NEC yabadili majina ya majimbo matatu na kutangaza tarehe za kuchukua fomu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,862
NEC YATANGAZA TAREHE ZA KUCHUKUA FOMU KWA NAFASI MBALIMBALI ZA UCHAGUZI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC nchini imetangaza kuwa itaanza kutoa fomu za Urais kuanzia Agosti 5 hadi Agosti 25 mwaka 2020. Fomu za kugombea urais zitatolewa katika Ofisi Kuu za NEC zilizoko Njedengwa jijini Dodoma

Aidha fomu za ubunge na udiwani zitaanza kutolewa Agost 12 hadi Agosti 25 katika Ofisi za Wasimamizi wa Uchaguzi kwenye makao makuu za Halmashauri na kata husika

===

Pia NEC imekumbushia kuwa kampeni za uchaguzi zitaanza Agosti 25
Tume ya Uchaguzi imetangaza kubadili majina ya majimbo matatu ya uchaguzi bila kubadili idadi kamili ya majimbo nchini

Jimbo la Chilonwa na Jimbo la Mtera yaliyoko Halmashauri ya wilaya ya Chamiwno mkoani Dodoma yamebadilishwa majina, Jimbo la Chilonwa litaitwa Jimbo la Chamwino, na Mtera uwa Jimbo la Mvumi

Pia jimbo moja la visiwani Zanzibar, Jimbo la Kijito Upele lililoko wilaya ya Magharibi ‘B’ lililoko mjini Magharibi limebadilishwa jina na kuwa Jimbo la Pangawe

Aidha majimbo yamebaki kuwa 264 kama ilivyokuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2019, Tanzania bara ikiwa na majimbo 214 na Tanzania Zanzibar ikiwa na majimbo 50
 
Hawajagawa Kata?
 
Yaani mzee akikohoa tu utitiri unaanza kudondoka wenyewe! Mzee kazungumza jana tu leo tayari yameshabadili na majina ya majimbo?? Jaji unajishushia heshimaaaaa!!
 
Labda CCM mlete wapiga kura wenu toka Lindi/Mtwara nk
Lakini wakazi wa Mbeya kura zote ni kwa Sugu tu.
 
Back
Top Bottom