Ndugu na Marafiki, Acheni tabia ya kuuliza unazaa lini!

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
Kwema??

Niende tu fasta, hii ishu binafsi naiona haijakaa poa. Kuna baadhi ya mambo yaachwe baina ya wana ndoa tu.

Ndugu wanayo haki ya kuuliza, sawa, lakini wakishapewa jibu wawe waelewa - Sio kila mtu anataka watoto na yuko tayari kuliongelea hili swala.

Maswali ya kuzaa kila iitwapo leo.. Sad!! Thing is, others enjoy life child free! Hata hivo, kwa kuwa unao uwezo wa kuzaa haimaanishi ni lazima uzae.

Pili, Tatizo la ugumba na tasa lipo kuliko unavyodhani. Ishu za mimba kuchoropoka zinatokea kuliko zinavyoongelewa! Ifike pahala ieleweke hivo.

Ndugu na marafiki acheni tabia ya kuuliza mtu anazaa lini. Tunaelewa mnajali, you have a good sense of caring yes ila don't feel so entitled to decide what is to be done in other people businesses!!

Kila mtu ni kwa ajili yake. Mungu tu ndio wa kwetu sote. Mtu akiona ni wakati sahii kwake kuwa na/kuongeza mtoto atazaa. Acheni mambo yenu! JIHESHIMUNI.
 
Hawajui kuna watu wanatamani kupata watoto lakini inashindikana, mtu kama huyo kumuuliza hivyo si unamuumiza
Mi wifi yang amebeba mimba, sasa sikuhiyo anavyonipa taarifa za ujauzito wake mwishoni mwa mazungumzo ananiuliza "vipi nikurushie nini uwe nayo na ww", niliumia sana coz mwaka wa tano sasa natafuta mtoto. Na yy ameolewa baada yngu na anawatoto wawili sasa mi hata mmoja mungu hajanipa.
 
Dah, pole sana mkuu, maneno ya mwanadamu ambaye hajui hata sekunde moja ya maisha mbele itakuwaje yasikutishe(rejea tukio la msamvu, r.i.p ndugu zetu).
Kumbuka kila jambo hutokea kwa sababu (kama ni Mkristo rejea habari za Sara na Isaka, Anna na Samwel, Rahel na Yusuph e.t.c) halafu mshukuru Mungu wako.
 
Dah, pole sana mkuu, maneno ya mwanadamu ambaye hajui hata sekunde moja ya maisha mbele itakuwaje (rejea tukio la msamvu, r.i.p ndugu zetu).
Kumbuka kila jambo hutokea kwa sababu (kama ni Mkristo rejea habari za Sara na Isaka, Anna na Samwel, Rahel na Yusuph e.t.c) halafu mshukuru Mungu wako.
Ujumbe mujarabu kabisa huu!
 
Back
Top Bottom