Neno La Leo: Adam Malima Na ' Trigger Happy Police'

Neno La Leo: Adam Malima Na ' Trigger Happy Police'

Mimi naona police alionyesha udhaifu mkubwa kwa kuanza kulia lia/kusema maneno mengiii hata kushindwa kuzuia hasira.
Suala moja, hajatii kamata peleka kituoni. Mengine ni uoga na kutojiamini na kujipendekeza kwa askari pindi wanapokutana na viongozi/viongozi wastaafu.
 
Kwenda kulipia faini ya kuegesha gari mahali sio sahihi ni gharama ndogo sana kuliko gharama ya kwenda kumlipa wakili Kibatala na usumbufu wa kesi nenda rudi mara dhamana n.k. Busara na ukomavu vilitakiwa vianzie kwa mtu mkubwa aliewahi shika wadhifa ktk baraza la mawaziri la JMT. Wala kusingetokea kufyatuliana risasi au kubishana na vijana wadogo sawa na wadogo zake au watoto wake. Zile risasi ni matokeo ya ukaidi wake. Tangu mwanzo angeweza kuepuka kadhia ile. Pale ni escalation of the situation from bad to worst. Tudai zaidi busara za Malima kuliko za askari. maggid unasema askari angeweza kuondoka akamuita Malima kituoni baade wakati pale yeye alikuwa anawafuata askari kubishana nao hata baada ya kuonekana wale askari wanaondoka toka ktk eneo la tukio bila kumkamata na kabla hata askari hajahamaki na kufyatua risasi.
Mmeona na kusikia maelezo ya kamishna Sirro? Afande Sirro anasema kama wale askari wangeondoka pale eneo la kituo bila kuwakamata watuhumiwa, jeshi la polisi lingewashitaki kwa kosa la 'uoga' na kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za jeshi hilo. Kwa kifupi, afande anasema ni kosa kwa askari polisi kuonesha 'uoga', na kitendo cha kufyatua zile risasi pale ndio ujasiri wenyewe uliofanikisha kukamata mtuhumiwa. Mnaojua sheria zaidi mtatusaidia.
 
Maggid Mjengwa wewe ni hovyo sana. Sheria haitambui kiongozi na asiye kiongozi. Ndiyo maana kwa Kiswahili tunasema sheria ni msumeno. Kwenye sheria wote ni sawa; sasa unaanzaje kutuambia Malima sijui ni alikuwa Kiongozi ... sijui angeitwa polisi angeenda tu bila shuruti .... aisee! Kweli mimi Magufuli sikubaliani naye kwenye mambo mengi ila nitamshukuru sana Rais kama atakwamisha juhudi zako zote za kutaka dhamana ya kutuongoza. Hakika wewe hovyo sana. Utawala wa sheria ni kitu cha muhimu sana; na kwenye utawala wa sheria kinachoangaliwa ni nani ametii au kuvunja sheria - kwa kuzingatia "evidence". Siyo career background yako mjomba.
Acha uwongo kwa Tanzania sheria inabagua kati ya mwenyecheo na asie na cheo.
Ingekua haibagui Leo Bashite asingekua anatamba hata baada ya kuvamia cloud TV kwa mtutu wa bunduki
 
Polisi wa kwetu wanafundishwa kwa amri na wao wanakuwa kama walivyofundishwa, kiamri amri tu.

Polisi wafundishwe upole zaidi ya ukali.
 
MAJJID MJENGWA Natamani niendelee kukuheshimu kama nlivyokuwa nakuheshimu enzi za MOTOMOTO, & RAI

ulikuwa unaandika Habari za kichunguzi Kweli na zisizoegemea upande fulani..... Wewe ni kati ya watu ambao nimejifunza NEUTRALITY

Rues uwe MJENGWA yule
 
Mimi sitaki kuangalia nani ana makosa au nani mkamilifu....kwa Maana sikuwa eneo la tukio na sitaki kum judge mtu kwa nisicho kiona

Nitajudge Yale tu niliyoyaona na kwa kutumia ufahamu wangu wa kawaida nagundua polisi hakuna na sababu ya kufyatua risasi hewani. Kwa Maana pale hakukuwa na tishio lolote lililomlazimu yeye kufanya vile

Samahani mapolisi,lakini nadhani wengi wao walioingia ni form four failure,ambao akili zao kung'amua mambo inakuwa shida sana. Hebu tumieni akili za kuzaliwa polisi wetu kama akili za kusomea na kuelekezwa zinawashinda.

Hatutaki drama zenu za marisasi risasi tushawachoka. Sisi waTz si watu wa dzain za Iraq buana
 
Ukweli Malima aliwa provoke hao polisi bila sababu ya maana. Polisi walikuwa kazini. Wakakuta gari hilo la Malima lina kosa dogo la ki traffic ambalo kisheria adhabu yake ni faini ya shs 30,000 tu. Sheria waliitunga wenyewe wa akina Malima enzi hizo. Sisi wananchi wa kawaida tumekuwa tukikamatwa sana na kulipa hizo faini. Inashangaza sana Malima baada ya kukutwa gari lake lina makosa hayo akawa mbabe kwa polisi.

Badala ya kukubali kosa na kuomba samahani au kukubali kulipa hiyo faini huko yard/ kituoni kama ambavyo sisi huwa tunafanya, yeye kawaijia juu hao polisi. Kwamba eti hawamjui yeye ni nani? Yaani kumbe hiyo sheria haiwahusu watu kama yeye; inatuhusu sisi tu makabwela. Hii ni dharau si kwa polisi wale tu bali ni dharau kwetu pia sisi wananchi tusio na vyeo kama vya akina Malima. Acha dharau hiyo imu cost. Badala ya kulipa faini ya sh 30,000, amelala lockup, amelipa mamilioni kwa akina Kibatala, usumbufu wa kesi na anaweza hukumiwa kifungo jela au faini kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi yao (obstruction of justice). Polisi kufyatua risasi hewani ilitokana na hiyo provocation ya Malima. Polisi naye alitaka kumwonyesha Malima kuwa naye (polisi) ni nani.
 
Nashangaa kwann yule polisi zile risasi alipiga alitakiwa apige kwenye miguu ya malima,anadhani kuwa bado kiongozi jamaa anadharau sana tangu akiwa waziri aliwahi kwenda uwanja wa taifa akiwa na watu watano hawa tiket lakini akalazimisha waingie kisa yeye waziri kwavile alikuwa waziri askari wakanyamaza akaingia na watu wake kwa dharau kubwa sana nadhani alifikiri bado ni waziri,mjinga sana.
wewe umesema vyema,
pale malima angeshinda ,polisi ingezaraulika sana,yaani kila ukiona ile gwanda unakumbuka yuleyule,
Yule polisi alitetea jeshi lote lisidharaulike.
Kumbuka kila raia anapaswa kutii sheria bila shuruti.
Pale ilibidi amvunje mguu mmoja tu kama angeendelea kubisha,ili ajue kuheshimu jeshi,
Polisi huyo anastahili aongezwe cheo.
Hiyo bunduki ndio kazi yake
 
Unazungumza vipi na mtu asiyetaka kufuata sheria wala kutii amri. Nini kingetokea kama angetoa gari alipokua amepaki. Ni kweli polisi alienda mbali ila naona kama tunampa lawama bure bila kuangalia chanzo chake. Malima alitaka kutumia diplomatic immunity vibaya na kuonyesha jeuri mbele ya watu kasahau hata si kiongozi tena.

Malima angetoa gari pale bila shurti yasingetokea yote haya.
Ukiwa kiongozi unaruhusiwa kuwa JEURI?Mjue mnawapa sifa viongoz kwa kauli zenu
 
Nashangaa kwann yule polisi zile risasi alipiga alitakiwa apige kwenye miguu ya malima,anadhani kuwa bado kiongozi jamaa anadharau sana tangu akiwa waziri aliwahi kwenda uwanja wa taifa akiwa na watu watano hawa tiket lakini akalazimisha waingie kisa yeye waziri kwavile alikuwa waziri askari wakanyamaza akaingia na watu wake kwa dharau kubwa sana nadhani alifikiri bado ni waziri,mjinga sana.
AHAHAH UMENICHEKESHAA SANA MKUU
 
Daaah, nimesikitishwa kweli na mleta mada, kwasababu ukiona vizuri ule mzozo ulivyokuwa ni dhahiri mheshimiwa Malima ndiye aliyekataa kutii sheria na dereva wake, alfu kitendo cha raia kuanza kuzomea askari wakiwa kazini ile ilkuwa na fedheha kwao. Sasa sijajua kama ulitaka wamuache kwa kulidharau jeshi la polisi au ile kadmnasi aliyokuwa anaikusanya pale ilikuwa hali? dereva wake kafuatwa anaambiwa umekosea anaondosha gari ili kufuta ushahidi, jamani tuwe makini tunapokuwa tunatetea vitu vingine.
 
watz hawana jema,mleta mada hukuona bwana mdogo anaitwa muhuni vyeti fake na ile kadamnasi???
Kwahiyo na wewe ukiitwa mhuni na vyeti fake ndo unarusha ngumi?
Yule "Mpuuzi' alomwonyesha nape Mguu wa Kuku ndo dizain ya hao askari
 
Kwenda kulipia faini ya kuegesha gari mahali sio sahihi ni gharama ndogo sana kuliko gharama ya kwenda kumlipa wakili Kibatala na usumbufu wa kesi nenda rudi mara dhamana n.k. Busara na ukomavu vilitakiwa vianzie kwa mtu mkubwa aliewahi shika wadhifa ktk baraza la mawaziri la JMT. Wala kusingetokea kufyatuliana risasi au kubishana na vijana wadogo sawa na wadogo zake au watoto wake. Zile risasi ni matokeo ya ukaidi wake. Tangu mwanzo angeweza kuepuka kadhia ile. Pale ni escalation of the situation from bad to worst. Tudai zaidi busara za Malima kuliko za askari. maggid unasema askari angeweza kuondoka akamuita Malima kituoni baade wakati pale yeye alikuwa anawafuata askari kubishana nao hata baada ya kuonekana wale askari wanaondoka toka ktk eneo la tukio bila kumkamata na kabla hata askari hajahamaki na kufyatua risasi.
Askari ametumia kodi kuchezea risas za walipa kodi
 
Ukiwa kiongozi unaruhusiwa kuwa JEURI?Mjue mnawapa sifa viongoz kwa kauli zenu
Nisome vizuri. Wapi nimempa kiongozi sifa, nimesema repeatedly nini kingetokea kama angetoa gari pale bila shurti?
 
Ukweli nataka nimtetee Malima ila nashindwa ukweli kuna chuki ambayo si yalazima inapandwa dhidi ya vyombo vya usalama hapa nchini ambavyo vinajitahidi sana kufata sheria ila watu design ya malima wamekuwa wakipotosha hasa wanapokuwa madarakani mi najua katika hatua ya kwanza kabisa kama wangekubali kutii sheria yale yasingetokea wala tusingeona clip isipokuwa mpaka walipoanza kukaidi
Na wananchi wakaanza kuzomea polisi kweli kabisaaa!!!!tumefika hatua anaesimamia sheria ni mbaya na anaevunja ni mzuri Nasema naunga mkono jeshi la polisi
 
Unazungumza vipi na mtu asiyetaka kufuata sheria wala kutii amri. Nini kingetokea kama angetoa gari alipokua amepaki. Ni kweli polisi alienda mbali ila naona kama tunampa lawama bure bila kuangalia chanzo chake. Malima alitaka kutumia diplomatic immunity vibaya na kuonyesha jeuri mbele ya watu kasahau hata si kiongozi tena.

Malima angetoa gari pale bila shurti yasingetokea yote haya.
Ni kweli kinachoonekana hapa ni kuwa tatizo limezaa tatizo...kama gar ingeondoshwa risasi zisingelindima
 
Back
Top Bottom