Ndugu wa Polepole ateta na Askofu!

Mmh
 
Free kila balozi Mzalendo
 
ok.🐒
 
Utawala wa awamu hii umevunja rekodi kwenye matukio ya kuteka, kupoteza, kuua, kufunga, kubambikia wakosoaji wake kesi za uhaini na ugaidi, na kupuuza malalamiko/mashinikizo ya ndani na nje ya nchi kuhusu kuirejesha nchi kwenye misingi yake ya kawaida.
 
Acheni masihara zile damu pale chini ni nyingi , ni aidha Polepole alifia palepale au alifia njiani wakiwa wanaondoka nae.

Kwa mambo aliyokua anaongea Polepole mission yao ilikua moja kumnyamazisha daima ,huyo mtu alikua na siri zao nyingi sana waliona muda unavyozidi kwenda angewasumbua sana .

Si mmeona Sativa alivyopona mikononi mwao alivyowaanika dunia nzima hadi Mafwele kafungiwa kuingia USA , sasa Polepole aliyekua na siri hata ya safari iliyosemekana ilileta shida kwa afya ya jiwe ndio wamuache?

Polepole aliyesema mfumo wa vitambulisho vya taifa umeungwa na portal za CCM na alikua tayari kutoa maelezo ya kina ndio waje wamuache hai walipomkamata?

Familia ifike mahali ikubali ukweli kuwa tarehe 6 October ndio aliuwawwa sasa wao wachague wataenda njia gani kusaka haki ya ndugu yao kudhulumiwa uhai wake.
 
Umeweza kufanya haya yote kwa sababu wananchi hatujitambui. Nakumbuka zamani shuleni wakati ukisoma historia ya utumwa tulikuwa tunaambiana eti mababu zetu walikuwa wajinga kupitiliza kukubali mwarabu mmoja kuwaswaga kama ng'ombe na wao hawajibu mapigo. Siku hizi nimegundua kuwa kizazi cha sasa ni cha mijitu mijinga kuliko enzi hizo. Watu wazima zaidi ya milioni 40 wanaswagwa na kundi la CCM ambalo hawazidi hata 1000. Akilizetu badoziko kwenye level ya u-kima au u-nyani.
 
hiyo familia imechanganyikiwa, kaka mtu alisema HP ana cheap mwilini
Hapo ndio nilipothibitisha maumivu ya kupotelewa ndugu yamewavuruga. Kwa uelewa wangu, hauwezi kumuwekea mtu active chip ya kuweza kujua alipo, kwa sababu hicho kifaa kitahitaji battery, antena na mambo mengine ili kiwe kinatuma taarifa kwenye kifaa kingine.

Kama ana chip, itakua ni le inayoweza kusomeka kwa masafa mafupi akipita kwenye eneo la karibu endapo kuna kitu cha kuweza kuitambua hiyo chip. Hii sio kitaalam ila ki layman.

Kwa muktadha huo, kiuhalisia, hana chip ya kuweza kujua mahali alipo. Huenda yalikua ni matamko ya kuwafanya wanaomshikilia watafakari na kuona kama wanaweza kubadili maamuzi kwa vitisho.

Kuna siku nilikua nasafiri, ile naingia kwenye ndege tu, ana kwa ana na yule jamaa mrefu wa kanda maalum, na ni mrefu kweli kweli, nilipata mtihani sana kuzuia kinywa na mikono yangu isitamke chochote au kurusha kelebu nikiwa napita kuelekea kwenye kiti changu. Ila kimoyo moyo nilifanya matendo yakutosha yanayostahili jinai.

Tulipofika mwisho wa safari, pale airport, akaja kuchukuliwa na VIP, hakutembea kuelekea kule wanatokea abiria wanaowasili, wakati huo nje msafara unamsubiria.
 
Kchanganyikiwa ni lazima labda kama wasingekuwa binadamu. Hata kuku huchanganykiwa anapomtoza kifaranga wake. Nadhani alisema hivyo ili kujaribu kuwatisha waliomteka.
sawa sawa ,ila inawezekana kweli akawa hi mpk leo ? wanakaa nae siku zote hizo ili iweje ? au inakua ni somo kwa wengine na vijana wanajiunga na hivyo vikosi sijui vikundi vya utekaji ?
 
Kweli inakanganya ila siamini kama kweli Yuko hai mpaka Sasa maana kama Yuko ukonga utawala mwingine ukija si utamtoa? Halafu itakuwa Soo kubwa zaidi?
Nakubaliana na wewe. Hata mimi sidhani kama yuko hai. Asilimia 99 aliuawa na asilimia 1 ndiyo naamini yuko hai. Lle gazeti la African confidential huwa naliiamini na lisingeweza kuandikajambo kubwa kama hili bila kuwa na source ya uhakika.
 
Nakubaliana na wewe. Hata mimi sidhani kama yuko hai. Asilimia 99 aliuawa na asilimia 1 ndiyo naamini yuko hai. Lle gazeti la African confidential huwa naliiamini na lisingeweza kuandikajambo kubwa kama hili bila kuwa na source ya uhakika.
Ilivyo ngumu kumlinda mateka! | JamiiForums Tanzania https://share.google/HennPeO8WV4k9ubyZ
 
hahahahaha ulimalizana nae kimyo moyo, ila tuache yote familia ya pole pole haiko sawa mpk sasa,bora hata wangepewa mwili kama kauwawa
 
Nikupe pole kwa kikaribiana na huyo shetani. Wewe uko kama mimi. Huwa nawaza nikikutana naye nje ya nchi, mtaani naweza kujikuta nafanya jambo moja baya sana. Ila kwa haya mauaji walifanya huwa nasema nitashangaa sana kama maisha yataendelea kama kawaida. Naamini kabisa, hakuna utawala ulioua raia wengi kiasi hicho na ukabaki salama. Halafu hawa wajinga wameshalewa damu sasa hivi, kila wanachofanya ni kama wanazidi kuharibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…