Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,753
- 218,366
Abiria wa kutoka mikoani na ambao walizoea mabasi wanayopanda kuwashusha karibu na makwao kama Mbagala, Kigamboni na Chanika wamefanya mgomo wa kushukia kwenye kituo hicho kikuu cha mabasi, kwa madai kwamba itawasababishia usumbufu mkubwa na kuongeza gharama za safari.
Serikali ya Tanzania imeyataka mabasi yote kupakia na kushusha abiria wake kwenye kituo hicho badala ya utaratibu wa zamani wa baadhi ya mabasi kuwapeleka abiria hadi kwenye Yard binafsi.
Chanzo: ITV
My take: niliwahi kuandika madhara ya jambo hili hapa jukwaani, hasa baada ya RC Amos Makalla kuja na mpango huo wa kulazimisha mabasi yote yapakie na kushusha Mbezi.
Nilishauri kwamba Mabasi yasizuiwe kupakia wala kushusha kwenye yard zao, lakini yalazimishwe kupitastendi ya mbezi kushusha na kupakia.
Ni ujinga mkubwa sana kwa basi linaloenda yard yake kigamboni kuacha abiria wanaoenda huko kituo cha Mbezi. Jambo hili ni unyama na halikubaliki, serikali ni lazima ijitafakari .
NOTE: Kwa taarifa hii naamini kwamba sijaitukana serikali mtandaoni kama Waziri Masauni alivyotuasa!