Neno La Leo: Adam Malima Na ' Trigger Happy Police'

Neno La Leo: Adam Malima Na ' Trigger Happy Police'

Kamwene Mkuu maggid , ama kweli leo umeongea ki utu uzima na busara sana. Tafadhali jongea maeneo ya kilabu cha msichoke pande za makorongoni, kuna wugimbi na wulanzi kidogo nimekuandalia. Ukitoka hapo lunch kwa mama siyovelwa.
 
Nashangaa kwann yule polisi zile risasi alipiga alitakiwa apige kwenye miguu ya malima,anadhani kuwa bado kiongozi jamaa anadharau sana tangu akiwa waziri aliwahi kwenda uwanja wa taifa akiwa na watu watano hawa tiket lakini akalazimisha waingie kisa yeye waziri kwavile alikuwa waziri askari wakanyamaza akaingia na watu wake kwa dharau kubwa sana nadhani alifikiri bado ni waziri,mjinga sana.
Mawaziri wa aina hyo ndo walofilisi mashirika ya Umma kama ATCL na mengineyo kwa kutaka kila kitu bure kisa vyeo vyao. Leo bado wanaendekeza ubwanyenye wao wakisahau kuwa enzi hizo zimepita.
 
Inatia mashaka unatumia nini kufikiri, yumkini tumbo sio bure!!!
Naona umetaja ''tumbo'', ''kufikiri'', hvo vote unavihusianisha vipi na maoni kuhusu upuuzi wa Malima ambae mpk sasa ni mtuhumiwa kortini? The fact that the police officer has not been punished and Malima has been brought to court for his alleged offence,the picture of the whole saga is clear. Let the law take its course.
 
Ndugu zangu,

Majuzi hapa nilifika Newala, Mtwara. Pale Newala kuna ofisi nilisahau mahali ilipo. Katika kuzunguka Newala Mjini huku nikiiulizia, wengi hawakuijua.

Nikafika mahali nikaona kulia Kituo cha Polisi na polisi kadhaa wakiwa nje, na kushoto Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi, Wilaya.

Nikamwambia mwenzangu kwenye gari, kuwa afadhali, sasa twende Kituoni polisi watusaidie ilipo ofisi tunayoitafuta.

Mwenzangu akashauri twende tukaulize CCM Wilaya. akaongeza kusema, kuwa kuuliza polisi linaweza likazuka jingine.

Jibu hilo lilinifanya nitafakari sana. Maana, kwangu mimi, raia tunapaswa kuwa na imani na jeshi la Polisi. Tunapaswa kuheshimu polisi, lakini si kuogopa polisi.

Trigger happy police ina maana ya polisi anayefurahia kufyatua risasi. Ni kama vile wamekaa muda mrefu bila kufyatua na vidole vinawasha.

Naam, nimeangalia mtandaoni video ya tukio la Masaki likimuhusisha aliyekuwa Waziri wa Serikali, Adam Malima.

Mimi limenihuzunisha, maana, kwangu niliona jambo dogo sana ambalo halikuhitaji purukushani ile mpaka polisi kufyatua risasi hewani.

Polisi walikuwa kwenye majukumu yao, na Adam Malima, ni kiongozi. Palihitajika uwepo wa mazungumzo tu na jambo lile lingemalizika kwa dakika kadhaa tu.

Nchi yetu ni ya amani sana. Hatuna mazoea ya milio ya risasi. Yasifanywe kuwa mazoea mapya. Polisi wenye furaha ya kufyatua risasi yumkini ni wachache, kuna polisi wengi wenye weledi na kazi zao na wenye kutambua kuwa hufyatui risasi pasipo na lazima ya kufanya hivyo.

Na viongozi si malaika, kuna mahala nao wanaweza kukosea. Kama polisi anabaini hilo, basi, atumie weledi wake katika kumuelewesha kiongozi husika taratibu zinavyotaka. Na hata kama atahitajika afike kituoni, kama kiongozi, hawezi kupotea, ataitwa atafika mwenyewe kituo cha Polisi.

Kimsingi, raia hupendezwa na uwepo wa mazingira ya raia kuheshimu mamlaka, na si kuogopa mamlaka, ikiwamo jeshi la polisi. Hivyo, raia hawapendi na hufadhaishwa kuona udhalilishaji wa raia wenzao kutoka kwa wenye mamlaka, wala kudhalilishwa kwa viongozi wao, tena hadharani.

Ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa.
SUFURI kabisa
Kwa kuwa biased
 
.... Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyo wengi tumesahau itikadi hii cheo ni dhamana ...sitakitumia cheo changu wala cha MTU mwingine kwa faida yangu ... Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko ......

Leo mheshimiwa kesho mtu wa kawaida sana
 
wajua yaweza kuwa ni ngumu lakini kwa ninavyoelewa kupitia baadhi ya rafiki na jamaa zangu police, nimeanza kuwaogopa na kuwakwepa maana katika mazungumzo yao dhahiri shahiri wanachukia raia na hasa ukiwa na mafanikio fulani ambayo anaona kana kwamba anapaswa kuwa nayo yeye.
chuki hizi sio kwa raia tu hata kwa viongozi wao....
inasikitisha
 
Police yetu means Command - yaani tii amri kwanza bila shuruti, kuhoji ni baadaye - ukigoma utakwenda tu hata kwa tanganyika jeki.
 
Pengine maana ya trigger happy inakupiga chenga.... hivi kama kweli police wetu yule angekuwa trigger happy asingeli limlamba shaba ya miguu yule Malima? mtu ana wazuia watu kufanya kazi yao wazi wazi ana tegemea nini?
 
Kwenye ile clip yenyewe kuna baadhi ya majawabu.

Ni kwa nini huyo polisi mwingine anaonekana kumzuia mwenzake "kutimiza wajibu wake"? Hakubaliani na hatua alizokuwa anachukuwa mwenzake? Kwa nini na yeye ashitakiwe kwa "woga"?
 
Maggid Mjengwa wewe ni hovyo sana. Sheria haitambui kiongozi na asiye kiongozi. Ndiyo maana kwa Kiswahili tunasema sheria ni msumeno. Kwenye sheria wote ni sawa; sasa unaanzaje kutuambia Malima sijui ni alikuwa Kiongozi ... sijui angeitwa polisi angeenda tu bila shuruti .... aisee! Kweli mimi Magufuli sikubaliani naye kwenye mambo mengi ila nitamshukuru sana Rais kama atakwamisha juhudi zako zote za kutaka dhamana ya kutuongoza. Hakika wewe hovyo sana. Utawala wa sheria ni kitu cha muhimu sana; na kwenye utawala wa sheria kinachoangaliwa ni nani ametii au kuvunja sheria - kwa kuzingatia "evidence". Siyo career background yako mjomba.
Unataka utawala wa sheria mbona mkulu wako haufwati huo utawala wa sheria
 
Na lazima polisi wawanyooshe Viongozi wasiojielewa kama kina Malima....na ana Bahati huyo askari ni mstaarabuu... Angekuwa Yule Afande Rasi angekuwa hata ashamuinamisha ...
 
Acha kulialia ndungu..dharau waache kwanza afu mengine yapo tu.

Asikali ndo waogope raia?

Embi acheni kupotosha hapa.

Malima ni raia tu..hakutakiwa kuonyesha ubabe wa namna yoyote..angetii tu sheria na mengine yakafuata.

Afu nyie ndo mnatubagua raia.
Eti wengine wa class A wengine class Class 0.
Ukielewa maana ya Police utaelewa wanaoajiriwa huko ni watu wa aina gani. Mkoloni aliajiri Polisi kwa kuzingatia kuwa ni mtu asiyefikiri anaambiwa nini zaidi ya kutenda kile alichogizwa. Uwezo wa Polisi kufikiri ni mdogo mno.
 
Yote yale ni matokeo ya dharau kwa askari iv kulikua na ugumu gn kufuata maelekezo aliyopewa au bd ana ubabe wa form two kwa form one,,cjawai ona jwtz wanamwambia mtu utakiwi kua eneo hili alaf mtu huyo akagoma kutii agizo coz anajua atakachokipata...askari wetu wanazaraulika sana ilibd malima ale mitama ya kutoxha...
 
Back
Top Bottom