Ndugu zangu,
Majuzi hapa nilifika Newala, Mtwara. Pale Newala kuna ofisi nilisahau mahali ilipo. Katika kuzunguka Newala Mjini huku nikiiulizia, wengi hawakuijua.
Nikafika mahali nikaona kulia Kituo cha Polisi na polisi kadhaa wakiwa nje, na kushoto Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi, Wilaya.
Nikamwambia mwenzangu kwenye gari, kuwa afadhali, sasa twende Kituoni polisi watusaidie ilipo ofisi tunayoitafuta.
Mwenzangu akashauri twende tukaulize CCM Wilaya. akaongeza kusema, kuwa kuuliza polisi linaweza likazuka jingine.
Jibu hilo lilinifanya nitafakari sana. Maana, kwangu mimi, raia tunapaswa kuwa na imani na jeshi la Polisi. Tunapaswa kuheshimu polisi, lakini si kuogopa polisi.
Trigger happy police ina maana ya polisi anayefurahia kufyatua risasi. Ni kama vile wamekaa muda mrefu bila kufyatua na vidole vinawasha.
Naam, nimeangalia mtandaoni video ya tukio la Masaki likimuhusisha aliyekuwa Waziri wa Serikali, Adam Malima.
Mimi limenihuzunisha, maana, kwangu niliona jambo dogo sana ambalo halikuhitaji purukushani ile mpaka polisi kufyatua risasi hewani.
Polisi walikuwa kwenye majukumu yao, na Adam Malima, ni kiongozi. Palihitajika uwepo wa mazungumzo tu na jambo lile lingemalizika kwa dakika kadhaa tu.
Nchi yetu ni ya amani sana. Hatuna mazoea ya milio ya risasi. Yasifanywe kuwa mazoea mapya. Polisi wenye furaha ya kufyatua risasi yumkini ni wachache, kuna polisi wengi wenye weledi na kazi zao na wenye kutambua kuwa hufyatui risasi pasipo na lazima ya kufanya hivyo.
Na viongozi si malaika, kuna mahala nao wanaweza kukosea. Kama polisi anabaini hilo, basi, atumie weledi wake katika kumuelewesha kiongozi husika taratibu zinavyotaka. Na hata kama atahitajika afike kituoni, kama kiongozi, hawezi kupotea, ataitwa atafika mwenyewe kituo cha Polisi.
Kimsingi, raia hupendezwa na uwepo wa mazingira ya raia kuheshimu mamlaka, na si kuogopa mamlaka, ikiwamo jeshi la polisi. Hivyo, raia hawapendi na hufadhaishwa kuona udhalilishaji wa raia wenzao kutoka kwa wenye mamlaka, wala kudhalilishwa kwa viongozi wao, tena hadharani.
Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa.