Habari wakuu,
Leo nimeona nije niwaletee maswaibu yangu yanayo nikabiri kwenye ndoa yangu.
Mimi na mke wangu tuna miaka 6 ndani ya ndoa yetu, miaka mi 5 ya nyuma mambo yalikuwa safi kabisa, ila huu mwaka wa 6 umekuwa na heka heka nyingi mno.
Mambo ni mengi sana ila Leo tuanzie hapa.
MKE WANGU ANANIONA MIMI NI MZEE KWAKE
Mimi na yeye tumepisha umri wa miaka 6 yaani nimempita miaka 6 ya kuzaliwa
LEO ananiambia "wewe umenipita miaka mingi sana, yaani miaka 6 ni mingi sana, ilitakiwa angalau unipite miaka 2, wewe ni mkubwa sana kwangu, ilitakiwa tupishane miaka 2, ulinioa nikiwa mdogo, kwani hukujua kuwa umenipita miaka mingi."
Mimi nilikaa zangu kimya nikitafakari maneno yake, inanishangaza kuniona Mimi ni mzee Kwake, najiuliza maswali kama Leo sijafikisha hata miaka 40 lakini ananiona age go, je? Uzeeni si ataninyanyasa sana.
Nasubiri maoni yenu wakuu, nilipanga nimuwezeshe kibiashara lakini naona bora nimuache awe mama wa nyumbani tuu, na hiyo pesa ya mtaji Bora nimtumie mama yangu aitafune taratibu.
NB: Umri wangu Mimi ni miaka 34 na yeye umri wake ni miaka 28