PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 879
- 956
Wakuu hi tozo ikiondolewa wakazi wa Kigamboni itawapunguzia Sana Ukali wa Maisha.
Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) ameitaka Serikali kuondoa tozo za Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni na badala yake Serikali ibebe mzigo wa deni la mkopo wa NSSF.
Ndugulile ameyasema haya leo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa anachangia taarifa ya Kamati ya Bajeti.
Ndugulile alieleza kwamba ni wakazi wa Kigamboni pekee nchini kote ambao wanalipia gharama ya daraja wakati kuna madaraja mengi yamejengwa kwa fedha za mikopo.
Dkt. Ndugulile alisema kuwa wakazi wa Kigamboni hawana njia mbadala ya kutumia kama ambavyo wakazi wa Msasani, Masaki na wengine wanaotumia Daraja la Tanzanite, hivyo kuwatoza fedha ni kutowatendea haki wakazi wa Kigamboni.
Wakazi wa Kigamboni wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu tozo za Daraja la Nyerere, hali inayopelekea kuongeza kwa gharama za maisha.