Neno la shukrani kwa Kamati kuu na NEC ya CCM kwa uteuzi bora wa wagombea

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Kwa mara nyingine tena siwezi kuficha hisia zangu za furaha kwa kazi nzuri iliyofanywa na kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM taifa kwa uteuzi bora wa wagombea.

Nami pia nilikuwa ni moja ya watia nia kwa nafasi ya uenyekiti wa UVCCM Taifa lakini sijafanikiwa kupita lakini hilo haliachi kukipongeza chama changu.

Ninatambua kwamba wengi walikuwa na matarajio tofauti na ndio maana uteuzi huu unaangaliwa kwa jicho la lawama. Kuna wanaosema ni wazanzibar tu na wengine wanasema ni waislamu tu.

Wanaangaliwa kama waislamu kwa sababu kuna kundi liliamini watakuwa wakristo tu na wanaosema wazanzibar tu waliamini angekuwa mtanganyika.

Katiba ya CCM na kanuni za UVCCM zimeelezea usawa wa kijinsia ambalo limeangaliwa kwa umakini na pia zimeelezea kama mwenyekiti mmoja atatoka upande mmoja wa muunguno basi m/kiti atoke upande mwingine na hiko kimefanyika a na wala hazijasema lazima awe mkristo au mwislamu.

Ukiona jambo hili la dini linazungumzwa kwa uchungu tambua kwamba maslahi ya watu yameguswa na dini inatumika kama kichaka tu. Namshukuru Mungu sikuwa na maslahi binafsi na ndio maana napongeza uteuzi wa wagombea.

Kipekee kabisa nimpongeze mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kazi nzuri na uongozi bora maana sio rahisi kumridhisha kila mtu.

Nikishukuru chama changu kwa kunipa nafasi ya kugombea na kunijadili, ni matumaini yangu sifa na uwezo wangu utatumika kutumikia nafasi nyingine ndani ya chama na serikali.

Kidumu Chama cha Mapinduzi
 
Back
Top Bottom