Ndoa yangu ipo mashakani

Ndoa yangu ipo mashakani

J Mbungi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
269
Reaction score
74
Naomba msaada wa kuinusuru ndoa yangu(Naona ipo ukingoni...

Mimi ni baba mwenye watoto wawili(7 & 4) Nipo kwenye ndoa mwaka wa 8 sasa... Nimeanza kupata matatizo na mke wangu yapata mwaka sasa kuhusiana na TENDO Zima la mchezo wa kitandani..

Kwakweli nimeshindwa hata kumuelewa,ANANIKATALIA kufanya mapenzi kwa visingizio kibao(Mara anasikia usingiz sana,mara hajisikii,mara amechoka sana)..Yaani ndani ya huu mwaka sijawahi kufanya naye mapenzi kwa ridhaa yake bila kumlazimisha kwanguvu)..

Yaani imefika wakati nika amua kumsaidia kazi zoote za nyumbani(Kufua kupika na kadhalika) Ili mradi akifika nyumbani asifanye kazi yoyote ya kumchosha..LAIKINI haija saidia kitu.. ANASEMA HANA HAMU KABISA HATA MWAKA UNAWEZA KUPITA BILA KUFANYA MAPENZI(WALA HAONI TAABU)..

Mwanzoni alikuwa akifanya kazi mjini(Akiondoka alfajiri na kurudi Jioni sana)..Sasa nimemfungulia salon hapa hapa maeneo ya nyumbani(Yote hiyo ni kujaribu kumpunguzia uchovu anosema ndio unamfanya akose HAMU.. Lakini haijasaidia kitu..

Kusema ukweli hii hali imenichanganya sana..( Mimi si mtu wa kutoka wala sijawazia jambo hilo) Lakini nitaishije bila kupata haki yangu ya ndoa??? Na mke ninaye???!

JAMANI NAOMBA USHAURI HATA KAMA NI WA KITABIBU : MAAANA HATA KAMA ANATEMBEA NA MTU MWINGINE(HATEMBEI NAYE KILA SIKU) LAZIMA KUNA SABABU ZA KIAFYA ZINAZOMFANYA HAKOSE HAMU...
 
Mh wengi wamelala, ngoja wakiamka kesho watakusaidia!! hii mi naona hutokeaga for sometime and not always sasa kama yako imefikia zaidi ya mwaka basi nahisi kuna tatizo!! Health problem, jaribu kumpa vyakula vitakavyoongeza ashiki, muone daktari kwa maelezo zaidi manake mi naijua REDDS tu
 
Awali ya yote pole.

Natumai mkeo hana njemba ingine pembeni inayompa dozi bora mara kwa mara maana hizi zama za dotcom nazo zimesababisha majanga matupu kwenye mahusiano.

Lakini, je, mshaenda kwa mganga kwa dhumuni la kupata ushauri wa kitaalamu pamoja na kufanyiwa uchunguzi? Maana hata wanawake nao husumbuliwa na 'female sexual dysfunction' pia. Ni vyema mkalifikiria hilo.

Kukosa kwake hamu kunaweza kukawa ni dalili ya magonjwa mengine kama vile kisukari, hormonal imbalance, matatizo ya moyo, menopause, na mengineyo.

Pia, kabla ya wewe kuanza tu kumyooshea kidole cha lawama mwenzio, je, wewe umejiangalia? Usafi wako ukoje? Ni wa hali ya juu, kawaida, au chini?

Manake usije ukawa unatema viharufu vya ajabu ajabu ambavyo vinaua mzuka wa mkeo kushiriki kufanya mapenzi na wewe. Niamini, viharufu ni mzuka killer mkubwa sana.

Mwanzoni mwanzoni mtu anaweza akavumilia viharufu flani flani toka kwa mwenzie lakini baada ya muda huo uvumilivu nao huanza kufifia na mwishowe mtu anashindwa kabisa.

Kila la kheri. Ila, jiangalie na wewe.
 
pole sana kaa chini fikiria na chukua hatua.
Nalog off
 
Mkuu ondoa shaka ya usaliti kwa mkeo,

Hali hiyo huwa inatokea kwa wanandoa na msipokuwa makini mnaweza kuivunja ndoa yenu takatifu,

Mkeo anamsongo wa mawazo, ni tatizo la kisaikolojia linalomfanya mwanandoa kukosa hamu ya tendo la ndoa,

Njia ya kubadili hali hiyo ni lazima uwe mbunifu mkuu,

Kwanza anza wewe kubadilika kwakubadili aina ya maisha unayoishi,

Unaweza siku ukaamua mtoke out jioni ambako mtakula chakula huko huko, mnaweza siku mkaamua mje beach kigamboni kwetu kama mpo dar,

Mnaweza kuamua mfano krismasi inakaribia muende mikumi nk,

Pia badili staili ya kuomba tendo la ndoa, usitumie kauli bali lugha ya mwili na vitendo tu,

Jaribu kubuni maeneo mapya ya kufanyia mapenzi kama vile jikoni, bustanini, bafuni, kwenye banda lakuku nk, lakini zingatia watoto wasione,

Na mwisho badika lugha yako ya kimahaba, mkeo keshaichoka, we umeng'ang'ania swaga zilezile za kipindi unamtongozo mpaka leo mna watoto wawili?

Ukipanga vizuri hayo nakuhakikishia utaona penzi jipya,

Zingatia lugha ya kumtoa nyoka pangoni kwamkeo ni kila sekunde itumike, sio lugha za mkato na za ukali
 
NYANI GABU - Ahsante kwa ushauri wako na angalizo( Natumia muda wangu mwingi kumuuliza namna gani anataka niwe au nifanye ili ajisikie,lakini sijafanikiwa) Suala la kunuka makwapa ua mwili sina tatizo hilo kabisa(Niapenda usafi na ninazingatia usafi wa mwili na mavazi.)
 
Naomba msaada wa kuinusuru ndoa yangu(Naona ipo ukingoni...
Mimi ni baba mwenye watoto wawili(7 & 4) Nipo kwenye ndoa mwaka wa 8 sasa...
Nimeanza kupata matatizo na mke wangu yapata mwaka sasa kuhusiana na TENDO Zima la mchezo wa kitandani..
Kwakweli nimeshindwa hata kumuelewa,ANANIKATALIA kufanya mapenzi kwa visingizio kibao(Mara anasikia usingiz sana,mara hajisikii,mara amechoka sana)..Yaani ndani ya huu mwaka sijawahi kufanya naye mapenzi kwa ridhaa yake bila kumlazimisha kwanguvu)..
Yaani imefika wakati nika amua kumsaidia kazi zoote za nyumbani(Kufua kupika na kadhalika) Ili mradi akifika nyumbani asifanye kazi yoyote ya kumchosha..LAIKINI haija saidia kitu..
ANASEMA HANA HAMU KABISA HATA MWAKA UNAWEZA KUPITA BILA KUFANYA MAPENZI(WALA HAONI TAABU)..
Mwanzoni alikuwa akifanya kazi mjini(Akiondoka alfajiri na kurudi Jioni sana)..Sasa nimemfungulia salon hapa hapa maeneo ya nyumbani(Yote hiyo ni kujaribu kumpunguzia uchovu anosema ndio unamfanya akose HAMU.. Lakini haijasaidia kitu..
Kusema ukweli hii hali imenichanganya sana..( Mimi si mtu wa kutoka wala sijawazia jambo hilo) Lakini nitaishije bila kupata haki yangu ya ndoa??? Na mke ninaye???!
JAMANI NAOMBA USHAURI HATA KAMA NI WA KITABIBU : MAAANA HATA KAMA ANATEMBEA NA MTU MWINGINE(HATEMBEI NAYE KILA SIKU) LAZIMA KUNA SABABU ZA KIAFYA ZINAZOMFANYA HAKOSE HAMU...

Ngono ni kwa ajili ya kupata watotot tu na watoto unao, shida unayo wewe mwanaume
 
YERICKO NYERERE - Ahsante sana kwa ushauri wa kina...Na mapendekezo ya kufanya..Hakika nitajaribu kumtoa out ..out(Mimi si mtu wa kutoka out sana...."Mara chache sana)..Kuhusu lugha ya kumtoa nyoka pangoni( Nayo nitajaribu--Ila yeye huwa si mtu wa kunisikiliza hata kama namwimbia wimbo anasema namchosha)..!
 
Nyie mna tatizo la kutofutiana personalities. Sasa hata kama unamuimbia anachokaje jamani? Ama unamuimbia myimbp za rose mhando zile za kurusha kichwa kama madogoli?

Zungumza nae taratibu akuamboe unamkera kwa nini. Lakini tahadhari, sio lazma ubadilike jumla ili utate tendo la ndoa. Baada ya hapo labda mue de hoapitali kama mlivyoshauriwa awali. Manale walau mara moja kwa mwezi angekutamani aisee.

Wewe kama ni mkristu mpeleke kamuonjeshe kiti moto. Ukiona kapiga kelele ujue ana mapepo. Otherwise jaribu upange siku uende naye kwenye maombi, akipiga kelele ujue janaume pepo lipo. Ila kuna wengine husema inawezekana kila mlalapi kitandani inawezekana jini linakuwa kati yenu, na likimvaa yeye basi anafanya nalo night, linamchosha na lina mridhisha, hivyo kijibao chako kinakuwa hakina maana.

Nadhani jaribu kutumia pia ushauri wa wazazi/wasimamizi wa ndoa n.k.
 
Nyie mna tatizo la kutofutiana personalities. Sasa hata kama unamuimbia anachokaje jamani? Ama unamuimbia myimbp za rose mhando zile za kurusha kichwa kama madogoli?

Zungumza nae taratibu akuamboe unamkera kwa nini. Lakini tahadhari, sio lazma ubadilike jumla ili utate tendo la ndoa. Baada ya hapo labda mue de hoapitali kama mlivyoshauriwa awali. Manale walau mara moja kwa mwezi angekutamani aisee.
Ahsantela personalities tutafanyaje? nipe mahali pa kuanzia kufanya personalities zi-match!!
 
huyo atakuwa anamapepo tu, la msingi mpeleke kwa Kakobe au Lusekelo akaombewe coz haiwezekani muwe normal tu halafu gafla aanze kuku-dis.

Hata kama wewe na mkeo ni imani tofauti still nakushauri umpeleke kuombewa tu coz watu wengi tumeridhi imani zetu toka kwa wazazi tu.
 
Jaribu kumsoma mwenzio ujue ni vitu gani vinamfurahisha zaidi kusudi muendane. Angalia mziki anaosikiliza, labda ujadiliane nae pia. Kwani hamna nafasi ya kucheza pamoja? Mfano muulize anataka kuimbiwa wimbo gani na kama hauujui basi muimbe pamoja nk.

Ngoja kwanza, wakati ambapo unamsaidia kufua na kupika ili asichoke yeye anakuwa saluni. Ina maana wewe haufanyi kazi yoyote?
Ahsantela personalities tutafanyaje? nipe mahali pa kuanzia kufanya personalities zi-match!!
 
Hiii ndo unajua kwamba dini ya kiislam ni ya haki kwa mfano hilo tatizo lako lingekua lishakwisha pindi ungeengeza mke
 
Nadhani nina kazi ya ziada kuhusu hiyo "personalities" Mke wangu hapendi story na mimi tangu kitambo hicho....Mimi ni mtu anayependa kumuongelesha sana mke wangu..Ila yeye huwa anasema namchosha na maongezi marefu(hata kama tunajadiliana masuala ya kifamilia..Mimi ni mtu wa kujishusha sana kwake(Huwa namuomba samahani hata kama sijamkosea..Nikiona amekasirika ninapomuhoji jambo hajalipenda.......Kuhusu kufanya kazi(Mimi nafanya kazi zangu"through ONLINE" Nina Kampuni ya utalii...Huwa kazi zangu naziratibu nikiwa nyumbani..(Ofisini huwa naenda kukagua na kufuatilia mambop muhimu( Nina ofisi Zanzibar)
Jaribu kumsoma mwenzio ujue ni vitu gani vinamfurahisha zaidi kusudi muendane. Angalia mziki anaosikiliza, labda ujadiliane nae pia. Kwani hamna nafasi ya kucheza pamoja? Mfano muulize anataka kuimbiwa wimbo gani na kama hauujui basi muimbe pamoja nk.

Ngoja kwanza, wakati ambapo unamsaidia kufua na kupika ili asichoke yeye anakuwa saluni. Ina maana wewe haufanyi kazi yoyote?
 
NYANI GABU - Ahsante kwa ushauri wako na angalizo( Natumia muda wangu mwingi kumuuliza namna gani anataka niwe au nifanye ili ajisikie,lakini sijafanikiwa) Suala la kunuka makwapa ua mwili sina tatizo hilo kabisa(Niapenda usafi na ninazingatia usafi wa mwili na mavazi.)

Usafi wa kinywa je?
 
Kaka, unaweza kupungiza kuongea pia. Mwanaume akinyamaza na kutoa majibu mafupi mafupi inaweza kuwa sexy sana tu. Ila uwe unaenda ofisini mara kwa mara akumiss bwanaa khaa.

Ushauri uliopewa kuhusu maombi nao uzingatie. Huenda anahitaji msaada wa kiimani
 
Back
Top Bottom