupi Ulemavu ikiwa ni kisababishi cha kwanza cha watu kukosa Melanin mwilini mwao.

Ulemavu wa ngozi husababisha watu kushindwa kuunda Melanin ambazo hutoa rangi nyeusi ya ngozi. "Albino" ni jina wanalopewa watu wenye aina fulani ya Ulemavu wa ngozi ambao unafanya wanashindwa kutengeneza metabolic activity ya kuunda Melanin kwa kutumia Photosynthesis. Ngozi zao hukosa Kemikali sahihi ambayo ikiunguzwa na Mwanga na mionzi ya Jua huweza kuunda au kugeuka kuwa Melanin nyeusi au Brown.

Moja ya Maoni kwenye sehemu ya kwanza yalikuwa ni kuuliza kama ninasema Photosynthesis Binadamu wanafanya kwa sababu ya Melanin, Je Albino ambao hawana Melanin nitasemaje.!?

Kwanza inabidi kueleweka vizuri. Binadamu hafanyi Photosynthesis kwa kutumia Melanin, bali kwenye kufanyika kitendo hicho ndipo anaunda Melanin, Ni Melanocyte ambazo hutumika kwenye mchakato mzima kuunda Melanin, na hata hivyo uundwaji wa Melanin huendelea hata kwenye mazingira ambayo hayana mwanga wa Jua, japo kwenye mionzi na Mwanga wa Jua ndipo hufanyika zaidi na faida hizo tumeziona sehemu ya kwanza.

Melanocyte kuunda Melanin hufanyika hasa kwa kutumia mionzi ya Ultraviolet (UV Radiation) Mionzi hii huwa sehemu yeyote kwenye mazingira ila hupungua nguvu kulingana na chanzo chake, mionzi mingi ya namna hii huingia kwenye mazingira kutoka kwenye Jua ndio maana Mionzi ya Jua (Sun Intensity) husaidia sana hata kama mwanga wa Jua (Sun Light) haupo.

Hivyo kwa Albino– Watu wenye Ualibino– kinachokosekana sio kisababishi cha Photosynthesis bali matokeo yake, na hii inatokana na Ulemavu uliopo kwenye Seli zao za ngozi zinazoitwa Melanocyte zinazotakiwa kuunda Melanin. Kwa Albino Melanin zinaweza kuwepo kidogo au zisiwepo kabisa, kwa sababu ya kuwa na Aina fulani za Melanocyte ambazo hizo ndo huo Ulemavu.

Albino pia wanafanya Photosynthesis lakini matokeo yake sio Melanin ni kitu kingine kabisa. Ndio maana niliwaambia kwenye "Mjadala na Wasomi" kuwa Photosynthesis inaweza kuwa na matokeo (by-product) mengi kulingana na Reactants zinazohusika kwenye mchakato.

Mfano kwenye Mmea utajitengenezea chakula (Carbohydrates) kwa kuchoma Chlorophyll, Binadamu atatengeneza Melanin kwa kuchoma Melanocyte, Sasa kuna huyu mlemavu ambaye hawezi kutengeneza Melanin kwa sababu mwanga hautaenda kuchoma Melanocyte ambazo zina Ukamilifu. Japo Viumbe hawa wote wamefanya Photosynthesis.

Iko hivi...
Melanocyte ni Seli zinazokuwa kwenye mwili wa Binadamu, Seli hizi hupatikana sanasana kwenye Ngozi, Macho na Nywele, husaidia kuipa ngozi na Nywele rangi, kuyapa macho rangi na uwezo wa kuona, nimesema kuhusu macho tutaongelea huko mbele...

Hizi Melanocyte zinatengenezwa kwa kufuata asili ya Vinasaba (Genetic Material) vya Binadamu husika.
Gene zinakuwa na kazi ya kuunda aina fulani za Kemikali maalumu ambazo huwa na kazi mbalimbali za kuunda Kemikali mwilini kama mbegu za kiume, machozi, Damu, Mayai ya kike, Mate, Hormone nk.

Zile Gene (Vinasaba) ndivyo pia huunda Seli kama Melanocyte ambazo hutumika kwenye kuunda Melanin.
Sasa unakuta kulingana na Vinasaba vya Binadamu fulani kuna baadhi ya Seli zimekosewa kwenye uumbaji wake; Ulemavu.!

Mfano; Kuna aina kama 8 za seli za Vinasaba zinashirikiana kuunda Melanocyte, ukiweza kukuta hata seli moja ina Ulemavu itasababisha hata kuwepo na Ulemavu kwenye Melanocyte. Wingi wa seli zenye Ulemavu kwenye Vinasaba itasababisha ukubwa wa Ulemavu kwenye Melanocyte. Hii inasababisha kuwepo na ma-Albino wa aina mbalimbali kulinga na kila mtu ana Ulemavu kwenye seli ipi ya Vinasaba.

Zinavyoundwa seli kwenye mwili kimakosa ndivyo na matokeo yatakuwa tofauti pale zitakavyochomwa na mionzi kadhaa ikiwemo mionzi ya Ultraviolet kutoka kwenye Jua. Hivyo Albino nao hufanya Photosynthesis lakini Seli zinazotumika ni zile Melanocyte zenye Ulemavu hivyo matokeo ya mchakato huo sio tena Melanin bali kitu kingine kabisa ambacho kulingana na Ulemavu uliopo kwa mtu mwenyewe inaweza kusababisha tatizo kubwa la kiafya.

Walemavu hawa wa ngozi walio wengi ngozi zao hazina Melanin kabisa, jambo ambalo linasababishwa na Melanocyte zao kuunda Sumu zinapochomwa na Mionzi ya Jua, wengi hawapendi kuingia kwenye mwanga wa Jua moja kwa moja kwa sababu Photosynthesis yao huunda madhara makubwa kwenye mwili wao.

Kwa albino wengi uwezo wao wa kuona huwa mdogo kutokana na Melanocyte za kwenye macho kushindwa kuunda Melanin sahihi au kushindwa kuchakata mwanga (Photo-synthesize) kuunda picha nzuri, hushindwa kuona maandishi madogo, kushindwa kuona mbali au karibu, au hata macho yao kushindwa kuchakata mwanga mkali tatizo hilo huitwa "Photophobia"

Nitakuja kukueleza matatizo wanayokumbana nayo Albino wakifanya Photo-Synthesis kwa kutumia Melanocyte ambazo zina Ulemavu, badala ya kuunda Melanin huunda kitu kingine, ikiwa ni pamoja na kufa au kuungua kwa seli hizo na kuunda "Melanoma" aina fulani za Seli ambazo husababisha Kansa ya Ngozi.

Itaendelea View attachment 2611390

FB_IMG_1683311600589.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom