Neno La Leo: Adam Malima Na ' Trigger Happy Police'

Binafsi Iyo Video Ninayo Katika Simu Na inaonyesha vizr Tuu

Nimeliangalia hilo Tukio kwa umakin Sana Sijaona kosa la polis

Bali Kosa Lipo Kwa Adam Malima

Amefanya kosa Ila Anataka Kutumia Uwazir mstaafu Katika uvunjifu wa sheria

Mara ya kwanza polis walienda wakamwambia toa Iyo Gar Malima Akagoma Kuna Askar Ambae Hakuwa amavaa Kot Akawa kama anambembeleza Malima na yure askali Mwenzake yule Askar mwenzake akawa anasema Namnukuu Kwanin Hawa watu Hawatii Sheria akawa anaongea kwa uchungu Sana yule Askar

Badae Akaja mkuu Wa ule Msafara Kesi Ikabadilika Kuwa toa Gari Mpaka Unashatakiwa kwa kosa la kukahid agizo Za Jesh La Polis

Mwisho Niseme Ivi Vyombo vyetu Wakat Mwingine Vinafanya mambo Vzr Ila kutokana Na watanzania wengi Kutawaliwa na Siasa Za Mihemuko Tunaona yule Askar amefanya makosa
 
..katika video uliyonayo umeona yule askari alivyokuwa akimfokea na kumsukuma-sukuma Mh.Malima?

..je ana haki ya kufanya vile?

..je Mh.Malima naye angemsukuma yule askari nini kingetokea?

..Askari anatakiwa kufoka na kujigamba namna ile huko akifyatua MARISASI hewani?
 
Double standard kila kona. Kupaki gari vibaya ni kosa dogo la kumuonya tu mwenye makosa, lakini serikali ya awamu ya tano imegeuza makosa ya watu wake kuwa mtaji. Usalama barabarani wanatumia ubabe kubambikiza makosa, same kwa madalali, wanatembea na polisi kukamata watu waliopaki magari vibaya wakati polisi hao walitakiwa kulinda raia. Hatuwezi kufika kwa ubabe huu, tutauana 2020
 
Acha kulialia ndungu..dharau waache kwanza afu mengine yapo tu.

Asikali ndo waogope raia?

Embi acheni kupotosha hapa.

Malima ni raia tu..hakutakiwa kuonyesha ubabe wa namna yoyote..angetii tu sheria na mengine yakafuata.

Afu nyie ndo mnatubagua raia.
Eti wengine wa class A wengine class Class 0.
Kuna ubabe wa Malima umeuona kwenye hiyo clip inayoonekana au ulikuwepo hivyo unataarifa zaidi ya hiyo tunayoiona wengine?
 
Maggid Mjengwa wewe ni hovyo sana. Sheria haitambui kiongozi na asiye kiongozi. Ndiyo maana kwa Kiswahili tunasema sheria ni msumeno. Kwenye sheria wote ni sawa; sasa unaanzaje kutuambia Malima sijui ni alikuwa Kiongozi ... sijui angeitwa polisi angeenda tu bila shuruti .... aisee! Kweli mimi Magufuli sikubaliani naye kwenye mambo mengi ila nitamshukuru sana Rais kama atakwamisha juhudi zako zote za kutaka dhamana ya kutuongoza. Hakika wewe hovyo sana. Utawala wa sheria ni kitu cha muhimu sana; na kwenye utawala wa sheria kinachoangaliwa ni nani ametii au kuvunja sheria - kwa kuzingatia "evidence". Siyo career background yako mjomba.
Yanaingiaje hayo ya dhamana ya uongozi?

Jibu kwa hoja na si maneno ya kejeli(matusi)
 
Ila kama vyeti feki kwao labda ni rwanda maana . maagizo ni kutoka juu sitaki mtu kiongozi na aliyekuwa kiongozi kumnyenyea isipokuwa juu kwenyewe ndio maana bunge ×
Mahakama×
Makamu waku juu×
Mawaziri×
Vyombo vya habari×
Raia×
Nisipoongea mimi huku juu basi basi phd yangu niliyoipatia kule rwanda itakuwa feki huku juu niseme na wewe useme nani atamsiliza mwenzie

Mnategemea nani ataitwa pembeni abebelezwe ili tuonekane huku juu tuko wengi .huku juu atakaa mtu mmoja tu ambaye nipo baada ya kuajast vikura vya yule na nikachukua mimi sasa inaonyesha wanawashwa. Iliyobaki ni kukunatu.
 
Tatizo hawa polisi wamepewa kiburi na hii serikali ya awamu ya5 wakati weengi wao wana vyeti bandia,na watatunyanyasa kweli kufika2020 tutakuwa tumenyooka
 
Ndugu zangu,

Majuzi hapa nilifika Newala, Mtwara. Pale Newala kuna ofisi nilisahau mahali ilipo. Katika kuzunguka Newala Mjini huku nikiiulizia, wengi hawakuijua.

Nikafika mahali nikaona kulia Kituo cha Polisi na polisi kadhaa wakiwa nje, na kushoto Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi, Wilaya.

Nikamwambia mwenzangu kwenye gari, kuwa afadhali, sasa twende Kituoni polisi watusaidie ilipo ofisi tunayoitafuta.

Mwenzangu akashauri twende tukaulize CCM Wilaya. akaongeza kusema, kuwa kuuliza polisi linaweza likazuka jingine.

Jibu hilo lilinifanya nitafakari sana. Maana, kwangu mimi, raia tunapaswa kuwa na imani na jeshi la Polisi. Tunapaswa kuheshimu polisi, lakini si kuogopa polisi.

Trigger happy police ina maana ya polisi anayefurahia kufyatua risasi. Ni kama vile wamekaa muda mrefu bila kufyatua na vidole vinawasha.

Naam, nimeangalia mtandaoni video ya tukio la Masaki likimuhusisha aliyekuwa Waziri wa Serikali, Adam Malima.

Mimi limenihuzunisha, maana, kwangu niliona jambo dogo sana ambalo halikuhitaji purukushani ile mpaka polisi kufyatua risasi hewani.

Polisi walikuwa kwenye majukumu yao, na Adam Malima, ni kiongozi. Palihitajika uwepo wa mazungumzo tu na jambo lile lingemalizika kwa dakika kadhaa tu.

Nchi yetu ni ya amani sana. Hatuna mazoea ya milio ya risasi. Yasifanywe kuwa mazoea mapya. Polisi wenye furaha ya kufyatua risasi yumkini ni wachache, kuna polisi wengi wenye weledi na kazi zao na wenye kutambua kuwa hufyatui risasi pasipo na lazima ya kufanya hivyo.

Na viongozi si malaika, kuna mahala nao wanaweza kukosea. Kama polisi anabaini hilo, basi, atumie weledi wake katika kumuelewesha kiongozi husika taratibu zinavyotaka. Na hata kama atahitajika afike kituoni, kama kiongozi, hawezi kupotea, ataitwa atafika mwenyewe kituo cha Polisi.

Kimsingi, raia hupendezwa na uwepo wa mazingira ya raia kuheshimu mamlaka, na si kuogopa mamlaka, ikiwamo jeshi la polisi. Hivyo, raia hawapendi na hufadhaishwa kuona udhalilishaji wa raia wenzao kutoka kwa wenye mamlaka, wala kudhalilishwa kwa viongozi wao, tena hadharani.

Ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa.
Hapatakuwa na urafiki tena,.Kuna mheshimiwa,mmoja alishasema, "tukinyamaza, basi mtatukumbuka"
 
Unajua, kuna,mambo ambayo tunatakiwa kutafakari kabla ya kuchukua hatua,yeyote. Je, Mheshimiwa Malima alionyesha reaction yeyote ambayo ni mbaya kwa.Jeshi letu tukufu,,alionyesha resistence yeyote ya kupinga sheria ya utii bila shurti? Je,,raia walionyesha fujo dhidi ya polisi wakati kamanda akitekeleza majukumu yake mpaka akaamua kufyatua risasi kuwatawanya watu?
Hapa, hatujui labda kama kuna ushahidi mzuri wa video hapo tynaweza kusema, maana jana kwenye,taarifa ya habari ya saa,2usuku, kamanda mh Siro alisema, "kufatua risasi ilikuwa ni lazima ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika na kuwazomea polisi"
 
Hivi neno happy silijuii au ninyi ndiof hamlijui! Huku unasema alikuwa anatulizwa na mwenzake wakati huo huo unasema alikuwa happy. Tunatuliza mtu mwenye huzuni ama mwenye hasira ila si mtu mwenye furaha!
..kwa viwango vya Tz yule askari ni trigger happy

.tena amejaa ubabe na majigambo.

..mwenzake aliyekuwa akimtuliza alionekana kui-handle ile situation much better.
Bahati mbaya sana mleta mada ni mvivu kupindukia kujibu hoja za wachangiaji wa uzi wake.
 
Ndugu zangu,

Majuzi hapa nilifika Newala, Mtwara. Pale Newala kuna ofisi nilisahau mahali ilipo. Katika kuzunguka Newala Mjini huku nikiiulizia, wengi hawakuijua.

Nikafika mahali nikaona kulia Kituo cha Polisi na polisi kadhaa wakiwa nje, na kushoto Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi, Wilaya.

Nikamwambia mwenzangu kwenye gari, kuwa afadhali, sasa twende Kituoni polisi watusaidie ilipo ofisi tunayoitafuta.

Mwenzangu akashauri twende tukaulize CCM Wilaya. akaongeza kusema, kuwa kuuliza polisi linaweza likazuka jingine.

Jibu hilo lilinifanya nitafakari sana. Maana, kwangu mimi, raia tunapaswa kuwa na imani na jeshi la Polisi. Tunapaswa kuheshimu polisi, lakini si kuogopa polisi.

Trigger happy police ina maana ya polisi anayefurahia kufyatua risasi. Ni kama vile wamekaa muda mrefu bila kufyatua na vidole vinawasha.

Naam, nimeangalia mtandaoni video ya tukio la Masaki likimuhusisha aliyekuwa Waziri wa Serikali, Adam Malima.

Mimi limenihuzunisha, maana, kwangu niliona jambo dogo sana ambalo halikuhitaji purukushani ile mpaka polisi kufyatua risasi hewani.

Polisi walikuwa kwenye majukumu yao, na Adam Malima, ni kiongozi. Palihitajika uwepo wa mazungumzo tu na jambo lile lingemalizika kwa dakika kadhaa tu.

Nchi yetu ni ya amani sana. Hatuna mazoea ya milio ya risasi. Yasifanywe kuwa mazoea mapya. Polisi wenye furaha ya kufyatua risasi yumkini ni wachache, kuna polisi wengi wenye weledi na kazi zao na wenye kutambua kuwa hufyatui risasi pasipo na lazima ya kufanya hivyo.

Na viongozi si malaika, kuna mahala nao wanaweza kukosea. Kama polisi anabaini hilo, basi, atumie weledi wake katika kumuelewesha kiongozi husika taratibu zinavyotaka. Na hata kama atahitajika afike kituoni, kama kiongozi, hawezi kupotea, ataitwa atafika mwenyewe kituo cha Polisi.

Kimsingi, raia hupendezwa na uwepo wa mazingira ya raia kuheshimu mamlaka, na si kuogopa mamlaka, ikiwamo jeshi la polisi. Hivyo, raia hawapendi na hufadhaishwa kuona udhalilishaji wa raia wenzao kutoka kwa wenye mamlaka, wala kudhalilishwa kwa viongozi wao, tena hadharani.

Ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa.

Wanaonyesha ujasiri - kamanda siro
 
Tatizo siyo Polisi,tatizo ni aina ya uongozi tulionao kwa kipindi hiki.
 
Kutetea upumbavu aliofanya yule askari etu kwa sababu alidharauliwa ni ujinga mkubwa kwenye swala la matumizi ya nguvu na siraha ya moto.

Vyovyote iwavyo askari aliepata mafunzo na akawiva lile sio swala la mkumfanya option pekee ilikuwa kufyatua risasi (warning shot) kwa mtu ambaye hakuwa ameyaweka maisha yao hatarini.

Kwenye mafunzo askari hupata shuruba na matusi mazito ambayo huwezi yaandika hapa. Hayo hufanyika makusudi kujenga mentality ya askari kucontrol temper. So to me ule haukuwa udhalilishaji wa kumfanya askari njia pekee iwe warning shot.

Inawezekana Malima alikosea, lakini askari alitumia makosa ya Malima kufanya makosa zaidi yenye athari kuliko ya Malima.

What if kungekuwa na ndege ndogo inapita usawa ule? What if kungekuwa na jengo refu? What if risasi ingepiga nyaya za umeme. Hiyo athari huioni? Mtu anaona eti Malima anadharau! Simtetei ila nabaki kwenye maadili ya uaskari.

Matumizi ya siraha ya moto yana miiko yake mikuu minne na ya zile 5 circumstances ambazo askari amezisoma kwenye rules of engagement model ya use of force. Akazielewa na akaapa kuzifuata ndio akakabidhiwa bunduki toka armoury.

Ni kwa raia wa kawaida ambaye haijui miiko ya matumizi ya siraha ya moto uwenda ndio akashabikia kitendo kile. Nilisema kama ningekuwa in charge wake siku hiyo angefikia rumande na asingepewa siraha mpaka afanye refresher course ya rules of engagement na confrontation skills.
 
Ndugu zangu,

Majuzi hapa nilifika Newala, Mtwara. Pale Newala kuna ofisi nilisahau mahali ilipo. Katika kuzunguka Newala Mjini huku nikiiulizia, wengi hawakuijua.

Nikafika mahali nikaona kulia Kituo cha Polisi na polisi kadhaa wakiwa nje, na kushoto Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi, Wilaya.

Nikamwambia mwenzangu kwenye gari, kuwa afadhali, sasa twende Kituoni polisi watusaidie ilipo ofisi tunayoitafuta.

Mwenzangu akashauri twende tukaulize CCM Wilaya. akaongeza kusema, kuwa kuuliza polisi linaweza likazuka jingine.

Jibu hilo lilinifanya nitafakari sana. Maana, kwangu mimi, raia tunapaswa kuwa na imani na jeshi la Polisi. Tunapaswa kuheshimu polisi, lakini si kuogopa polisi.

Trigger happy police ina maana ya polisi anayefurahia kufyatua risasi. Ni kama vile wamekaa muda mrefu bila kufyatua na vidole vinawasha.

Naam, nimeangalia mtandaoni video ya tukio la Masaki likimuhusisha aliyekuwa Waziri wa Serikali, Adam Malima.

Mimi limenihuzunisha, maana, kwangu niliona jambo dogo sana ambalo halikuhitaji purukushani ile mpaka polisi kufyatua risasi hewani.

Polisi walikuwa kwenye majukumu yao, na Adam Malima, ni kiongozi. Palihitajika uwepo wa mazungumzo tu na jambo lile lingemalizika kwa dakika kadhaa tu.

Nchi yetu ni ya amani sana. Hatuna mazoea ya milio ya risasi. Yasifanywe kuwa mazoea mapya. Polisi wenye furaha ya kufyatua risasi yumkini ni wachache, kuna polisi wengi wenye weledi na kazi zao na wenye kutambua kuwa hufyatui risasi pasipo na lazima ya kufanya hivyo.

Na viongozi si malaika, kuna mahala nao wanaweza kukosea. Kama polisi anabaini hilo, basi, atumie weledi wake katika kumuelewesha kiongozi husika taratibu zinavyotaka. Na hata kama atahitajika afike kituoni, kama kiongozi, hawezi kupotea, ataitwa atafika mwenyewe kituo cha Polisi.

Kimsingi, raia hupendezwa na uwepo wa mazingira ya raia kuheshimu mamlaka, na si kuogopa mamlaka, ikiwamo jeshi la polisi. Hivyo, raia hawapendi na hufadhaishwa kuona udhalilishaji wa raia wenzao kutoka kwa wenye mamlaka, wala kudhalilishwa kwa viongozi wao, tena hadharani.

Ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa.
Maggid uliona clip vizuri? Malima alikuwa mbabe anauliza WEWE NI NANI mara HUNA MAMLAKA huku amrweka mikono yake mfukoni. Askari alikuwa kazini kama angedharauliwa akamwacha aende tu askari angepata wapi moyo wa kuwakamata wahalifu wengine? Raia "wema" walikuwa wameshaanza kumzomea askari na kumzonga; ni wazi taasisi nzima ya polisi ingedharaulika. Kwa nini unamtetea Malima, ni lipi zuri alilofanya hapo? Kumbuka kiongozi unatakiwa kuwa mfano wa utii wa sheria. Trigger happy? Polisi ni jeshi, si boy scouts. Ukimchezea njia pekee aliyonayo kukukamata ni kutumia nguvu, na police orders zinasema kabla hujatumia nguvu toa onyo. Bila kupiga risasi juu Malima angeshinda na polisi wangeshitakiwa kwa kosa la COWARD.
 
Back
Top Bottom