Ndugu Polepole, nitajie kituo Cha mabasi cha Wilaya au mkoa chenye Hoteli yenye hadhi Kama hoteli binafsi zinazohusu abiria wa safari ndefu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kuna hoja ameiwasilisha Polepole kwenye television (chanel 10) kipindi cha papo kwa papo nakuungwa mkono na Mhe Waziri kwamba mabasi badala ya kwenda kwenye hoteli zenye hadhi na chakula salama wawapo safarini Basi mabasi hayo yasimame kwa muda mrefu stand watu wale chakula nakupata huduma nyingine.

Haya maamuzi ni maamuzi yanayosukumwa na watendaji ambao wanatumia mashangingi ya serikali na chama na ambao hawapandi bus kwenda popote. Leo hii vituo vya mabasi vinafahamika, havikujengwa kwa lengo lakutoa huduma ya chakula kwa abiria bali vimejengwa kama points zakusubirua abiria wapande na kushuka. Vituo hivi vina matundu machache sana yakujisaidia na huduma hii inagharamiwa huku kukiwa hakuna usafi Wala maji yakutosha.

Standard yavituo vyetu haikidhi viwango vyakuhudumia abiria labda tuingie kwenye uwekezaji mpya wa kuvikarabati

Turudi kwenye gharama ya chakula, gharama ya chakula inategemea na eneo unapopata huduma. Inashangaza Leo hii uniambia gharama ya Serena hoteli ilingane na gharama ya mama ntilie kisa wananchi wamelalamika.

Kama tutataka kuweka usawa tufike pointi tujadiliane na watoa huduma, wale wamiomiliki wanaopenda wakae stand muda mrefu wajitangaze ili abiria wajue bus ili linasimama stand kwa ajili ya chakula na bus ili linasimama hotel binafsi kwa ajili ya chakula....abiria wachague watapanda gari gani lakini si kulazimisha watu wote waishi, wasafiri na kula kwa maelekezo ya Waziri.

Polepole umechemka acha siasa kwenye huduma, pokea kero wakabidhi vijana wa chama wazifanyie utafiti the waishauri serikali njia inayofaa siyo kumlazimisha Waziri atoe msimamo wa kisera kwenye media.....w
 
Dah! Ila binadamu bwana tuna mambo!

Malalamiko si yamekuwa yakitolewa humu humu 'repeatedly' kwamba hoteli ambazo mabasi husimama chakula ni ghali sana, hakuna value for money na hakuna options? Kwa hiyo mabasi yatakiwe kuimama sehemu zinazowafaa wananchi wote.

Sasa malalamiko yamefanyiwa kazi, kabla hata utekelezaji haujaanza, waja tunalalamika tena? Eti kwa nini mapendekezo ya walalamikaji yamefanyiwa kazi. Duh!

Kwa hili polepole yuko sahihi sana na amekuwa very efficient. Kama kuna wa kulaumiwa kwenye hilo, basi ni waliolalamika ambao sasa wamepewa wanachotaka kisha wanalalamika tena.

Ni vyema tukawa tunajiridhisha kuwa tunataka nini au hatutaki nini kabla ya kuomba, vinginevyo kama kila ambacho mtu hupewa (hata kama kaomba) analalamika, mwishowe mfanya maamuzi huchanganyikiwa na kuamua chochote ili iwe vyovyote na chanzo cha tatizo la namna hiyo ni 'consumers'.

Mwisho wa siku kulalamika wakati mwingine nayo ni tabia, kuna mtu vyovyote itakavyokuwa tu, atalalamika na kulaumu, yaani ni sehemu ya maisha yake.
 
.... Leo hii vituo vya mabasi vinafahamika, havikujengwa kwa lengo lakutoa huduma ya chakula kwa abiria bali vimejengwa kama points zakusubirua abiria wapande na kushuka. Vituo hivi vina matundu machache sana yakujisaidia na huduma hii inagharamiwa huku kukiwa hakuna usafi Wala maji yakutosha. Standard yavituo vyetu haikidhi viwango vyakuhudumia abiria labda tuingie kwenye uwekezaji mpya wa kuvikarabati
...
... additionally, ni points za kukusanya ushuru! Nothing less, nothing more. Imagine basi linalazimika kuingia stendi ya halmashauri hata kama limejaa na halina abiria anayeshuka hapo.
 
Dah! Ila binadamu bwana tuna mambo!

Malalamiko si yamekuwa yakitolewa humu humu 'repeatedly'kwamba hoteli ambazo mabasi husimama chakula ni ghali sana, hakuna value for money na hakuna options? Kwa hiyo mabasi yatakiwe kuimama sehemu zinazowafaa wananchi wote. Sasa malalamiko yamefanyiwa kazi, kabla hata utekelezaji haujaanza, waja tunalalamika tena? kwa nini mapendekezo ya walalmikaji yamefanyiwa kazi. Duh!

Kwa hili polepole yuko sahihi sana na amekuwa very efficient. Kama kuna wa kulaumiwa kwenye hilo ni walilalamika sasa wamepewa wanachotaka wanalalamika tena.

Ni vyema tukawa tunajirridhisha kwa na tunataka nini au hatutaki nini kabla ya kuomba, vinginevyo kama kila ambacho mtu hupewa (hata kama kaomba) analalamika, mwishowe mfanya maamuzi huchanganyikiwa na kuamua chochote ili iwe vyovyote na chanzo cha tatizo la namna hiyo ni 'consumers'.
Labda ni mmiliki wa hotel mojawapo
 
...
Kama tutataka kuweka usawa tufike pointi tujadiliane na watoa huduma, wale wamioiki wanaopenda wakae stand muda mrefu wajitangaze ili abiria wajue bus ili linasimama stand kwa ajili ya chakula na bus ili linasimama hotel binafsi kwa ajili ya chakula....abiria wachague watapanda gari gani lakini si kulazimisha watu wote waishi, wasafiri na kula kwa maelekezo ya Waziri.
...
... LATRA iweke classification kwenye haya mabasi; yatambulike from the beginning kabla msafiri hajakata tiketi kwamba hili ni la kusimama stendi muda mrefu na hili ni la private hotels kama ilivyo Daraja la 1, la 2 na la 3. Unajua kabisa nikipanda basi hili mahala pa kula ni Stendi ya Kibaigwa, hili ni private hotel, n.k.

Pia bus owners walazimishwe kuwa taarifu abiria kabla ya kukata tiketi, jina la hoteli ambalo basi husika linatarajia kusimama kwa ajili ya chakula na sio utashi wa dereva anawapeleka sehemu za ajabu ajabu analizo na maslahi nazo.
 
Kuna hoja ameiwasilisha Polepole kwenye television (chanel 10) kipindi Cha papo kwa papo nakuungwa mkono na Mhe Waziri kwamba vmabasi badala yakwenda kwenye hoteli zenye hadhi na chakula salama wawapo safarini Basi mabasi hayo yasimame kwa muda mrefu stand watu wale chakula nakupata huduma nyingine.

Haya maamuzi ni maamuzi yanayosukumwa na watendaji ambao wanatumia mashangingi ya serikali na chama na ambao hawapandi bus kwenda popote. Leo hii vituo vya mabasi vinafahamika, havikujengwa kwa lengo lakutoa huduma ya chakula kwa abiria bali vimejengwa kama points zakusubirua abiria wapande na kushuka. Vituo hivi vina matundu machache sana yakujisaidia na huduma hii inagharamiwa huku kukiwa hakuna usafi Wala maji yakutosha. Standard yavituo vyetu haikidhi viwango vyakuhudumia abiria labda tuingie kwenye uwekezaji mpya wa kuvikarabati

Turudi kwenye gharama ya chakula, gharama ya chakula inategemea na eneo unapopata huduma. Inashangaza Leo hii uniambia gharama ya Serena hoteli ilingane na gharama ya mama ntilie kisa wananchi wamelalamika.

Kama tutataka kuweka usawa tufike pointi tujadiliane na watoa huduma, wale wamioiki wanaopenda wakae stand muda mrefu wajitangaze ili abiria wajue bus ili linasimama stand kwa ajili ya chakula na bus ili linasimama hotel binafsi kwa ajili ya chakula....abiria wachague watapanda gari gani lakini si kulazimisha watu wote waishi, wasafiri na kula kwa maelekezo ya Waziri.

Polepole umechemka acha siasa kwenye huduma, pokea kero wakabidhi vijana wa chama wazifanyie utafiti the waishauri serikali njia inayofaa siyo kumlazimisha Waziri atoe msimamo wa kisera kwenye media.....w
Alikua anatoa ushauri hau mwongozo? Na huyo waziri alitoa maelekezo hau walikutana kilingeni kupiga story? Inaonekana we ni mdau wa hizi hoteli.
 
Dah! Ila binadamu bwana tuna mambo!

Malalamiko si yamekuwa yakitolewa humu humu 'repeatedly' kwamba hoteli ambazo mabasi husimama chakula ni ghali sana, hakuna value for money na hakuna options? Kwa hiyo mabasi yatakiwe kuimama sehemu zinazowafaa wananchi wote.

Sasa malalamiko yamefanyiwa kazi, kabla hata utekelezaji haujaanza, waja tunalalamika tena? Eti kwa nini mapendekezo ya walalamikaji yamefanyiwa kazi. Duh!

Kwa hili polepole yuko sahihi sana na amekuwa very efficient. Kama kuna wa kulaumiwa kwenye hilo, basi ni waliolalamika ambao sasa wamepewa wanachotaka kisha wanalalamika tena.

Ni vyema tukawa tunajiridhisha kuwa tunataka nini au hatutaki nini kabla ya kuomba, vinginevyo kama kila ambacho mtu hupewa (hata kama kaomba) analalamika, mwishowe mfanya maamuzi huchanganyikiwa na kuamua chochote ili iwe vyovyote na chanzo cha tatizo la namna hiyo ni 'consumers'.

Mwisho wa siku kulalamika wakati mwingine nayo ni tabia, kuna mtu vyovyote itakavyokuwa tu, atalalamika na kulaumu, yaani ni sehemu ya maisha yake.
Hotel nyingi ambazo zilikuwa zinauza chakula njiani nje na vituo vya mabasi zimekufa. Abiria hawana pesa za kula njiani hali ni ngumu sana,hapa tusidanganye watu. Pita njia ya Mwanza Dar au Dar Arusha utajionea mwenyewe. Hata stendi magari yakisimama watu hawali wananunua soda na biscuit tu. Polepole anazingua tu hamna la maana hapo.
 
... LATRA iweke classification kwenye haya mabasi; yatambulike from the beginning kabla msafiri hajakata tiketi kwamba hili ni la kusimama stendi muda mrefu na hili ni la private hotels kama ilivyo Daraja la 1, la 2 na la 3. Unajua kabisa nikipanda basi hili mahala pa kula ni Stendi ya Kibaigwa, hili ni private hotel, n.k.

Pia bus owners walazimishwe kuwa taarifu abiria kabla ya kukata tiketi, jina la hoteli ambalo basi husika linatarajia kusimama kwa ajili ya chakula na sio utashi wa dereva anawapeleka sehemu za ajabu ajabu analizo na maslahi nazo.

Mkuu umeeleza kama mawazo yangu ila nakazia kila kampuni ya Bus ijulikane vituo vyake vya chakula na kujisaidia kabla ya kuanza Safari kwani hii itasaidia wasafiri kufanya uchaguzi na itasaidia TRA kufanya makadirio sahihi, hebu kwanza tujiulize kwanini wenye hotel hizo hutoa chakula bure na posho kwa kila dereva na wasaidizi wake anayepeleka abiria? Nafikiri uamuzi wa polepole ni wa kutetea wanainchi wanyonge wanaonyonywa kila siku na washenzi wachache .

Polepole na Waziri kazeni hapohapo ingawa kisu kimegusa mfupa lakini faida itakuwa ya wengi na Latra wake na amendments zinazohusu jambo hili
 
Mkuu umeeleza kama mawazo yangu ila nakazia oils kampuni ya Bus ijulikane vituo vyake vya choo na kujisaidia kabla ya kuanza Safari kwani hii itasaidia wasafiri kufanya uchaguzi na itasaidia TRA kufanya makadirio sahihi, hebu kwanza tujiulize kwanini wenye hotel hizo hutoa chakula bure na posho kwa kila dereva na wasaidizi wake anayepeleka abiria? Nafikiri uamuzi wa polepole ni wa kutetea wanainchi wanyonge wanaonyonya kila siku na washenzi wachache
Kwa hiyo unataka kudhania kuwa wakiwa wanakaa stendi ili kupata chakula hawatakula bure? Tumia akili bro kabla ya kutetea upuuzi.
 
Hotel nyingi ambazo zilikuwa zinauza chakula njiani nje na vituo vya mabasi zimekufa. Abiria hawana pesa za kula njiani hali ni ngumu sana,hapa tusidanganye watu. Pita njia ya Mwanza Dar au Dar Arusha utajionea mwenyewe. Hata stendi magari yakisimama watu hawali wananunua soda na biscuit tu. Polepole anazingua tu hamna la maana hapo.
Si kweli na ndio Kwanza zinaongezeka Tena na Bei imepanda
 
... additionally, ni points za kukusanya ushuru! Nothing less, nothing more. Imagine basi linalazimika kuingia stendi ya halmashauri hata kama limejaa na halina abiria anayeshuka hapo.
Pamoja na hayo lakini hii ni hatua nzuri kabisa. Wengi tumekuwa tunalalamika hapa mabasi yanatupeleka hoteli ambazo bei zao wanapanga bila kujali kwani wanajua hakuna ushindani na abiria hana sehemu nyingine ya kula. Wakihamia stendi watajitokeza watu wengi wataokajenga au kuimarisha hoteli za stendi kama zamani.
 
Dah! Ila binadamu bwana tuna mambo!

Malalamiko si yamekuwa yakitolewa humu humu 'repeatedly' kwamba hoteli ambazo mabasi husimama chakula ni ghali sana, hakuna value for money na hakuna options? Kwa hiyo mabasi yatakiwe kuimama sehemu zinazowafaa wananchi wote.

Sasa malalamiko yamefanyiwa kazi, kabla hata utekelezaji haujaanza, waja tunalalamika tena? Eti kwa nini mapendekezo ya walalamikaji yamefanyiwa kazi. Duh!

Kwa hili polepole yuko sahihi sana na amekuwa very efficient. Kama kuna wa kulaumiwa kwenye hilo, basi ni waliolalamika ambao sasa wamepewa wanachotaka kisha wanalalamika tena.

Ni vyema tukawa tunajiridhisha kuwa tunataka nini au hatutaki nini kabla ya kuomba, vinginevyo kama kila ambacho mtu hupewa (hata kama kaomba) analalamika, mwishowe mfanya maamuzi huchanganyikiwa na kuamua chochote ili iwe vyovyote na chanzo cha tatizo la namna hiyo ni 'consumers'.

Mwisho wa siku kulalamika wakati mwingine nayo ni tabia, kuna mtu vyovyote itakavyokuwa tu, atalalamika na kulaumu, yaani ni sehemu ya maisha yake.
Siyo wote hapa JF tunalaumu hii hatua. Huwezi kujua pengine huyu member ana hisa kwenye hizo hoteli. Ni member mmoja ametoa maoni yake japo hata mimi naona ni potofu. Hiki kilio kimekuwepo hapa jamvini kwa muda mrefu sana na kama serikali itachukuwa hatua itakuwa jambo zuri. Mabasi yakisimama stendi watajitokeza watu wengi wataokaboresha hoteli na huduma zake na wasafiri watafaidi kwani kutakuwa na ushindani wa bei na kutoa huduma tofauti na sasa ambapo abiria wanalazimishwa kula sehemu moja ambayo wenye hoteli wanaweka bei wanayotaka na hakuna ushindani wala variety ya chakula.
 
Pamoja na hayo lakini hii ni hatua nzuri kabisa. Wengi tumekuwa tunalalamika hapa mabasi yanatupeleka hoteli ambazo bei zao wanapanga bila kujali kwani wanajua hakuna ushindani na abiria hana sehemu nyingine ya kula. Wakihamia stendi watajitokeza watu wengi wataokajenga au kuimarisha hoteli za stendi kama zamani.
... huko kwenye hoteli za stendi nako bei itapanda. Tena wamepewa monopoly ndio balaa kabisa; wanajua basi ipende, isipende itakuja hapa not only bei lakini huduma zitakuwa mbovu ajabu.

Muhimu mkata tiketi ataarifiwe mapema hoteli ambayo basi litasimama kwa ajili ya chakula ili aamue kukata ya basi hilo au lingine. Hii itaondoa monopoly na nguvu ya kuamua itakuwa imerudishwa kwa abiria hivyo hoteli zitashindana both in terms of price and QoS.
 
Hizi ni ndoto za alinacha..mabasi kama KLM yaende kusimama kwenye vistendi vya ovyo ovyo..? Kila basi Liwe na hotel yake kama KLM anavyofanya
Mabasi ya abiria yanatoa huduma kwa kufuata sheria zilizowekwa na serikali. Pengine wewe una umri mdogo na hujui huduma zilivyokuwa zamani wakati mabasi yanasimama stendi. Hizo unazoita ''vistendi vya hovyo hovyo'' zilikuwa ni stendi zenye hoteli na huduma nzuri sana lakini wenye mabasi walipoanza kulamisha kusimama kwenye hoteli wenye maslahi nazo ili wapate faida kubwa au kupewa kamisheni ndiyo hoteli za stendi zilivyodorora. Kila basi haliwezi kuwa na hoteli yake na kisheria sehemu ya basi kusimama ni stendi.
 
Back
Top Bottom