OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 3,624
- 9,170
Ukiona mtu au watu wanatamani ushindwe, uanguke, uumie, ufeli au kupoteza uhai kabisa wewe binafsi mkeo au watoto wako usikimbilie kusema binadamu ni wabaya, binadamu wanachuki, binadamu wanakinyongo, binadamu wana wivu n.k huo ni muda wako kujitafakari.
Kila binadamu ana wivu, kila binadamu ana kisasi, kila binadamu anachuki n.k endapo utakuwa umemkosea, umemdhalilisha, umemnyanyasa, umemkejeli, umemtendea ubaya n.k
Ukitaka kuamini tizama mifano ifuatayo.
Mfano kumshitaki mtu polisi ni aina mojawapo ya kisasi (indirect revenge), kuombea kiongozi flani anayekejeli watu afukuzwe kazi na akifukuzwa unafanya sherehe kabisa ni aina moja wapo ya kutamani mtu aanguke, kuombea kampuni flani iliyokunyanyasa au kukufukuza kwa kukudhalilisha kuiombea ishindwe au kufa kabisa ni aina moja wapo ya kisasi, kufumaniwa na mke wa mtu kupigwa au kujeruhiwa ni aina moja wapo ya kisasi , watu kuombea ufukuzwe kazi kwa kihere here chako cha kuiomba serikali iweke kodi kwenye huduma flani n.k n.k n.k.
Binadamu ndivyo tulivyoumbiwa, kila mtu ana wivu, anakisasi, anakinyongo anatamani ushuke au uanguke kabisa, ukiona mtu au watu wanakuombea mabaya au wanatamani jambo lolote kati ya hayo likupate, usikimbilie kulaumu au kulalamika bali ni muda wako wa kujitafakari na kuangalia ni wapi ulipokosea.
Nawasilisha.