Ndoto mbaya zinazoleta usumbufu ndotoni

Ndoto mbaya zinazoleta usumbufu ndotoni

Hakikisha kabla hujalala jifunike kwa damu ya Yesu na ufunike malango ya ndoto zako ilinshetani asipite.

Pia omba toba maana dhambi hufungua mlango ili shetani akutese. Kaa vizuri na Mungu wako na hio nyumba unapolala iombee.

Ubarikiwe
 
Kwenye kuota unaingiliwa.. Umeshawahi hesabu marinda yako ukakuta yamitimia (yaani marinda 16, 8chini 8 juu). Maana usijesema ni ndoto kumbe kunajamaa anakufanyia ziara
Aiseee barikiwa sana mkuu. Nakushukuru kwa kuchangia mada.
 
Ndoto ni milango ya ulimwengu wa Kiroho.Kwa ndoto unaweza kukutana na ulimwengu wa giza au nuru.Ulimwengu wa kiroho unaweza kumiliki maisha yako kupitia ndoto.Samahani nitatumia biblia kufafanua,Mfano katika biblia malaika wa Bwana alimtokea Yusufu ktk ndoto kumpa warning amuondoe Yesu bethlehem ssb herode alitaka kumuua.Mathayo 2:13.Ndoto ni channel ya Mungu kuwasiliana na wanadamu.Hivyo hivyo shetani hutumia milango hiyo hiyo kukutana na binadamu.Kwa maelezo ya ndoto yako ulimwengu wa giza unakutesa kupitia ndoto.Ushauri wangu tumia damu ya Yesu,Damu ya Yesu itakuokoa kwenye hili tatizo,haijalishi una imani ipi biblia inasema ukimkiri Yesu kwa kinywa kuwa ni Bwana na kwamba Yeye ni mwana wa Mungu utaokoka.Warumi 10:9 Mkiri Yesu na umpokee moyoni mwako ili akupiganie hii vita hutaweza peke yako.Ukishakiri Yesu ataokoa nafsi yako then anza kufanya maombi na kujifunika kwa damu ya Yesu.Tafuta watumishi wanaoweza kukuombea mpaka upokee deliverance.Pia kama unaweza kupata Lion of Judah oil ya Prophet Shepherd Bushiri au TB Joshua apply kabla hujalala.

Sexual dreams demons can destroy your life completely,kama hujaoa unaweza usioe na hakuna relationship inawork,na kila ukitazama hutaelewa umekosea wapi sbb sio wewe ni mapepo yanafight kuuwa destiny yako.Na hata kama umeoa mahusiano yanakuwa magumu mno hakuna furaha na ukitafuta sababu hamzioni,kuachana ndio inakuwa solution.These are the worst demons on earth,Yesu tu ndio anaweza kukusaidia.
Amazing mkuu asante na ushauri wako nitaufuata nimekuelewa vizuri sana
 
Wasalaam,
Mwenyezi Mungu ametuamsha salama kabisa wakuu.

Nina changamoto ya ndoto zinazonisumbua sana, zipo za aina tofauti 5 isipokuja hii itakuja hii. Zipo hivi:

Naota nafanya mapenzi na jitu nisiloifahamu. Hapa linaweza nibadilisha niwe mwanaume lenyewe linakuwa la kike au linakuwa la kiume linaniingilia.

Naota nakimbizwa na N'gombe mkuubwa mweusi mwenye pembe Kali sana.. Huwa nakimbia sana na linaponikosa ghafla hubadilika na kuwa binadamu na kuanza kunirushia mishale mingi kwa haraka ila mungu mwema halijawahi kunichoma na mshale.

Naota nataka kung'atwa na nyuki...! Lakini pia naota kuna majoka yananikimbiza ila moja ya majoka haya hujificha sehemu/ kama kujibanza ili lisionekane.

Naota nimetekwa..hii ndio niliyoiota hata leo! Hapa huwa nakuwa na wakati mgumu sana wa kukabiliana na mtekaji.. Nimekimbia sana nimeomba wapita njia msaada lakini Mzee mmoja alisema nastahili kutekwa, .. Nilijaribu kumkimbia mtekaji na pikipiki ila kabla sijapanda pikipiki nae alichukua yake akaanza kumfukuza bodaboda niliyemkodi.. Tumesumbuana sana ila mwisho kuna wanaume nilikutana nao na mmoja wao akanishika mkono yule mtekaji akakubali kushindwa.

Wakuu hii ni hali y kawaida au ni mini... Hiizi ndoto zimekuwa na muda mrefu kama miaka minne .. Ila miaka ya hivi karibuni linakuwa sugu.

Je wewe unaota ndoto za aina moja tu? Nakaribisha maoni na ushauri nifanyeje ili nisiote tena?
Pole sana mkuu, binafsi nimejifunza somo la ndoto recently kutoka kwa watumishi kadhaa. Kwako hapo nnaona una vita kubwa. A war that you should not joke with. Nimeona kuna mdau ameku refer kwa video za Mwl mwakasege, well. Lkn nadhan hazipo directly related to your case. Hebu zama YouTube Mcheki mtumishi mmoja anaitwa Dr Daniel Olukoya ameelezea vizuri sana kuhusu ndoto. Just search "Dealing with evil dreams seed by Olukoya" sikiliza itakufungua macho kirahisi.. barikiwa.
 
Ndoto ni ujumbe /taarifa ya yale kinachoendelea katika maisha yako katika ulimwengu was kiroho ambayo inaweza kuwa na adhari katika maisha yako halisi kama hautachukua hatua.
Ndoto pia ni mlango ambao unaweza kutumiwa na Mungu au miungu kuingilia maisha yako kwa wema ikiwa ni Mungu, kwa ubaya ikiwa ni shetani.Mlango huo unafunguliwa kama IPO mikataba\maagano kati yako\wazazi wako\mababu na Mungu au miungu/shetani
Vyanzo vya ndoto ni:
1.Mungu kusema na wewe
2.shetani
3.shughuli nyingi za Siku husika
4.arthi unapolala ikiwa kuna mazindiko au madhabahu

Aina ya ndoto unazoota inaonekana sio nzuri ni za shetani MF nyoka anakufukuza INA maana adui anataka ukose utulivu/focus kufanikisha maono yako.
Cha kufanya
Tubu kama we ni mkristo tumia damu ya Yesu kunyunyiza katika maeneo yote ambayo unawaona hao maadui.
Nyunyuza damu ya yesu kwa imani ulitakaze lango LA ndoto ukizuia ndoto zote mbaya zisipenye kuna kwako.
Ref.kutoka12:12,22
Damu ya Yesu ndo damu pekee nyenye nguvu kwenye ufalme was Mungu na dhidi ya shetani.
 
Kipengele cha Kuota harusi na misiba na pia na kula minyama hadi naamka nikiwa kichefuchefu nimekisahau hapo juu .
Pole sana. Kutokana na ndoto zako hapo kuna nguvu za giza unazopigana nazo.
Usikimbilie kwa waganga watakutapeli, hakuna suluhu kwa waganga zaidi ya kutuliza tu.
Tafuta kanisa lolote lenye nguvu za Mungu. Usikimbilie kwa manabii kwa sbb sasa hawana tofauti na waganga wa kienyeji
Omba mchungaji akuongoze sala ya toba na uanze kusali (siyo kusali uwepo kanisani hapana hata nyumba inabid usali)
Kabla ya kulala Muombe YESU KRISTO WA NAZALETI ALIYE HAI akusaidie.
Kuhusu ndoto huwa ni jambo la kweli ktk ulimwengu wa kiroho. Nakumbuka kuna sehemu nilienda, hiyo sehemu bila kusali, narudia tena BILA KUSALI ILI YESU ANILINDE nilikuwa naota ndoto mbaya kila siku. Ila nilipoanza kusali hali ilitulia kbsa.
Ndoto ambayo siwezi kuisahau ni hii.
Niliota nipo na rafiki yangu tunaenda sehemu fulani huku tunapiga story( ni sawa na ww nikuambie unisindikie sehemu fulani) basi tumeondoka tunaenda sehemu hiyo ina mandhari ya kijiji
NITAENDELEA
 
Endelea nakuomba[emoji120] [emoji120]
 
Ndoto ni ujumbe /taarifa ya yale kinachoendelea katika maisha yako katika ulimwengu was kiroho ambayo inaweza kuwa na adhari katika maisha yako halisi kama hautachukua hatua.
Ndoto pia ni mlango ambao unaweza kutumiwa na Mungu au miungu kuingilia maisha yako kwa wema ikiwa ni Mungu, kwa ubaya ikiwa ni shetani.Mlango huo unafunguliwa kama IPO mikataba\maagano kati yako\wazazi wako\mababu na Mungu au miungu/shetani
Vyanzo vya ndoto ni:
1.Mungu kusema na wewe
2.shetani
3.shughuli nyingi za Siku husika
4.arthi unapolala ikiwa kuna mazindiko au madhabahu

Aina ya ndoto unazoota inaonekana sio nzuri ni za shetani MF nyoka anakufukuza INA maana adui anataka ukose utulivu/focus kufanikisha maono yako.
Cha kufanya
Tubu kama we ni mkristo tumia damu ya Yesu kunyunyiza katika maeneo yote ambayo unawaona hao maadui.
Nyunyuza damu ya yesu kwa imani ulitakaze lango LA ndoto ukizuia ndoto zote mbaya zisipenye kuna kwako.
Ref.kutoka12:12,22
Damu ya Yesu ndo damu pekee nyenye nguvu kwenye ufalme was Mungu na dhidi ya shetani.
Asante mkuu wangu.
 
Ukishakiri Yesu ataokoa nafsi yako then anza kufanya maombi na kujifunika kwa damu ya Yesu.Tafuta watumishi wanaoweza kukuombea mpaka upokee deliverance.Pia kama unaweza kupata Lion of Judah oil ya Prophet Shepherd Bushiri au TB Joshua apply kabla hujalala.

Mkuu;
Hapo ndio umenimaliza kabisa. Kwanza; Kujifunika kwa damu ya Yesu. Hivi, ile damu ya Yesu iliyomwagika pale msalabani ilimwagwa kutuosha dhambi zetu au ni kwa ajili ya kuwa blanketi letu la kujifunikia??
Pili; Hao watumishi wa bwana; Bushiri na Tb Josjua, watakaa milele au? Yaani wakifa leo (Mungu apishe mbali) ndo uhuru wa mapepo kuuonea ulimwengu??
Tatu; Hayo mafuta ni bure au yana gharama?? Niliwahi kusoma mahali flani kwenye hiyo hiyo biblia yako kuw; Mlipewa bure, toeni bure. Leo iweje Mungu ampe utajiri mkuu Bushiri ati Lion of Judah oil, ya kutoa mapepo. Aje awauzie wenye shida ka huyu mtu. Kweli huyo Mungu ni mwenye haki??
Jamani, poteeni wenyewe msiwatafute wenye shida mkawaongezea mizigo zaidi.
Nadiriki kusema; Nitawaamini watumishi wengi sana lakini sio hawa Mitume wenu na Manabii wenu wa kuchongwa. Yesu alijua tutakutana na haya magumu hivyo angelituachia mafuta hayo na maji hayo in plenty.
Endeleeni kuwanadi hawa wenye dhiki lakini mjue Mungu anawaona.
Mtoa mada, sijui weye ni dini gani lakini usimfuate huyu JOANNA. Ni mwana wa upotevu huyu haswaaaa
 
Endelea nakuomba[emoji120] [emoji120]
Sawa
Cha ajabu tunaota pamoja na shemeji yako ndoto mbaya kila siku. Bila kusali ilikuwa ni shida. Ok
Back to the story

Basi tupo barabarani tunapiga story, kumbuka haya ni mazingira ya kijijini. Tukapita karibu na nyumba mmoja ya nyasi, kulikuwa na watu nje wazee wanaongea. Basi tukawasalimia. Kulikuwepo na mtoto mdogo umri km miaka 11 wa kiume nikamuomba maji ya kunywa. Basi akaingia ndani akatoka na jagi na kikombe. Akanimimia maji kweny kikombe, napokea naweka kikombe mdomo, naangalia jagi naona lina mavi ya binadamu mabichi, nikatema pyuuuu, kuangalia kweny kikombe kina mavi.....
Hapo hapo nikamwambia rafiki yangu twende.
Tumeondoka hatujazungumza chochote. Tumeenda kwa mbele kulikuwa na nyumba ya nyasi. Nikamwambia rafiki yangu tupite hapo niombe maji kwa sabb nina kiu na pia nataka ninawe uso.
Tumefika tukawasalimia. Nikaomba maji. Hapo nje kulikuwa na madumu, na kulikuwa na mtoto wa kiume yupo kifua wazi halafu kavaa kaptula ya blue lkn imeshaisha isha.
Hii nyumba ilikuwa na mawe madogo kwa nje. Siyo yakuwekwa hapana . Basi nikachukua dumu nikazunguka nyuma kwenye mawe, na huyu dogo alikuwepo.
Ile namimina hivi mavi.., yakamwagika kweny mikono yangu mabichi, nilikaliachia dumu, mavi yakawa yanamwagika (ni yale ambayo mtu katoka kujisaidia muda si mrefu). Cha ajabu kipind nabeba dumu sikusikia harufu yyte. Kinyaaa mpaka nikaanza kutapika, nilipomtazama huyu mtoto alikuwa amekaa chini, kaptula yake ilikuwa imejaa mavi yaliyoanza kukaukiana. Nikapiga kelele nikamwambia rafiki yangu tuondoke. Nikashituka toka usinginzini ila kinyaaaa. Tangia hapo siwezi kulala bila kusali. Cha ajabu ndoto hiz za ajabu zilikuwa kila siku km haujasali. Ukisali unalala vizuri, usingiz mtamu. Niliamka asubuhi nahis kinyaaa
 
Back
Top Bottom