Ndoto mbaya zinazoleta usumbufu ndotoni

Ndoto mbaya zinazoleta usumbufu ndotoni

anamila

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2017
Posts
227
Reaction score
356
Wasalaam,
Mwenyezi Mungu ametuamsha salama kabisa wakuu.

Nina changamoto ya ndoto zinazonisumbua sana, zipo za aina tofauti 5 isipokuja hii itakuja hii. Zipo hivi:

Naota nafanya mapenzi na jitu nisiloifahamu. Hapa linaweza nibadilisha niwe mwanaume lenyewe linakuwa la kike au linakuwa la kiume linaniingilia.

Naota nakimbizwa na N'gombe mkuubwa mweusi mwenye pembe Kali sana.. Huwa nakimbia sana na linaponikosa ghafla hubadilika na kuwa binadamu na kuanza kunirushia mishale mingi kwa haraka ila mungu mwema halijawahi kunichoma na mshale.

Naota nataka kung'atwa na nyuki...! Lakini pia naota kuna majoka yananikimbiza ila moja ya majoka haya hujificha sehemu/ kama kujibanza ili lisionekane.

Naota nimetekwa..hii ndio niliyoiota hata leo! Hapa huwa nakuwa na wakati mgumu sana wa kukabiliana na mtekaji.. Nimekimbia sana nimeomba wapita njia msaada lakini Mzee mmoja alisema nastahili kutekwa, .. Nilijaribu kumkimbia mtekaji na pikipiki ila kabla sijapanda pikipiki nae alichukua yake akaanza kumfukuza bodaboda niliyemkodi.. Tumesumbuana sana ila mwisho kuna wanaume nilikutana nao na mmoja wao akanishika mkono yule mtekaji akakubali kushindwa.

Wakuu hii ni hali y kawaida au ni mini... Hiizi ndoto zimekuwa na muda mrefu kama miaka minne .. Ila miaka ya hivi karibuni linakuwa sugu.

Je wewe unaota ndoto za aina moja tu? Nakaribisha maoni na ushauri nifanyeje ili nisiote tena?
 
Hizo ndoto ni mbaya na usipozifuatilia zitakugharimu nikushauri Fuatilia hii video kwa makini kuna kitu kikubwa sana utajifunza

Angalia na hii usiruke angalia kwa makini mwanzo mwisho

Asante mkuu
 
Ndoto ni milango ya ulimwengu wa Kiroho.Kwa ndoto unaweza kukutana na ulimwengu wa giza au nuru.Ulimwengu wa kiroho unaweza kumiliki maisha yako kupitia ndoto.Samahani nitatumia biblia kufafanua,Mfano katika biblia malaika wa Bwana alimtokea Yusufu ktk ndoto kumpa warning amuondoe Yesu bethlehem ssb herode alitaka kumuua.Mathayo 2:13.Ndoto ni channel ya Mungu kuwasiliana na wanadamu.Hivyo hivyo shetani hutumia milango hiyo hiyo kukutana na binadamu.Kwa maelezo ya ndoto yako ulimwengu wa giza unakutesa kupitia ndoto.Ushauri wangu tumia damu ya Yesu,Damu ya Yesu itakuokoa kwenye hili tatizo,haijalishi una imani ipi biblia inasema ukimkiri Yesu kwa kinywa kuwa ni Bwana na kwamba Yeye ni mwana wa Mungu utaokoka.Warumi 10:9 Mkiri Yesu na umpokee moyoni mwako ili akupiganie hii vita hutaweza peke yako.Ukishakiri Yesu ataokoa nafsi yako then anza kufanya maombi na kujifunika kwa damu ya Yesu.Tafuta watumishi wanaoweza kukuombea mpaka upokee deliverance.Pia kama unaweza kupata Lion of Judah oil ya Prophet Shepherd Bushiri au TB Joshua apply kabla hujalala.

Sexual dreams demons can destroy your life completely,kama hujaoa unaweza usioe na hakuna relationship inawork,na kila ukitazama hutaelewa umekosea wapi sbb sio wewe ni mapepo yanafight kuuwa destiny yako.Na hata kama umeoa mahusiano yanakuwa magumu mno hakuna furaha na ukitafuta sababu hamzioni,kuachana ndio inakuwa solution.These are the worst demons on earth,Yesu tu ndio anaweza kukusaidia.
 
Kwenye kuota unaingiliwa.. Umeshawahi hesabu marinda yako ukakuta yamitimia (yaani marinda 16, 8chini 8 juu). Maana usijesema ni ndoto kumbe kunajamaa anakufanyia ziara
 
Ningekwambia kitu ila naona uvivu kuandika,,, vipi unaishi nyumba za kupanga;???
 
Ndoto ni milango ya ulimwengu wa Kiroho.Kwa ndoto unaweza kukutana na ulimwengu wa giza au nuru.Ulimwengu wa kiroho unaweza kumiliki maisha yako kupitia ndoto.Samahani nitatumia biblia kufafanua,Mfano katika biblia malaika wa Bwana alimtokea Yusufu ktk ndoto kumpa warning amuondoe Yesu bethlehem ssb herode alitaka kumuua.Mathayo 2:13.Ndoto ni channel ya Mungu kuwasiliana na wanadamu.Hivyo hivyo shetani hutumia milango hiyo hiyo kukutana na binadamu.Kwa maelezo ya ndoto yako ulimwengu wa giza unakutesa kupitia ndoto.Ushauri wangu tumia damu ya Yesu,Damu ya Yesu itakuokoa kwenye hili tatizo,haijalishi una imani ipi biblia inasema ukimkiri Yesu kwa kinywa kuwa ni Bwana na kwamba Yeye ni mwana wa Mungu utaokoka.Warumi 10:9 Mkiri Yesu na umpokee moyoni mwako ili akupiganie hii vita hutaweza peke yako.Ukishakiri Yesu ataokoa nafsi yako then anza kufanya maombi na kujifunika kwa damu ya Yesu.Tafuta watumishi wanaoweza kukuombea mpaka upokee deliverance.Pia kama unaweza kupata Lion of Judah oil ya Prophet Shepherd Bushiri au TB Joshua apply kabla hujalala.

Sexual dreams demons can destroy your life completely,kama hujaoa unaweza usioe na hakuna relationship inawork,na kila ukitazama hutaelewa umekosea wapi sbb sio wewe ni mapepo yanafight kuuwa destiny yako.Na hata kama umeoa mahusiano yanakuwa magumu mno hakuna furaha na ukitafuta sababu hamzioni,kuachana ndio inakuwa solution.These are the worst demons on earth,Yesu tu ndio anaweza kukusaidia.
Asante Joanna.. Mungu akubariki.
 
Back
Top Bottom