Ndugu wasio na shukrani!

Ndugu wasio na shukrani!

Wapumbavu kama hao wapo wengi sana kwenye jamii zetu.

Halafu ni hao hao ukipata adha au matatizo flan ni wa kwanza kukutangaza.

Yaani kamwe hawawezi kutangaza mema uliyomfanyia kama vile kumsaidia ila ngoja upatwe na baya.

Hawatoacha kusema asilani.
 
Leo umenigusa haswa maana duh "Ndugu lawama" yaani ukiwa nacho kila mtu anataka na akishapata huyo anasepa na ukimwambia huna habari yake utaipata mjini hapa full matangazo
 
umesahau na marafiki unamkopesha pesa yaan Italia machozi simu hapokei sasa unaapa kwa mungu siwezi kusaidia mwingine, mwezi tu huyo mwingine ataliaaaa weeee mwishowe Natoa yaan kama vile nilirogwa sijawahi kumpa ndugu au rafiki pesa akanirudishia.

jitu nililikopea laki 8 kwenye chama hadi Leo na liba nalipa mm dunian kuna majaribu.
 
Ndugu wenye uwezo pia mkishasomesha mtu au ukamsaidia kupata kazi inakuwa kama ulikuwa unawekeza kwake hivi.. Utaskia
"Amekaa hapa kwetu miaka yote siku hizi hata 100 hatutumii"
Wakati mtu mwenyewe still ana matatizo kibao, asapport wadogo zake,wazazi wake, kamshahara kenyewe ka kawaida tu.. Bleeh!!
 
Mkuu Nyani Ngabu
1. You will never be able to meet everybody's need
2. Before pledging an assistance, ask yourself how much can you afford to give and how much is going to affect your budget.
3. Once you are giving help to someone, let it be a thanks giving to God the Almighty, even your right hand is not supposed to be aware of what the left did.
4. When you are a giver, God knows who will be allocated to meet your necessities when you are in need.
 
Tabia ya kuomba wakati unashida ni urithi wa Dunia...
 
...hatuwatafuti mara kwa mara coz kila mkiona calls zetu mnadhani tunataka kusaidiwa, kumbe masikini ya Mungu tunataka kuwajulia hali tu.

Ukiwa na ndugu wenye uwezo ni bora mkutane kwenye "shughuli" tu, wengi nyodo zimezidi, kila akitoa senti kumi anatangaza kwa marafiki na ndugu wenye uwezo kuwa kakusaidia....

I'd rather be masikini jeuri.
Ndugu wa hivi hata mguu kwake sitii, coz kuna ndugu yetu anazo kidogo, ukifika kwake kabla hujaondoka keshatangaza kuwa flani kaja kwangu nimempikia hiki na kile, na shida iliyomleta ni ile. Basi wengi tumekata mguu kufika kwake, amebaki kulalamika hatutaki kufika kwake.
 
Wapumbavu kama hao wapo wengi sana kwenye jamii zetu.

Halafu ni hao hao ukipata adha au matatizo flan ni wa kwanza kukutangaza.

Yaani kamwe hawawezi kutangaza mema uliyomfanyia kama vile kumsaidia ila ngoja upatwe na baya.

Hawatoacha kusema asilani.

Watu wa hivyo huwa ni mahodari sana wa kueneza habari zako zinazoonekana kuwa ni hasi.

Hovyo kabisa yaani.
 
Haya mambo yapo kwa extended families za kiafrika. Trna hapo itokee mambo yakuendee kombo utaiskia yule.alikuwa mfujaji wa pesa, anagawa gawa pesa. Wkati naye ni mnufaika mmojawapo. Mi nafikiri saidia penye ulazima.
 
umesahau na marafiki unamkopesha pesa yaan Italia machozi simu hapokei sasa unaapa kwa mungu siwezi kusaidia mwingine, mwezi tu huyo mwingine ataliaaaa weeee mwishowe Natoa yaan kama vile nilirogwa sijawahi kumpa ndugu au rafiki pesa akanirudishia.

jitu nililikopea laki 8 kwenye chama hadi Leo na liba nalipa mm dunian kuna majaribu.

Kumbuka usemi kwamba ukimkopesha ndugu uwe tayari na mawazo ya uwezekano wa kulifuta deni. Haya yanatokea mara nyingi. Wakishakujua ni mgumu basi utasikia yule ana roho mbaya.
 
Mi ndugu zangu ni kulalamika tu eti siwapigii simu,wakati wao wenyewe wana simu na hawanipigii.

Aisee hiyo nayo huwa inanichefua sana.

Eti wao huona wajibu wa kupiga simu ni wako tu.

Wao tu ndiyo watafutwe lakini wao kukutafuta utadhani mwiko!

Huo udumavu wa akili.
 
Ndugu wengi sana mimi nimewapotezea....

Nna ndugu yangu mmoja huyo sasa hivi kutwa ananiomba hela
nikimtafutia kazi anaanza kusema subiri kwanza sijui nini
ila hela kuomba haachi

ndugu mzigo
 
Ndugu wengi sana mimi nimewapotezea....

Nna ndugu yangu mmoja huyo sasa hivi kutwa ananiomba hela
nikimtafutia kazi anaanza kusema subiri kwanza sijui nini
ila hela kuomba haachi

ndugu mzigo

Halafu wengine wapo ambao hawana kazi.

Ukimwambia sehemu flani kuna kazi ya udereva wa ofisi ya mkurugenzi flani, mwenzio hataki eti hawezi kuwa dereva.

Hiyo kazi siyo saizi yake. Haina hadhi.

Huku kwa wakati huo huo hela hana na haachi kukupiga mizinga.

Mwanaume hachagui kazi, chambilecho Le Mutuz!
 
na mizinga ya hela ndefu sometimes....mimi wananiacha hoi kwa kweli
mtu anataka umpe almost income yako yote ya mwezi
huku kwenda kufanya kazi hataki
 
Huwezi kumfurahisha kila mmoja, kuna mwezi nilikaa nikawa narekodi kila aliyenipigia simu kuomba hela bila kujali kama nimempa au la, mwisho wa mwezi nikajumlisha zote nikaona ilikuwa ni zaidi ya kipato changu. Hapo ndo nilipothibitisha kuwa siwezi kusaidia kila tatizo linalokuja mbele yangu, mwanzoni nilikuwa napata tabu sana navoona nashindwa kusaidia shida ya ukweli mpaka nakopa ili nimpe mtu mwingine ambao wengi huwa hawalipi au watachelewa sana kulipa
 
Ndugu wa hivi hata mguu kwake sitii, coz kuna ndugu yetu anazo kidogo, ukifika kwake kabla hujaondoka keshatangaza kuwa flani kaja kwangu nimempikia hiki na kile, na shida iliyomleta ni ile. Basi wengi tumekata mguu kufika kwake, amebaki kulalamika hatutaki kufika kwake.
Ndugu wa hivi siwezi kabisa, miaka hii ni bora kuishi kivyako tu coz wenye uwezo wanalalamika, wasio na uwezo wanalalamika. Ya nini kumtembelea mtu ambaye atakutangaza kuwa ulienda kula ubwabwa kwake?
 
Leo umenigusa haswa maana duh "Ndugu lawama" yaani ukiwa nacho kila mtu anataka na akishapata huyo anasepa na ukimwambia huna habari yake utaipata mjini hapa full matangazo
Kama wewe ulivyosepa kuleeeee au vipi?
 
Ndugu wa hivi siwezi kabisa, miaka hii ni bora kuishi kivyako tu coz wenye uwezo wanalalamika, wasio na uwezo wanalalamika. Ya nini kumtembelea mtu ambaye atakutangaza kuwa ulienda kula ubwabwa kwake?

Naam, kuishi kivyako ndo kwenyewe.

Laiti watu wengi wangekuwa na falsafa kama yangu ya 'live and let live', basi mitafaruku ingekuwa michache sana hapa duniani.

Bahati mbaya uhalisia wa maisha hauko hivyo!
 
Back
Top Bottom