Uchaguzi 2020 NEC: Tulifanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum baada ya orodha ya majina hayo kuwasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA 19 Novemba 2020

Inasikitisha sana watu wasomi kabisa lakini ajabu wanabuluzwa hovyo na wana siasa kiasi hiki!!
Wafia vyama. Esther Matiko mke wa Mwalimu yule mgombea mwenza. Eti kaenda bungeni bila mmewe kujua. Mbowe wote hao wanajua sana na wapo Ok.

Sema wanaplay games ili kuwapoza wafia vyama ambao hajawahi hata faidika na Chadema. Mbowe anaingiza ruzuku tu. Mimi ndo maana nasema wote wawe Chadema,CCM .....etc. Tanzania ndo chama langu. Kura nitampigia mtu na siyo sababu ya chama chake.
 
Halima Mdee anasema wana baraka za mwenyekiti, katibu wa chama anasema hajatuma wala kuwasilisha majina ya wabunge wa viti maalumu wakati tume imesema imepokea majina kwa barua toka kwa katibu mkuu chadema tarehe 20/11/2020 hii movie imefika sehemu nzuri ngoja niagize popcorn
 
Nacheka Sana jinsi wee jamaa unavyobebwa hovyo na wanasiasa aisee inasikitisha sana.
Shituka mkuu huku tuendako siko maigizo yamezidi hapo kaka.

Nimecheka kwa nguvu, eti ninabebwa na wanasiasa. Hivi unadhani siwezi kuangalia na kupima uhalisia?
 
Tatizo lenu mnawaamini Sana viongozi wa chadema kana kwamba wao ni Malaika hapana
Hata kama umenyofolewa ubongo basi hata kupapasa huwezi ? hivi Unajua kwamba Nusrat alitolewa gerezani tarehe 23 usiku na Mdee akishirikiana na mfumo ? ni wapi katibu mkuu wa Chadema alimsainisha fomu Nusrat aliyewekwa selo tangu july 2020 ? halafu hata kama kichwani umewekwa udongo tangu lini ccm na Ndugai wakawa watetezi wa wabunge wa Chadema ?
 
Katibu ws Tume ya Uchaguzi na watumishi wa serikali wengine wengi wameweka rehani maisha yao kwa kulubali kutumiwa na wanasiasa waliopoteza uhalali na ambao uhai wao kisiasa hauwezekani tena bila kuvunja katiba na sheria ya nchi. Jinai haizeeki. Hakika kuna siku watawajibishwa.
 
Nimecheka kwa nguvu, eti ninabebwa na wanasiasa. Hivi unadhani siwezi kuangalia na kupima uhalisia?
Ungeweza usingekuwa hivyo kaka, huo ndio ukweli japo naamini huto ukubali.
( Uko timamu kabisa na huna tatizo lakini umeweka Imani zaidi kwa wana siasa kuliko kutumia vema jicho la tatu?
 
Hakuna kosa kubwa Tz kama kugushi sahihi ya mtu sasa kama NEC wamegushi mimi naomba Chadema wafungue kesi ya kugushi sahihi.

CHADEMA WAKIFUNGUA KESI NAOMBA MNITAG.
Ni mjinga pekee anae waza mahakama wakati mtoa hela ni mmoja tu
 
Back
Top Bottom