NENDA CHUO , NENDA MDOGO WANGU By Jonathan Kwizera ( JK)

Bakulutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2011
Posts
2,597
Reaction score
1,868
NENDA CHUO , NENDA MDOGO WANGU.

Nakupongeza kwa kufaulu kwenda Chuo Kikuu , aya nenda Mdogo wangu.

Wanafunzi wengi watapata mkopo , na wewe utapata mdogo wangu nenda.

Najua hujawahi kumiliki hata elfu 20 ya kwako mdogo wangu.

Pesa uliyokuwa unapata ni ile mia 5 ya *Shikamoo baba /shikamoo mama , naomba nauli ya kwenda shule* .Najua mdogo wangu.

Nenda nenda mdogo wangu.

Ukifika chuo kikuu utamiliki akaunti benki kwa Mara ya kwanza mdogo wangu nenda .

Kwa Mara ya kwanza utamiliki laki saba za kwako nenda mdogo wangu.

Kutoka kwenye miatano ya shikamoo Baba naomba nauli ya shule mpaka laki saba nenda mdogo wangu.

Ukipata laki saba utakosa cha kuifanyia nenda mdogo wangu.

Ukikosa cha kuifanyia utanunua Simu kama zote , PC kama zote , utawatumia pesa nyumbani bila hata kuombwa , utaenda club kama zote ila mwisho utarudi nyumbani Itigi.Nenda Mdogo wangu.

Nenda nenda mdogo wangu .

Mdogo wangu , hujawahi kufanya *Birthday Party* ila utafanya Chuo Mdogo wangu.

Utachukua laki tatu siyo nyingi mtatumia kwa Siku moja ya sherehe yako mdogo wangu .Kwani wewe ndo hupendi kuburudika mdogo wangu? Nenda mdogo wangu lakini ukimaliza Chuo hufanyi tena Birthday party mdogo wangu.

Nenda Chuo , nenda Mdogo wangu.

Kwani wewe hupendi kwenda Club ukalewe , wewe hupendi kuzijua beach kama zote za mjini. Nenda Mdogo wangu ila ukimaliza Chuo utakosa nauli ya kukurudisha nyumbani kwenu Itigi mdogo wangu.

Nenda chuo Nenda Chuo Mdogo wangu.

Najua hapo shuleni ulikuwa unawaona wanawake unatamani kuwaona kila kitu , mpaka unaenda na kioo shuleni ili ukawachungulie , *aya nenda chuo nenda Chuo Mdogo wangu*.Kona hii utakutana na Mchekoslovakia , kona ila utakutana na mnyarwanda , pale Mzungu mtanzania , hautohtaji vioo tena , hata ukipanda juu ya mti na yeye akiwa chini utaona unachokitaka ila nenda Ukimwi upo kama wote Mdogo wangu.

Nyumbani kwenu wewe ndiye umebahatika kufika Chuo kikuu mdogo wangu, umefka Chuo kwa lift ya Mjomba /Shangazi /Bamdogo kwasababu kwenu hamjiwezi Mdogo wangu. Soma miaka mitatu urudi tena kukaa kwa mjomba au shemeji yako Mdogo wangu.Nenda Chuo Nenda Mdogo wangu.

Nenda Chuo , Nenda Mdogo wangu.

Ni Elimu ambayo utaamua uingie darasani au usiingie , uandike au usiandike na ukiandika ukifanya mtihani utachana daftari mdogo wangu.Nenda

Ni pale ambapo Dada zako waliotumia Pesa vibaya utawakuta kwenye madanguro , utachagua aidha kuwa mteja wao au kufumba macho yote yapite na wewe ubaki imara.Nenda Ndogo wangu nenda .
Nenda Chuo , nenda Mdogo wangu.

Ni Chuo pale ambapo hutaweza kujifulia wala kujifatia Chakula , bali Pesa itafanya yote kwa ajili yako nenda Chuo Nenda, ila ukimaliza Chuo utayaweza nenda .

Nenda Mdogo wangu nenda .

Nenda Chuo, sehemu utakayohisi kwamba *Ukimalilza Chuo unaenda kwenye ile Ofsi ya ndoto yako, utakayohisi kuwa ukihtimu unamiliki maisha ya ndoto yako* , lakini usopoweka mipango vizuri ukimaliza utamiliki stress badala ya kazi na ofsi yako itakuwa ni bar kwenye gongo na Chang'aa. , nenda chuo Mdogo wangu nenda.

Nenda Mdogo nenda.

Ukiishiwa Pesa ujitahidi tu kuweka Voucher na uwe na Namba ya Waziri Wa mikopo .Kazi yako iwe kumtumia SMS *Pesa yetu mbona hamjaweka*?
Nenda Chuo Nenda Mdogo wangu.

Ninayo mengi ya kukusihi mdogo wangu ila tutaendelea kukumbushana , Ondoka na haya kwa leo *Kila anayefurahia maisha leo , alipata tabu sana Jana na kila anayepata tabu sana leo atafurahia maisha kesho*

Jonathan Kwizera (JK)
Author & Motivational Speaker
+255757741748
kwizerajonathan99@gmail.com
 
Laki tano kwa miezi miwili afu mnasema wakale bata.
Kwa wale ambao hawajawahi kushika pesa zao wenyewe ndio wataona ni pesa ndefu bila kujua kuwa inatumika kwa miezi miwili.
 
Mambo yote hayo yanafanywa na hela ya boom?

Pambanua tuu mbona rahisi kung’amua . Sio lazima yote hata . Kuna mengi mwandishi hajaweka ila hata haya machache ni wasio tosha.
 
Laki tano kwa miezi miwili afu mnasema wakale bata.
Kwa wale ambao hawajawahi kushika pesa zao wenyewe ndio wataona ni pesa ndefu bila kujua kuwa inatumika kwa miezi miwili.

Wangapi wanashika hii pesa zao wenyewe wakiwa shule ? Simple mind!
 
Ni wachache ila wapo baadhi ya vijana walioachiwa urithi au wanaoendesha biashara pamoja na wazee wao au kaachiwa awe anachukua kodi ya nyumba.
Huyu anaweza kuzishika hizo pesa.
 
Wangapi katika kundi la wanafunzi 10 kwa mfano ?
 
namuunga mkono mtoa mada kwa wosia,inawezekana asiwepo kabisa aliyewahi kuishika,lakini tujue kuwa 90% ya wanafunzi wa chuo hubadilika tabia negatively wanapofika chuo tena plus wakipata boom...chukua hiyo taadhari kama wewe ni mmojawapo unakwenda chuo,cha msingi kasome kozi yako husika kiukamilifu huku ukiyasoma na mazingira,epuka yote aliyoyahusia mtoa mada na pia kumbuka uliyohusiwa na wazazi na uishi maisha ya kumpendeza Mungu siku zote,naamini kila mmoja ana Imani fulani,na uzuri hakuna Imani inayokubaliana na upuuzi wowote ule,Mshukuru Mungu kwa kuipata nafasi ya chuo.Take care, achana na maigizo ya maisha,ishi maisha yako,badilika kielimu na kistaarabu uive....uhuni sio kitu cha kujivunia,usitafute jina chuoni,tafuta Elimu bora...
 
NENDA CHUO , NENDA MDOGO WANGU.

Nakupongeza kwa kufaulu kwenda Chuo Kikuu , aya nenda Mdogo wangu.

Wanafunzi wengi watapata mkopo , na wewe utapata mdogo wangu nenda.

Najua hujawahi kumiliki hata elfu 20 ya kwako mdogo wangu.

Pesa uliyokuwa unapata ni ile mia 5 ya *Shikamoo baba /shikamoo mama , naomba nauli ya kwenda shule* .Najua mdogo wangu.

Nenda nenda mdogo wangu.

Ukifika chuo kikuu utamiliki akaunti benki kwa Mara ya kwanza mdogo wangu nenda .

Kwa Mara ya kwanza utamiliki laki saba za kwako nenda mdogo wangu.

Kutoka kwenye miatano ya shikamoo Baba naomba nauli ya shule mpaka laki saba nenda mdogo wangu.

Ukipata laki saba utakosa cha kuifanyia nenda mdogo wangu.

Ukikosa cha kuifanyia utanunua Simu kama zote , PC kama zote , utawatumia pesa nyumbani bila hata kuombwa , utaenda club kama zote ila mwisho utarudi nyumbani Itigi.Nenda Mdogo wangu.

Nenda nenda mdogo wangu .

Mdogo wangu , hujawahi kufanya *Birthday Party* ila utafanya Chuo Mdogo wangu.

Utachukua laki tatu siyo nyingi mtatumia kwa Siku moja ya sherehe yako mdogo wangu .Kwani wewe ndo hupendi kuburudika mdogo wangu? Nenda mdogo wangu lakini ukimaliza Chuo hufanyi tena Birthday party mdogo wangu.

Nenda Chuo , nenda Mdogo wangu.

Kwani wewe hupendi kwenda Club ukalewe , wewe hupendi kuzijua beach kama zote za mjini. Nenda Mdogo wangu ila ukimaliza Chuo utakosa nauli ya kukurudisha nyumbani kwenu Itigi mdogo wangu.

Nenda chuo Nenda Chuo Mdogo wangu.

Najua hapo shuleni ulikuwa unawaona wanawake unatamani kuwaona kila kitu , mpaka unaenda na kioo shuleni ili ukawachungulie , *aya nenda chuo nenda Chuo Mdogo wangu*.Kona hii utakutana na Mchekoslovakia , kona ila utakutana na mnyarwanda , pale Mzungu mtanzania , hautohtaji vioo tena , hata ukipanda juu ya mti na yeye akiwa chini utaona unachokitaka ila nenda Ukimwi upo kama wote Mdogo wangu.

Nyumbani kwenu wewe ndiye umebahatika kufika Chuo kikuu mdogo wangu, umefka Chuo kwa lift ya Mjomba /Shangazi /Bamdogo kwasababu kwenu hamjiwezi Mdogo wangu. Soma miaka mitatu urudi tena kukaa kwa mjomba au shemeji yako Mdogo wangu.Nenda Chuo Nenda Mdogo wangu.

Nenda Chuo , Nenda Mdogo wangu.

Ni Elimu ambayo utaamua uingie darasani au usiingie , uandike au usiandike na ukiandika ukifanya mtihani utachana daftari mdogo wangu.Nenda

Ni pale ambapo Dada zako waliotumia Pesa vibaya utawakuta kwenye madanguro , utachagua aidha kuwa mteja wao au kufumba macho yote yapite na wewe ubaki imara.Nenda Ndogo wangu nenda .
Nenda Chuo , nenda Mdogo wangu.

Ni Chuo pale ambapo hutaweza kujifulia wala kujifatia Chakula , bali Pesa itafanya yote kwa ajili yako nenda Chuo Nenda, ila ukimaliza Chuo utayaweza nenda .

Nenda Mdogo wangu nenda .

Nenda Chuo, sehemu utakayohisi kwamba *Ukimalilza Chuo unaenda kwenye ile Ofsi ya ndoto yako, utakayohisi kuwa ukihtimu unamiliki maisha ya ndoto yako* , lakini usopoweka mipango vizuri ukimaliza utamiliki stress badala ya kazi na ofsi yako itakuwa ni bar kwenye gongo na Chang'aa. , nenda chuo Mdogo wangu nenda.

Nenda Mdogo nenda.

Ukiishiwa Pesa ujitahidi tu kuweka Voucher na uwe na Namba ya Waziri Wa mikopo .Kazi yako iwe kumtumia SMS *Pesa yetu mbona hamjaweka*?
Nenda Chuo Nenda Mdogo wangu.

Ninayo mengi ya kukusihi mdogo wangu ila tutaendelea kukumbushana , Ondoka na haya kwa leo *Kila anayefurahia maisha leo , alipata tabu sana Jana na kila anayepata tabu sana leo atafurahia maisha kesho*

Jonathan Kwizera (JK)
Author & Motivational Speaker
+255757741748
kwizerajonathan99@gmail.com
usitutisheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee//// kama kuna kifest yia kizur humu kinitafute pm
 
Wewe kuna probabillity kubwa sana hata chuo hujafika.
Yaani mtubufanye yote hayo kwa pesa ya boom? Kwa io wewe kwa akili yako laki 5 miexi miwilli ule,ulipe kodi,ununue makorokoro kibao ya chuo nk bado ibaki pesa ya kwenda kula bata??
Wewe huna tofauti na ndalichako aliwai kusema kuna watu wamejenga na pesa ya boom
 
Pole ndugu , hapa panaitwa Home of Great Thinker! Uwe una jiongeza kidogo, Sio lazima uwe umeenda chuo ndio ujue maisha ya wanafunzi, unaweza kuta hata ni mfanyakazi anae fanya usafi kule UDSM, IFM n.k kwa miaka zaidi 10 na anajua tabia za wanafunzi kuliko alie soma .

We unaona laki 5 ndogo wenzio ndio mara ya kwanza anaishika kama yake , kwenye familia huko kijijini alisha zoea wana tumia sh elfu 10 kwa wiki 2 . Anaweza ona laki 5 ndio kila kitu hata darasani haiingii tena .

We huku muelewa Mama Ndalichako kabisa , kwani hakuna waliopata mkopo nawako vizuri sana kiuchumi kwao, unataraji kama anapewa pesa za kutosha kwao na nyumba labda kapewa hawezi tumia pesa ya zaida hata kuweka dirisha moja la almunium [emoji1][emoji1][emoji1] any way naandika sana ukute hata hunielewi🤚🏿🤚🏿
 
Back
Top Bottom