Ndugu zangu wana MMU na msio wana MMU

Ndugu zangu wana MMU na msio wana MMU

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
4,922
Reaction score
3,244
Naitaji maombi yenu dhidi ya huyu shetani. Nimeokoka jana nikapokelewa kwa fujo na nderemo toka katika familia yangu pamoja na majirani. Saa saba usiku nimerudi tilalila vibaya sana. Kisa kilikuwa hivi, jamaa yangu moja nilikuwa namdai laki sita. Ilipofika muda wa jioni akanipigia simu. Njoo uchukuwe pesa yako nipo sehemu fulani akanielekeza. Nikasema kweli Yesu atukuzwe, mdaiwa sugu kaniita akanilipe!!!

Nikachukuwa bodoboda huyo mpaka sehemu husika. Huwa bodaboda nikipanda lazima iwe na kiti cha kuegemea sababu nikimkumbuka Kayumba huwa nakithamini sana kichogo changu. Punde nikafika kiwanja, eee bwana ehee nikamkuta jamaa kazungukwa na wadada viwango wanakata maji. Akaniagizia nikamwambia ushidwe nimeokaka. Akaniambia kama aunywi ----- wewe nakulipa laki tatu tu na matusi kibao. Nikasema kimoyomoyo ngoja nizifakamie, kwanza sijasimama kiimani.

Nikaanza kupiga bia mara valuu baada ya kuchangamka tu nikadai pesa zangu. Tukaenda chobingo jamaa akanihesabia changu na kwa bahati nzuri alikuwa pombe sana, alinipa laki sita sabini badala ya laki sita kamili. Mishale ya saa sita na nusu nikachukuwa cab mpaka nyumbani nikagonga geti kipombe pombe nikafunguliwa then nikaingia sebuleni hapo ndipo nilipo zima mazima. Saa tatu asubuhi kustuka nimezungukwa na wale walionipongeza pamoja na yule aliye niongoza sala ya toba.
 
hongera sana kwa kufanikiwa kushindwa kuilinda imani yako
 
pombe za kununuliwa mbaya sana na ungezima kitaani watu wangekula 0712 bwaaaaaaaah!
 
ha ha ha haaaaa pole sana mkuu. Tubu na endelea kumwomba Mungu akuondolee pepo la ulevi.
 
Je laki sita na sabin zlipona? Hahahah pesa ndo habare ya town..
 
Mkuu......hapo ulipoamua kumuaibisha Mungu wako na kutuonyesha kuwa shetani ni m'babe ndipo uliponimix.........bora tu ungeanzia hapo kwa mdaiwa wako story ingeeleweka na kunoga zaidi........
 
Nikachukuwa bodoboda huyo mpaka sehemu husika. Huwa bodaboda nikipanda lazima iwe na kiti cha kuegemea
Boss unaemiliki kampuni na vigari vidogo vidogo kadhaa.

Hapo ile verrosa na harrier yako zilikuwa zimekata kiwese nini???



Kwa msaada Tyta naomba picha ya Harrier na Verrosa bila kusahau vigari vidogo vidogo kadhaa.
 
Last edited by a moderator:
ungewauliza, where am I?

whats wrong with me?

tell them to call the police! --- we jifanye chizi tu!
 
[/QUOTE=Boss unaemiliki kampuni
hapo sasa! [/QUOTE=na vigari vidogo vidogo kadhaa[/QUOTE].

Hapo ile verrosa na harrier yako zilikuwa simekata kiwese nini???[/QUOTE]
 
Its funny, vp 2kuelewe vipi sasa we mpendwa au bado una undugu na Kinana...
 
sasa mkuu tunakusaidiaje hapo? pesa zipo salama au? kama uliokoka imekuaje ukajiingiza majaribuni kiasi hicho? kama alikuambia atakupa laki 3 kama hautokunywa kwa nini haukuchukua laki 3 hiyo hiyo na kuondoka? hayo yote yasingetokea, tubu na usirudie kosa.
 
Pesa ipo mkuu hesabu tna icijekuwa ulihesabu vibaya
 
Back
Top Bottom