Yaliyomshinda Mbunge wangu Kigamboni

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
69
252
Yaliyomshinda Mbunge wangu Kigamboni:

Sina pa kusemea, ukurasa wangu hapa facebook ndio kipaza Sauti changu.

Anyways, Sikuwa na matarajio mkubwa kwake kwa kuwa Sina Imani na kikundi cha watu(chama) kilichomweka kwenye nafasi hiyo, kwa mantiki hiyo pia Sishangazwi na jinsi anavyotupuuza wana Kigamboni.

Yes, neno zuri ni hilo tu, anatupuuza, anatuchukulia kirahisi saaaana, anatuona hatuna jeuri dhidi yake, hatuna la kufanya wala hatuna PA kumshitaki.

Yaani ndo kusema kwamba ana uhakika asilimia zaidi ya miamoja watu wa Kigamboni Daima dumu wao kura zao ni CCM tu bila kujua kwanini wanapiga hizo kura(hii ni kansa)

Kigamboni kama jimbo tunayo matatizo yetu mengi ya msingi ambayo nilitarajia ndio inge kuwa kipaumbele cha viongozi wetu na hasa Mbunge ambaye tumempigia kura.

Lakini ni bahati mbaya sana, huyu bwana mkubwa matatizo yetu yamemshinda na Sasa tunakwenda kimazoea mradi kukuche tu akisubiri awamu nyingine chama chake kimpitishe atudanganye tena kwa miaka mitano mingine kama alivyozoea.

Mengi yamemshinda, leo nitagusa machache tu:

1. Huduma ya Daraja la Kigamboni
Siku za nyuma alikaririwa Mbunge wetu akitupa lawama kwa aliyekuwa waziri wa ujenzi wa kipindi cha Rais mstaafu J. Kikwete kwamba ndiye alikuwa sababu ya matumizi mbaya ya huduma ya daraja dhidi yetu. Nakumbuka alikuwa ni huyu huyu Mbalawa.

Hoja kuhusu daraja la Kigamboni iko wazi sana, kwanini wanaKigamboni tulipie huduma ya daraja ilhali limejengwa na serikali yenye wajibu wa kutoa huduma kwa watu wake ambao ni walipa kodi. Kwani nini mwananchi anawajibika kuifanya kwa serikali zaidi ya kutimiza wajibu wake wa kulipa Kodi tu kama wana Kigamboni tunavyo fanya.

Badala ya kufaidi matunda ya kodi zetu eti leo serikali inatukopesha huduma ambayo tunalazimika kulipia kwa muda usiojulikana.

Utaratibu huu umeitenga Kigamboni na maeneo mengine ya jiji kwa kuwa inatafsiri kwamba lazima ulipie visa wakati wa kuingia na kutoka Kigamboni, jambo ambalo haifanyiki kwa sehemu nyingine zinazotumia huduma za madaraja.

Kwa ufupi huduma ya usafiri imekuwa kero kubwa sana kwetu kwa kuwa hata daladala nazo zinatoa huduma zao kwa viwango duni kwa kuwa nao inawalazimu kulipia fedha kubwa kila wanapotumia daraja la Kigamboni.

Sababu hiyo pia imekuwa chachu ya kukoleza makali ya maisha kwa wanaKigamboni kwa kuwa vyakula vinapokuja Kigamboni kupitia daraja au Pantoni wafanyabiashara nao hulazimika kulipia Ada ya huduma na wao wa nakuja kufidia hiyo kwa kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu.

Ni hali inayokatisha tamaa sana kwa kutokumuona Mbunge wako hana muda wa kuyazungumza matatizo yetu mbele ya chombo chenye maamuzi, basi walau nilitarajia alipokuwa Waziri angetumia fursa hiyo, lakini waaaapiiii , bado Kigamboni ni ileile tu.

Leo daraja la Tanzanite nimezinduliwa na huduma zake ni bure, watumiaji wa daraja hilo wengi wao ni wananchi wenye uwezo kiuchumi na viongozi kama yeye waishio ukanda huo wa makazi ya viongozi.

Hili la daraja la Tanzanite na Kigamboni si sawa hata kidogo, kisheria, Kikatiba, kijamii na hata kiutu, sijui Mbunge wetu na serikali yake wanatuangalia kwa upeo upi, yaani wanatuonaje sisi

2. Michezo

ENEO jingine nyeti ambalo Mbunge wangu Kigamboni analipuuza ni hili, nilitarajia kama kiongozi angezingatia mchango wa sekta ya michezo kijamii na kiuchumi.

Kigamboni kimichezo ni zaidi ya Dolooo licha ya vipaji lukuki tulivyonavyo, jamaa hana jitihada yoyote kuipigania michezo,hata ukijitolea kumuanzishia halafu walau umialike aja kama mgeni rasmi tu, simu yako haitopokelewa tena.

Hata mara kadhaa tumejaribu kumshawishi kudhamini ligi ya Mpira kwa gharama ndogo kabisa ambayo tena ingetumia Jina lake kama wanavyofanya wanasiasa wengine, jamaa hana huo muda. Mtaongea vizuri

Kuna wakati alitangaza kuanzisha timu ya netiboli sijui iliishia wapi
Kwa masikio yangu na macho nimeshuhudia wanamichezo mbalimbali mfano Tenis na basketball wakiomba sapoti yake jamaa hana time!

Yeye husubiri ile michezo ya matukio ya kisiasa (bonanza) mfano Jogging ambayo kimsingi tusidanganyane haina tija yoyote kwa vijana wenye vipaji vyao, lakini Nina uhakika siku mwammichezo yeyote kutoka Kigamboni akifanya vizuri yeye atakuwa wa kwanza kujitokeza kujivunia
Jamaa hataki Michezo.

VIJANA:
Bila kumung'unya maneno, binafsi Sina kumbukumbu ya Mheshimiwa huyu kuwaita vijana au kusimamia kuwaweka pamoja na kuwapa walau semina ndogo Dogo za namna ya kupambana na maisha.

Kundi kubwa sana la vijana(wasichana na wavulana) lipo mtaani halina elimu wala mtaji wa maisha, hawa wanahitaji kuweka pamoja na kupewa mafunzo maalum kuwajenga uwezo na maarifa ya kimaisha, nani wa kuyafanya haya kama si kiongozi wao ambaye siku ya kampeni anawahitaji sana kumnadi?

Aaaaaaaaah, bwanaeee, yapo mengi ya kuyasema hapa, kwa Leo yatoshe hayo, jamaa anatuzingua

LA Elimu naliacha kiporo!

Lakini najua kwanini anatuburuza, kwa sababu vyama vya Upinzani hawajawekeza kabisa kulichukua jimbo la Kigamboni, jamaa nao hawajajipanga kila mwaka wa uchaguzi huoni mipango yoyote ya uhakika kushinda uchaguzi, Siasa za Tanzania taabu sana!

FB_IMG_1643782129117.jpg
 
View attachment 2104949
Hama huko
 
Back
Top Bottom