Uchaguzi 2020 Ndugu Zitto wakati unagombea mwaka 2015, uliahidi kutoa mikopo kwa vijana hususani waendesha pikipiki

NTWA MWIKEMO

JF-Expert Member
Oct 7, 2014
734
365
Leo nataka kuteta kidogo na Ndugu Zitto Kabwe,Kijana uliejizolea umaarufu mitandaoni na kuyasahau matatizo ya wananchi wanyonge katika jimbo lako la Kigoma Mjini.

Hakika umekuwa machachari kwa kujenga hoja,kukosoa Serikali ,kuponda na hata kutukana na kubeza kila kitu kinachofanywa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri Rais Dkt.John Magufuli.

Binafsi sikushangai maana huenda ndivyo ulivotafsiri upande wa chama chako yaani Chama cha upinzani Upinzani.Ni huko ACT Wazalendo ulikuwepo.

Ndiyo hatukatai wala kubisha wewe ni mpinzani ambaye kila siku jicho lako limekuwa likimulika kibanzi kwa wenzio nakusahau kama unalojukumu la kusiman na wananchi wako katika jimbo la Kigoma Mjini.

Nakumbuka mwaka 2015 wakati unagombea ubunge kapitia chama chako hicho ulituahidi mengi ,lakini mpaka naandika ujumbe huu ,hukufanya chochote zaidi ya porojo za mitandaoni na ubishi usokuwa na faida.

Tujikubushe Kidogo.
Ndugu Zitto nakumbuka ulituahidi kujenga hospitali kubwa ya kanda katika jimbo letu lakini mpaka sasa ahadi hiyo imesalia kuwa adidhi na sintofahamu ni kwamba umeshindwa kujenga hata zahanati moja.

Ulituahidi kwamba baada ya kupata ridhaa utahakikisha kila mkazi wa Kigoma mjini anapata bima ya afya ,naona ahadi hiyo umeishia kuitekeleza katika familia yako.

Ndugu Zitto ulituahidi kujenga uwanja mkubwa Mpira katika eneo la COMMUNITY CENTRE hadi leo hakuna hata dalili za mradi huo kufanyika.Pia ulituahidi kujenga barabara za mawe kama ile ya Ujiji mpaka sasa hakuna kilichofanyika.

Ndugu zitto wakati unagombea mwaka 2015, uliahidi kutoa mikopo kwa vijana hususani waendesh pikipiki desha( Bodaboda).

Uliahidi kuanzisha shule maalumu ya michezo(sports academy ili kuvisaidia hikundi vya sanaa mpaka sasa hakuna kilichofanyika .

Aidha uliwaahidi Wavuvi,akina mama washona Shuka,Wakulima wa Bustani,waendesha bodaboda na daladala kwamba utawaunganisha kwenye mfumo wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili wapate mikopo nafuu na Bima ya afya lakini ahadi hizi zote zimekuwa hewa na hakuna lolote lililofanyika kuhusu ya vijana.

Sasa unarudi tena kudanganya kwa mara nyingine ,nadhani kabla hujatoa ahadi mpya utupe majibu ya ahadi hizo ,umezitekeleza wapi?

Kama zipo huko kwenye mitandao ya kijamii basi twambie tujue maana huenda wapiga kura wako wapo huko mitandaoni .

Nalokusihi ni kwamba HATUDANGANYIKI TENA.

Imeandikwa na Mpiga kura Jimbo la Kigoma Mjini.
 
SABABU 27 ZA KUMKATAA MAGUFURI 2020.


1. Hajatoa ajira miaka 5
2. Hajaongeza mishahara kwa miaka 5
3. Ameongeza makato HESLB toka 8% to 15%
4. Amefukuza wafanyakazi na hajawapa hata senti tano kisa vyeti feki
5. Kaondoa fao la kujitoa NSSF
6. Kaondoa wanunuzi binafsi wa kahawa waliokuwa wanatoa bei nzuri
7. Karudisha gharama za matibabu kwa watoto na wajawazito
8 .Anatoza maiti kodi kuzitoa mochwari
9. Kavunja katiba ya nchi kuzuia wapinzani kufanya mikutano halali ya siasa
10. Katunga sheria kandamizi kukomoa watu
11. Kabambikia kesi watu kwa visasi na chuki
12. Kafilisi wafanyabiashara kwa chuki binafsi
13. Kathibiti mashirika ya kutetea haki za binadamu
14. Kadhibiti na kutisha vyombo vya habari na kuviamrisha vimtangaze yeye tu na chama chake
15. Kavuruga sana mahusiano ya kimataifa
16. Kavuruga demokrasia na anataka wananchi waishi kama mifugo yake kufuata analotaka
17. Kazima bunge live na kulitumia bunge kama muhuri kufanya mambo yake
18. Mahakama imebinywa na imekuwa siyo huru tena
19. Kawadhibiti viongozi wa dini wanaomkosoa na kumwambia ukweli
20. Kanunua ndege bila kufuata sheria ya PPRA
21. Watu wengi wameuwawa na kupotea na kutekwa
22.Amelea na kulinda kikosi kazi cha "watu wasiojulikana"
23. Amepandikiza hofu,ukatili na dhuluma kama nyenzoza siasa mpya za Tanzania na utu umetoweka
24. Kakivuruga chama chake na kukimega vipande vipande
25. Kajenga uwanja wa ndege kwao bila ya approval ya bunge wala cabinet
26. Alisema tutaishi kama MASHETANI.. kwa madai kuwa tulikuwa tunaishi kama Malaika. Hakika amelitimiza hilo.🤔
27. Kuwa na kundi la watu wasiojulikana awamu hii ya tano na polisi hawajawai
 
Unafiki wa wana ccm kukataa katiba ya Warioba,sasa tunajuta kimyakimya pamoja.
 
Back
Top Bottom