Ndugulile: Tozo za Daraja la Kigamboni zipunguzwe kurahisisha maisha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Wananchi wa Kigamboni wanashukuru sana kwa ujenzi wa Daraja la Nyerere. Ni mkombozi mkubwa. Changamoto ni tozo. Daladala moja inatozwa Sh5,000 ikienda mara kumi kwenda na kurudi ni Sh100,000 kwa siku. Hapo hajaweka mafuta, hajaweka hela ya tajiri-@DocFaustine

“Nakuomba sana Rais twende tukaliangalie jambo hili. tuangalie jinsi gani tunaweza kuleta nafuu kwa wananchi wa Kigamboni na kufanya maisha yawe mepesi. Wananchi wamenituma hilo niweze kulifikisha kwako,” amesema Ndugulile wakati Rais
@SuluhuSamia aliposimama Kibada, kusalimia.
 
Kama madereva wa daladala wanalalamika kulipia hiyo 5000 basi waruhusiwe kupandisha nauli, raia atakayeona ni gharama apige mbizi. Hakuna huruma, hizi kauli za wananchi wanyonge ndio zinachelewesha maendeleo, Tozo ni muhimu kwa ujenzi wa taifa!
 
Hili daraja limejengwa kwa bei ya kifisadi kutumia mfuko wa NSSF. Wizara ya ujenzi chini ya Magufuli walipinga sana gharama hizo lakini mwisho wake Rais Kikwete alimpelekaMagufuli wizara ya vitoweo na katibu mkuu wake Mhandisi Kijazi akapelekwa ubalozi India. Daraja likajengwa. Mpaka leo huo mzigo unalipwa na Watanzania.
 
Hili daraja limejengwa kwa bei ya kifisadi kutumia mfuko wa NSSF...wizara ya ujenzi chini ya Magufuli walipinga sana gharama hizo lakini mwisho wake Rais Kikwete alimpelekaMagufuli wizara ya vitoweo na katibu mkuu wake Mhandisi Kijazi akapelekwa ubalozi India..daraja likajengwa ...mpaka leo huo mzigo unalipwa na watanzania.
Kwahio Magufuli alipelekwa wizara ya vitoweo😅😅😅
 
Kama madereva wa daladala wanalalamika kulipia hiyo 5000 basi waruhusiwe kupandisha nauli, raia atakayeona ni gharama apige mbizi...hakuna huruma, hizi kauli za wananchi wanyonge ndio zinachelewesha maendeleo, Tozo ni muhimu kwa ujenzi wa taifa!
Duh..!
 
Hili daraja limejengwa kwa bei ya kifisadi kutumia mfuko wa NSSF...wizara ya ujenzi chini ya Magufuli walipinga sana gharama hizo lakini mwisho wake Rais Kikwete alimpelekaMagufuli wizara ya vitoweo na katibu mkuu wake Mhandisi Kijazi akapelekwa ubalozi India..daraja likajengwa ...mpaka leo huo mzigo unalipwa na watanzania.
Huo ndiyo ukweli
 
Yaani unafuu wa maisha uletwe kwa kupunguza tozo hiyo ya daladala?hiyo 5000 si ni kama gharama ya lita 2 tu tu za mafuta? Wakizungukia kongowe ni zaidi ya hizo lita 2, kwa hiyo hesabu iko pale pale tu, wanashindwa kupigia kelele vitu vya msingi eti tozo ya daladala/magari madogo!!
 
Alishindwa kushawishi akiwa waziri leo nani atamsikiliza? Hata mjumbe wa mtaa atampuuza tu!
Diko baba diko baba!! Angenyang' anywa diko mdomon 🤣🤣🤣 ukipata madaraka na ukae kwa kutulia ndugu yang ukijidai dai inakula kwako mazimaaaa NCHI ngum hii!!
 
Back
Top Bottom