Singo Batan
JF-Expert Member
- Apr 24, 2020
- 292
- 191
Wanaobeza na kujilalamisha hapa wote hakuna mwenye facts za namna gani Tume ilifanya vibaya kwenye uchaguzi mkuu wa 2020. Wote wanakuja na porojo za WANASIASAMKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera ametoa wito kwa viongozi, wadau wote wa uchaguzi kuendelea kujipanga kikamilifu kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa bora, mzuri na kuaminika katika jamii na ulimwenguni kote.
Alisema hayo juzi wakati akifungua kikao cha wadau wa uchaguzi kujadili na kuchangia taarifa ya uchaguzi 2020, kilichoandaliwa na Kituo cha Amani Haki na Msaada wa Kisheria Tanzania (PLAJC). "Tanzania ni nchi yenye misingi ya demokrasia inayozingatia sheria, ni imani yangu mapendekezo yatakayotokana na kikao hiki yatajielekeza katika kuboresha na kuimarisha demokrasia nchini na hatimaye kukuza na kudumisha umoja na mshikamano wa kitaifa," alisema.
Alisema uchaguzi ni muhimu katika nchi kwani unaashiria kukua na kukomaa kwa demokrasia katika nchi, kupitia uchaguzi wananchi hupata fursa na kuchagua viongozi wanaowataka kwa hiari.
“Kwa upande mwingine uchaguzi unawafanya viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kwa kujiamini kwa kuwa wana ridhaa ya wananchi wanaowaongoza.
Pamoja na ukweli huo ili uchaguzi ukidhi malengo hayo ni lazima usimamiwe vizuri na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki,” alisema.
Mwenyekiti wa PLAJC, Leatitia Petro alisema kikao hicho ni kwa ajili ya kujadili na kuchambua taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ya NEC pamoja na taarifa mbalimbali za wadau wa ndani na nje waliopewa vibali na tume kuangalia uchaguzi mkuu 2020.
Alipongeza serikali kwa kugharamia shughuli za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa asilimia 100.
Pia alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujenga mazingira wezeshi kwa taasisi zisizo za kiserikali kuendelea kufanya kazi za kuleta maendeleo kwa wananchi.
Nchi ngumu sana hii.
Mahera endelea kupiga kazi na timu yako Mtoto wetu.
Sisi tunataka leadership transitions za amani. Hawa waongo wachache walozoea kushindwa tushawazoea