NEC yabadili majina ya majimbo matatu na kutangaza tarehe za kuchukua fomu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imebadilisha majina ya majimbo matatu, likiwemo jimbo la Chilonwa, ambalo kwa sasa linaitwa Chamwino, Jimbo la Mtera limebadilishwa na kuitwa Mvumi, na Jimbo la Kijitopele lililopo Wilaya ya Magharibi B linaitwa jimbo la Pangawe.
Source
EATV

2020
 
Taarifa kamili inakuja.

Source Radio One!
Unatakaa uwe wa kwanza kupost sio? Ndo akili zenu hizi ccm

Hii kubadilisha majina ya majimbo inamana asemacho raisi ni sheria? Jana tu aalisema kuna jimbo lipewe jinaa la Chamwino na leo hii mkurugenzi mwenye akili ya kikasuku kabadilisha
 
Figisu za nini sasa?
Si jina tu limebadilishwa kwani kuna nini zaidi?

Naweza kuwa nina mbwa wangu nikamuita Simba, akiwa legelege nitambadilisha na kuwa Koko/Nyumbu nk

Au kuna kitu ambacho sijui?
Vipi kuhusu vitambulisho vya kura wametoa muda wa kurekebisha? Vinginevyo kuna kura hazitapigwa.
 
Yaani mzee akikohoa tu utitiri unaanza kudondoka wenyewe! Mzee kazungumza jana tu leo tayari yameshabadili na majina ya majimbo?? Jaji unajishushia heshimaaaaa!!

Alisemaje jana mkuu??

Aliongelea majina ya majimbo?? Ilinipita hii
 
Yes, ilikuwa kwenye hafla ya kuzindua jengo la Uchaguzi na lile la TAKUKURU Chamwino, alisema anashangaa kwanini hilo jimbo lisiitwe Chamwino badala ya Chilonwa? Akasema namwachia Spika ma Waziri mkuu muangalie! Sasa hamaad leo tayari limeshabadilishwa!!
 
Ikumbukwe kwamba walioweka Majina ya Majimbo ya awali hawakuwa wajinga , waliifahamu Chamwino kuliko hawa viongozi wa sasa , kila jina lililowekwa lilikuwa na maana yake , hatuwezi kubadili asili ya jambo kwa kuzingatia ushauri wa mtu mmoja tu .

Baada ya Mh Rais kutoa mapendekezo yake kulikuwa na haja kwa tume ya uchaguzi kuwashirikisha wadau wengine vikiwemo vyama vya siasa na viongozi wa halmashauri zilizo kwenye maeneo yaliyobadilishiwa majina , wangeulizwa kama wanakubaliana na ushauri wa Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa ccm au la , huo ndio utaratibu , siyo kila linaloshauriwa na mkubwa basi lipitishwe tu , hii haikubaliki .

kitendo cha Mwenyekiti wa Tume kupitisha mabadiliko bila kushirikisha wadau si tu kwamba hakikubaliki bali pia kinaonyesha utii wake kwa mmoja wa Wagombea jambo linaloweza kuleta upendeleo huko tuendako , Jaji hakutakiwa kuburuzwa tu kama ilivyofanyika , na wala hakukuwa na sababu zozote za msingi za yeye kukurupuka , anaogopa nini ?

Kwa uoga alionao sioni kama anaweza kutenda haki kwenye uchaguzi unaokuja , maana inaonekana akitingishwa kidogo tu ataufyata .

TUTAENDELEA KUANIKA KILA UOZO KWA KADRI TUNAVYOUSTUKIA , hatutanyamaza
 
Back
Top Bottom