Ndugu ni ndugu na ndiyo undugu wenyewe huo mmoja akitoka, basi inaaminika kwamba umefungua njia.
Mimi ndugu zangu hua wanastukia tu kuniona nipo around na ntakuwa na ratiba zangu.
Huwa nawaambia kwamba msaada mkubwa kutoka kwangu ni kukusaidia ada ya kozi (ku-top up) unayosoma yenye kuja kukusaidia maishani au kunisaidia shughuli zangu za shamba au kukusaidia mawazo ya ujasirimali.
Halafu wanafahamu siwezi kukusaidia tu bila kuja na business plan, kama kuwa na Barber shop, hair dressing saloon, grosery shop na aina yoyote ile ya biashara.
Lakini mimi sio benki kwani wengine wanaomba hata mitaji kabisa kama 10,000,000 hivi.
Sasa hii si anaweza kuipata akienda benki na business plan yake?
Ila siwasahau ndugu zangu kwa vitu vidogovodogo ambavyo ukiwapa anaweza kuwa nacho wakati wote kama kofia, top original ya Arsenal na handset ya kawaida.
Akiwa nacho anakuwa akikukumbuka kwamba ndugu upo.
Halafu mkuu NN, jaribu kuwaunganisha ndugu zako kwenye WhatsApp Group ndiyo utaona hizo feeds za maombi na utaweza kuchuja zipi za kuzingatia.
WhatsApp inaleta togetherness baina ya ndugu na mnakuwa mkiwasiliana kila mara.
Hizo feeds zingine unapotezea tu.