Binadamu hanaga shukrani hivyo kama unampenda we mpende tu

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Feb 9, 2019
859
1,012
Binadamu siku zote hanaga shukran hivyo kama unampenda wee mpende tu tena mpe kila kitu ila hatutaki kelele baadae.

Wengi wamelizwa kwa kusubiri kutegemea SHUKRANI kutoka kwa wapenzi wao kutoka kwa WATOTO wao kutoka kwa MARAFIKI zao.

Hivyo basi kama unampenda wee mpende tu tena mpe kila anachokitaka kwako

Mpe GARI, NYUMBA, MPE MAPENZI YOTE, MPE FIGO, MPE JICHO👁️👌 MPE HATA NA MOYO WAKO.
Kama ni mtoto muonyeshe mapenzi mazuri yote, msomeshe katika shule zenye hadhi ya juu, mtibie kwenye hospitali za gharama kubwa.

Ila kama mategemeo yako ni SHUKRANI kutoka kwake basi hesabu tu UMEUMIA.

JAPO WENGINE HUWA WANAKUMBUKA WALIPO TOKA.

Ila ni binadamu wachache sana wenye kuwakumbuka walio wasaidia kipindi wana shida.
Ndio maana huwa kuna mambo mengi sana unapohitaji kukopa pesa benki kwani huwa wanaamini ni ngumu kukumbuka shida baada ya shida kukuisha.

Huyo ndiye binaadam hivyo kama unamsaidia au unanisaidia basi nisaidie kama sehemu TAKWA la DINI yako au la moyo wako.
Usikae kusubiri fadhila kutoka kwangu.
 
Back
Top Bottom