Neno la leo: Ukiona wanatamani ushuke kimaisha au uanguke jitafakari

Plan Paris

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,881
2,000
Ukiona mtu au watu wanatamani ushindwe, uanguke, uumie, ufeli au kupoteza uhai kabisa wewe binafsi mkeo au watoto wako usikimbilie kusema binadamu ni wabaya, binadamu wanachuki, binadamu wanakinyongo, binadamu wana wivu n.k huo ni muda wako kujitafakari.

Kila binadamu ana wivu, kila binadamu ana kisasi, kila binadamu anachuki n.k endapo utakuwa umemkosea, umemdhalilisha, umemnyanyasa, umemkejeli, umemtendea ubaya n.k

Ukitaka kuamini tizama mifano ifuatayo.

Mfano kumshitaki mtu polisi ni aina mojawapo ya kisasi (indirect revenge), kuombea kiongozi flani anayekejeli watu afukuzwe kazi na akifukuzwa unafanya sherehe kabisa ni aina moja wapo ya kutamani mtu aanguke, kuombea kampuni flani iliyokunyanyasa au kukufukuza kwa kukudhalilisha kuiombea ishindwe au kufa kabisa ni aina moja wapo ya kisasi, kufumaniwa na mke wa mtu kupigwa au kujeruhiwa ni aina moja wapo ya kisasi , watu kuombea ufukuzwe kazi kwa kihere here chako cha kuiomba serikali iweke kodi kwenye huduma flani n.k n.k n.k.

Binadamu ndivyo tulivyoumbiwa, kila mtu ana wivu, anakisasi, anakinyongo anatamani ushuke au uanguke kabisa, ukiona mtu au watu wanakuombea mabaya au wanatamani jambo lolote kati ya hayo likupate, usikimbilie kulaumu au kulalamika bali ni muda wako wa kujitafakari na kuangalia ni wapi ulipokosea.

Nawasilisha.
 
Plan Paris

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,881
2,000
quote-i-don-t-want-people-to-see-me-fall-i-mean-i-got-enough-people-cheering-for-me-to-fall-st...jpg
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,527
2,000
Tuna visasi na chuki, ila kuomba mtu aanguke ili usuuzike ni uchawi usio rasmi.

Kuna wimbo unasema ombea adui yako aishi siku nyingi ili utakapobarikiwa ashuhudie.

Usiombe ashuke jiombee kunyanyuka huku yeue ukimwombea kuishi zaidi.
 
Hivi kwani umesahau Makonda alivyoshindwa ubunge watu walikula sherehe,
Umesahau ole sabaya alivyotiwa nguvuni watu walifurahi sana, je huo ni uchawi?

Point yangu ni kwamba mtendewa asikimbilie kusema uchawi bali ni muda wa kujitafakari
 
St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,588
2,000
Mimi adui zangu wakifa naona nitafilisika kabisa manake bila ya wao nisingefika hapa nilipo. Sasa na zile kapicha WhatsApp status ataangalia nani?
Mwenyezi Mungu waongezee maisha ya kuishi all my haters

Lunatic
 
Maadui zako au ni EX zako? Maana ni ngumu kumaa na namba ya adui unless kuna ka undugu au kinyongo kilichojificha
 
St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,588
2,000
Maadui zako au ni EX zako? Maana ni ngumu kumaa na namba ya adui unless kuna ka undugu au kinyongo kilichojificha

Mkuu kikulacho kinguoni mwako ndugu yako anaweza kuwa adui sijui ka hujui jui hapo itakapo kuzibia bania dunia. Ndipo atakapo kususia dizaini ile namna ile.

Mr 2 ft Weusi Asilia - Yamenikuta

Lunatic
 
kijana13

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
1,379
2,000
Yaan SIO KILA ANAYEKUCHUKIA UMEMKOSEA ,Kuna watu wanaweza kukuchukia au kupenda ukwame kwenye shughuli zako bila sababu yeyote..wapo wengi Sana hao.unaweza tafuta sababu umemkosea wapi na usipate ...Kuna watu wengi Sana wanachukua watu bila sababu yeyote

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,450
2,000
Hapana, sababu lazima iwepo
😲😲
Mkuu hivi mtu baki akiwa amejawa WIVU MBAYA dhidi yako na akakufanyia ubaya...sababu hiyo usemayo haiwezi ikawa ni KULE KUFANIKIWA MAISHA YAKO TU ?!!!

Ogopa sana "DESPERATE MINDS"....

Mathalani mjini kila mtu huwa "busy" na maisha yake....

Nimeshawahi kuingia katika vita na wahuni nilipomuokoa jirani yangu msichana mrembo wa miaka 25 anayefanya kazi benki.....

Ulikuwa usiku wa saa 9 ameshushwa na teksi nje ya aishipo na kuanza kupiga kelele....

Bahati nzuri nilikuwa uani kwangu nakandamiza "tumbaku" nikibarizi kwa kuangalia nyota angani"...

Nilitoka na "mmeme" wa haja nikichukua tahadhari zote za mapambano....niliwakuta wakiwa naye katika pagale mita 200 kutoka kwangu...nilipopiga filimbi walitawanyika ila nilifanikiwa kumkamata mmoja wao ambaye baada ya kumpa kisago cha mwanaukome alinieleza "MOTIVE" nzima juu ya KUMFANYIA VIBAYA HUYO DADA....hakika ulikuwa ni ujinga ,upumbavu,roho mbaya na wivu wa WANAWAKE WENZAKE WALIO DESPERATE mtaani dhidi ya huyo mrembo....so dunia ni pana sana mzeya....si lazima iwe na majibu ya 2+2=4

N.B Tofautisha WIVU na HUSUDA...binadamu wote tuna wivu...ila husuda ni maradhi mabaya ya nyoyo...Husuda ni ile hali ya kuchukia na kutaka mwenzako neema imuondoke pale anapokuwa amepata/amefanikiwa/ana uzuri wa sura ama mwili.

#YetzerHaTov
#ShavuaTov
#SiempreJMT
 
Wengi tu....

Walio na "Desperate minds"....
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,527
2,000
Hivi kwani umesahau Makonda alivyoshindwa ubunge watu walikula sherehe,
Umesahau ole sabaya alivyotiwa nguvuni watu walifurahi sana, je huo ni uchawi?

Point yangu ni kwamba mtendewa asikimbilie kusema uchawi bali ni muda wa kujitafakari
makonda yuko masaki ana maisha bora sana.

hata sabaya sio wa kumwanini kwa haya yanayotokea.

unajua kwanini Mungu alitwagiza kuwa watu wa kusamehe na kusahau??sababu mipange yake sio sawa na yetu,asante.
 
Plan Paris

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,881
2,000
makonda yuko masaki ana maisha bora sana.

hata sabaya sio wa kumwanini kwa haya yanayotokea.

unajua kwanini Mungu alitwagiza kuwa watu wa kusamehe na kusahau??sababu mipange yake sio sawa na yetu,asante.
Kwa sababu kukaa na hasira au chuki ni hatari kwa afya yako
 
Ed Kawiche

JF-Expert Member
May 28, 2020
1,552
2,000
😲😲
Mkuu hivi mtu baki akiwa amejawa WIVU MBAYA dhidi yako na akakufanyia ubaya...sababu hiyo usemayo haiwezi ikawa ni KULE KUFANIKIWA MAISHA YAKO TU ?!!!

Ogopa sana "DESPERATE MINDS"....

Mathalani mjini kila mtu huwa "busy" na maisha yake....

Nimeshawahi kuingia katika vita na wahuni nilipomuokoa jirani yangu msichana mrembo wa miaka 25 anayefanya kazi benki.....

Ulikuwa usiku wa saa 9 ameshushwa na teksi nje ya aishipo na kuanza kupiga kelele....

Bahati nzuri nilikuwa uani kwangu nakandamiza "tumbaku" nikibarizi kwa kuangalia nyota angani"...

Nilitoka na "mmeme" wa haja nikichukua tahadhari zote za mapambano....niliwakuta wakiwa naye katika pagale mita 200 kutoka kwangu...nilipopiga filimbi walitawanyika ila nilifanikiwa kumkamata mmoja wao ambaye baada ya kumpa kisago cha mwanaukome alinieleza "MOTIVE" nzima juu ya KUMFANYIA VIBAYA HUYO DADA....hakika ulikuwa ni ujinga ,upumbavu,roho mbaya na wivu wa WANAWAKE WENZAKE WALIO DESPERATE mtaani dhidi ya huyo mrembo....so dunia ni pana sana mzeya....si lazima iwe na majibu ya 2+2=4

N.B Tofautisha WIVU na HUSUDA...binadamu wote tuna wivu...ila husuda ni maradhi mabaya ya nyoyo...Husuda ni ile hali ya kuchukia na kutaka mwenzako neema imuondoke pale anapokuwa amepata/amefanikiwa/ana uzuri wa sura ama mwili.

#YetzerHaTov
#ShavuaTov
#SiempreJMT
upo sahihi kabisa mtaalam.
ila hizo hashtag # daah!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom