Ndugu AUGUSTINO MTITU aliyejeruhiwa kwa kuchomwa na mkuki jana anaendelea vizuri na matibabu

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
SIFA NA UTUKUFU ARUDISHIWE MWENYEZI MUNGU.

Maendeleo Ya Ndugu AUGUSTINO MTITU aliyejeruhiwa kwa kuchomwa na mkuki jana tarehe 25/12/2016 Kijiji cha Dodoma Isanga Kata Ya Masanze Jimbo La Mikumi na jamii ya wafugaji, hivi sasa anaendelea vizuri na matibabu baada ya kutolewa mkuki mdomoni salama salimini kwenye HOSPITALI YA MKOA MOROGORO na amelazwa wodi namba moja hospitalini hapo.

Ofisi Ya Mbunge Jimbo La Mikumi inatoa shukrani zake za dhati kwa Madaktari na wauguzi waliofanikisha zoezi hilo, Lakini pia Ofisi Ya Mbunge Mikumi itakuwa ikiwapa maendeleo ya Bwana AUGUSTINO MTITU mpaka hapo hali yake itakapokua imetengemaa. Lakini la muhimu zaidi Mh. Mbunge amefanya mawasiliano na ngazi mbalimbali zinazohusika akiwemo Waziri wa Mambo Ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba juu ya kile kilichotokea na waziri amesikitika sana na ameahidi kulifuatilia suala hili kwa kina na kulitolea maamuzi magumu.

Imetolewa na :- Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Jimbo La Mikumi.
FB_IMG_1482765070646.jpg
 
wafugaji ni viumbe wa ajabu sana. wamefanya maeneo yao ya huko usukumani na umasaini kuwa jangwa, wakaamia morogoro ambako asili yao sio wafugaji kabisa, na wanajifanya maeneo hayo ni yao. nilishawahi kushuhudia wanalisha shamba la mahindi kwa makusudi kabisa. vichwa vyao ni vyeupe balaa.
 
Back
Top Bottom