Ndugai asisahau, kadi yake ya CCM ndio inampa uspika, CCM wanaweza kuiondoa muda wowote na akawa raia wa kawaida tu

Kwa mujibu wa katiba, mtu yeyote anaweza kugombea uspika na kuchaguliwa. Ni kweli anaweza kuvuliwa uanachama na kupoteza ubunge lakini hawezi kupoteza uspika. Vile vile hata ikilazimishwa apoteze uspika anaweza kugombea tena uspika kama raia huru au kudhaminiwa na chama kingine na wabunge kama wanampenda watamchagua tena kuwa spika.
Hivi wewe unazungumzia siasa za nchi gani?!!kweli kwa akili za kawaida hili linaweza tokea kwa Tz?yaani spika awe hana chama?eti kama wabunge wanampenda watamchagua tena!
Kifupi akifukuzwa ccm, automatically na uspika ndio basi tena, bila kuangalia mazingira mengine.
 
Kuna watu wanamdanganya eti anaweza kutikisa Urais wa Samia. Wasidanganye, siku anaanza ndio siku anafutiwa uanachama, ubunge wake unakoma, na uspika unakoma
Wewe unaamini unalielewa hilo kumshinda Ndugai?
 
Hebu tupeleke polepole , unasema spika wa Bunge la JMT si lazima awe mbunge?
YES, SIR! Tena sio "si lazima awe mbunge" tu bali "si lazima awe mwanachama wa siasa"! Hata wewe, hata kama sio mbunge na sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bado unaweza kugombea na kuukwaa uspika provided sifa zingine unazo!
 
Kuna watu wanamdanganya eti anaweza kutikisa Urais wa Samia. Wasidanganye, siku anaanza ndio siku anafutiwa uanachama, ubunge wake unakoma, na uspika unakoma
pety analogy. vitisho vya kijinga
 
Sasa atakuwaje mbunge.. akivuliwa ubunge anakuwa hana sifa ya kuwq spika
Umasema??? Akifukuzwa uanachama ataendelea kuwa spika kama wale covid 19???
Sijui unaongea kwa kujifurahisha au ni nini, huyu ameupata uspika kupitia Chama, hakupata uspika kupitia mgombea asiye na Chama. Kama CCM mpaka Leo hawataki mgombea binafsi hata wa ubunge au udiwani ndiyo watakubali spika asiye na Chama???
Ibara ya 84(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema:

Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.

Je, mna maswali zaidi?! Naweka mkazo: mtu halazimiki kuwa mbunge ili kuwa spika wa bunge! Anayelazimika kuwa mbunge ni Naibu Spika!
 
Hivi wewe unazungumzia siasa za nchi gani?!!kweli kwa akili za kawaida hili linaweza tokea kwa Tz?yaani spika awe hana chama?eti kama wabunge wanampenda watamchagua tena!
Kifupi akifukuzwa ccm, automatically na uspika ndio basi tena, bila kuangalia mazingira mengine.
Soma kwanza katiba. Sharti la kuwa spika sio lazima awe mbunge; ila naibu spika ni lazima awe mbunge.

Hivyo kumfukuza uanachama kutamvua ubunge tu sio uspika. Pili nafasi ya uspika ni kubwa sana kumpoka inahitaji timing sana la sivyo nakuambia nchi itatikisika hata kana hatimaye mwishoni itafanikiwa lakini tayari madhara makubwa yatakuwa yametokea. Kumbuka kura zinapigwa kwa siri na wale wabunge kwa uchache wao wanaweza kabisa kumsapoti wakati wa kura. Narudia tena suo rahisi kumg'oa bila nchi kutikisika.

Kinachowezekana na kumvizia mwaja 2025 wakati kiti kikiwa wazi kama ilivyokuwa wakati ule wa Sitta.
 
Ibara ya 84(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema:

Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.

Je, mna maswali zaidi?! Naweka mkazo: mtu halazimiki kuwa mbunge ili kuwa spika wa bunge! Anayelazimika kuwa mbunge ni Naibu Spika!
Embu nenda namba 84.7 hapo alafu utujibu hapa ndugai akivukiwa uanachama uspika wake unakuwaje??

84.(7) Spika atakoma kuwa spika na ataacha kiti cha spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa mbunge kwasababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa bunge.
 
Kuna watu wanamdanganya eti anaweza kutikisa Urais wa Samia. Wasidanganye, siku anaanza ndio siku anafutiwa uanachama, ubunge wake unakoma, na uspika unakoma
acha ujinga, wewe, basi kama ni hivyo bunge zima. Litanyang'anywa hizo kadi. Asilimia 90 ya wabunge wote wapo upande wa Ndugai achana na hao wanao wapiga domo wasio bungeni
 
Kudhaminiwa na chama sio hoja, hoja ni matakwa ya mtu kuwa spika!! Kudhaminiwa na chama ndo hiyo backup ninayoisema lakini unaweza kugombea uspika hata kama huna chama!!
Atapoteza sifa ya kuwa mbunge tu na atabaki kuwa na sifa ya kuwa spika.
 
Soma kwanza katiba. Sharti la kuwa spika sio lazima awe mbunge; ila naibu spika ni lazima awe mbunge.

Hivyo kumfukuza uanachama kutamvua ubunge tu sio uspika. Pili nafasi ya uspika ni kubwa sana kumpoka inahitaji timing sana la sivyo nakuambia nchi itatikisika hata kana hatimaye mwishoni itafanikiwa lakini tayari madhara makubwa yatakuwa yametokea. Kumbuka kura zinapigwa kwa siri na wale wabunge kwa uchache wao wanaweza kabisa kumsapoti wakati wa kura. Narudia tena suo rahisi kumg'oa bila nchi kutikisika.

Kinachowezekana na kumvizia mwaja 2025 wakati kiti kikiwa wazi kama ilivyokuwa wakati ule wa Sitta.
Sijakataa kuwa spika, ni lazima awe na chama, hilo ni suala la kikatiba, lakini kwa siasa zetu hilo haliwezekani, ktk nchi hii ni mala ngapi wanapoamua kudhibitiana wana ccm, wanalazimisha kura zipigwe wazi?na sasa hivi huwaoni wabunge wakisema ni kutokana na kutojua nini kitafuata, lakini mfano kwa sasa, katibu mkuu wa ccm/kamati kuu itoe tamko kali juu ya Ndugai, labda la kumfukuza uanachama, utawaona watakavyojitokeza, na likishafanyika hilo tu, hiyo kanuni inabadirishwa tu ya kuwa kura itapigwa kwa kunyoosha vidole, kwisha habari yake.ndio maana nikasema ikifikia huko tu uspika utapotea tu, Nchi hii wakiamua hakuna cha eti katiba inasemaje.Hakuna nchi kutikisika.
Utaratibu wa kumtoa CAG, si upo wazi kikatiba nini kilimtokea?
Hii ni Afrika bnana,
 
Kuna watu wanamdanganya eti anaweza kutikisa Urais wa Samia. Wasidanganye, siku anaanza ndio siku anafutiwa uanachama, ubunge wake unakoma, na uspika unakoma
Ndio uzuri wa katiba ! Maana katiba ni sheria mama !!
 
Ule ushauri wake ndio unawafanya muanze kuona anyang'anywe kadi?
Hivi hii nchi akili tumezipeleka wapi?
Mbona hatuna uwezo wa tafakuri?
Kwanini tusitafakari ushauri wake?
Kwanini kila kauli itolewayo ionekane ni hujuma?
Kwani hata huyo Rais kinachompa sio kadi ya CCM?
Au Katibu Mkuu wa CCM, kinachompa cheo sio kadi?
Yaani hatutaki kupewa ushauri wa tahadhari juu ya mikopo?
Kwani nchi ngapi maskini zimeshazidiwa na mikopo?
Ninyi haya mmeyajua leo kuwa kuna mawazo mbadala, mbona upinzani wakitoa mawazo mbadala zengwe linakuwa kubwa sanaa
 
acha ujinga, wewe, basi kama ni hivyo bunge zima. Litanyang'anywa hizo kadi. Asilimia 90 ya wabunge wote wapo upande wa Ndugai achana na hao wanao wapiga domo wasio bungeni
Wabunge wako upande wake? Alianzishe halafu ageuke nyuma aangalie walio upande wake, hatawaona, Siasa ni unafiki pias
 
Unaweza kuwa Spika hata usipokuwa mwanachama wa chama cha siasa unless kama kifungu husika cha katiba kimebadilishwa! Sema, akifukuzwa CCM, halafu 2025 akajaribu tena kugombea, kwake itakuwa ngumu kupita bila backup ya CCM
Unaweza kuwa spika bila kua mbunge?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom