Ndoa yangu haina amani

Ndoa yangu haina amani

Mkuu Liverpool VPN njoo umshauri jamaa

BTW anayewadanganyaga eti mke anaweza mlea mume ni nani?

Yaan kweli unaomba hela kwa mke ukaangalie mpira .....yaan bila aibu kabisa unaomba
Kawaida mbona kumuomba hela mkeo ila ni ile uliyompa wewe na sio anayoitafuta yeye
 
Wanawake wengi ni wabinafsi cha msingi wewe pambana urudi kwenye msitari
 
Aisee Polee Papaa.

Ila usikimbie nyumba.

Alaf Kwan hujui hela anaweka wapi? Ukiwa na shida unachukua na unamwambia kabisa na sio kuiba.
Anapofanya biashara huwez kwenda na kuchukua hela?.

Tafuta mishe nyingine,kopa hela kwa watu na nyingine kachukue kwenye biashara ya mke wako.

Hiyo kununa ipo tu, haitaisha kirahisi mpaka mambo yako yakawe sawa.

Alaf naona umezidi upole, dizaini kama mke anakupanda kichwani.

mwanaume mara nyingi unatakiwa uwe na roho na maamuzi magumu Mzee.
Wewe ndio Kidume sasa jamaa kazidi upole huyu
 
Ukweli nimechoka nahitaji kusafiri mbali na nyumbani kwangu kila mtu aishi maisha yake maana tunakaa muda wote kama mtu na mke mwenza.

Ndoa yangu ina miaka 5 tuna watoto 2. Nilikuwa nafanya Biashara vizuri nikafanikiwa kujenga nyumba ya Familia na kumfungulia wife biashara naye ili asinitegemee kila kitu.

Bahati mbaya biashara yangu ikayumba nikawa nakomaa nayo ila yeye muda wote ni kunikatisha tamaa niachane nayo.
Nikapata dharura ya kusafiri kwanda mkoani kwa wazazi nikamwacha kijana.

Huku nyuma wife akamsonga songa kijana mwisho Biashara yangu ikafugwa nikapigiwa simu na wife kijana anaingiza hasara nimefunga.

Niliporejea home uzi ni ule ule anataka niachane nayo. Kweli nikaamua kuachana nayo kwani kodi ya pango iliisha na pia palifugwa wateja wangekuwa wametuhama zaidi hivyo nikilazimisha naweza tengeneza hasara na madeni
nikahitimisha kufunga Rasmi.

Niko zangu home najipanga kutafuta mishe ya kufanya wife ndiye mwenye kazi ndiye kila kitu kinacho husiana na hela. Manyanyaso yakaanzia hapa,
kelele, kupangiwa anachotaka.

Jumamosi ya ngao jamii kati ya Simba na Yanga niliomba Elfu mbili tu nikakae kwenye kibanda umiza niangalie mechi nilitolewa nje.

Siku hiyo nilishinda home kuna kazi nilikuwa nafanya. Nilichoka kweli,
basi nikajirudia zangu home saa 18:00 kujilalia saa tatu na nusu akawa anaingia. Alipofika akanyosha moja kwa moja kitandani. Nikauliza “wife hupiki?” maana njaa inauma. Akasema sipiki na sijakununulia chochote tutakula kesho. Kila nikimwongelesha kimya basi kuepusha shari nikakaa kimya nikalala japo usingizi wa tabu uchovu + njaa + mawazo

Kuanzia siku hiyo ni kununiwa hakuna kusemeshana. Nimewaza niuze nyumba nipate mtaji naona ugumu biashara zikigoma.

Wazo langu kwa sasa kwa sababu sina thamani kwake niondoke nikatafute maisha mbali ata miaka 10 ili nipate amani na faraja. Nahofia nitakufa bure na mawazo naye abaki na amani yake anilelee tu wanangu.
Kuhusiana na mkasa huu nitoe Tu Angalizo Kwa wanaume Usiruhusu mwanamke akajua uthaifu wako na pia kukuzoea na kujua kila movement yako hawafai kabisa mfano nzur ni Delila Na Samson
 
Kwanini ulikubali kufunga biashara na ndo kipato pekee?. Au sijakuelewa?.
 
Story kama hii sikia tu kwa mwenzio,pole sana mkuu kwa unayopitia,sio kwa nia mbaya lakini inaonesha wife ana mchepuko wake tayari anakutafutia sababu tu ya kuachana..
My Take:Achana nae kabla hajakuletea vituko vya wazi wazi
jamaa kaandika kwa hisia sana,namwelewa snaa
 
Pole Sana mkuu,, Huyo Mwanamke anataka wewe uondoke ili umuachie nyumba. Ameshaona umepoteza dira hivyo hana tena mapenzi na wewe. Naamini time heal,, ni suala la muda tu utakaa sawa kiuchumi. Nakushauri hata kama utaondoka akikisha nyumba haiuzwi. Ondoka kafanye Maisha mbele ya Safari ili upate furaha ya moyo.. Hana mapenzi nawe hivyo jipende mwenyewe. Usikimbilie kuoa kwa kuamini utapata amani ya Moyo. Wanawake karibu wengi wapo hivyo.. Tafuta pesa utaenjoy Maisha... Mimi yalinikuta kama yako lkn sasa hivi naenjoy tu sina haraka ya kuoa. Bata Kwanza
 
Kuna mzee mmoja alinambia
Mwanamke akikuzingua na kwenye mawazo yako unawaza kumuacha unachotakiwa kufanya ni kutekeleza kile ulichowaza Mara moja..!
Ukianza Panga Pangua Mwanamke atakuwahi na atakufanya mbaya.
Usikubali kuachwa na Mwanamke huo Ni mkosi Mwanaume anaacha haachwi.
 
Una Elimu gani?, Huwezi tafuta kazi yoyote ile? Tafuta kitu chochote cha thamani uza, fungua biashara isiyohitaji mtaji mkubwa, hata kama ni banda la chips anzisha, sio lazima iwe karibu na nyumbani unapoishi, kwa mfano kama unaishi Kimara anzisha Banda Mbezi jinsi utakapokuwa busy na biashara moja itakufungua mawazo zaidi ya nini cha kufanya, ukipata mahali pazuri unaweza weka chips na Supu ya makongoro na ndizi.
Ushauri mzuri
 
Mkuu hi ilishanitokea,nilichofanya nikakopaa mtaji kwa baadhi ya watu wangu wakaribu.....kimya kimya nikafungua kibiashara,akawa anaona natoka asubui na Rudi usiku,nikaaza kulipaa bills zote,hapo hatushemedhani ikaenda nikasimama kuja kugundua na biashara akaaza kujirudi,nikaona hapa ndo penyeweeee nilikuwaaa nampelekeaaa motoo mzee baba,nikiwa juu ya kifua namkumbukaa yalee masimango naongezaaa kupeleka Moto mwisho wa siku Hadi hela zakee akaanza kuletaaa kwangu
You're a real man!
 
Kuna mzee mmoja alinambia
Mwanamke akikuzingua na kwenye mawazo yako unawaza kumuacha unachotakiwa kufanya ni kutekeleza kile ulichowaza Mara moja..!
Ukianza Panga Pangua Mwanamke atakuwahi na atakufanya mbaya.
Usikubali kuachwa na Mwanamke huo Ni mkosi Mwanaume anaacha haachwi.

You’re very Right,Dingi yangu aliwahi kunipa ushauri kama huu.Yaani unaacha mtu kwanza,kisha una deal na consequences!..sio unajiuliza itakuwaje wakati hata maamuzi hujafanya!
 
Mwanamke akiamua kukunyanyasa utatamani ardhi ipasuke uingie .pole yatapita ila ujifunze sasa kwamba unaishi na adui ndani.
 
Ukweli nimechoka nahitaji kusafiri mbali na nyumbani kwangu kila mtu aishi maisha yake maana tunakaa muda wote kama mtu na mke mwenza.

Ndoa yangu ina miaka 5 tuna watoto 2. Nilikuwa nafanya Biashara vizuri nikafanikiwa kujenga nyumba ya Familia na kumfungulia wife biashara naye ili asinitegemee kila kitu.

Bahati mbaya biashara yangu ikayumba nikawa nakomaa nayo ila yeye muda wote ni kunikatisha tamaa niachane nayo.
Nikapata dharura ya kusafiri kwanda mkoani kwa wazazi nikamwacha kijana.

Huku nyuma wife akamsonga songa kijana mwisho Biashara yangu ikafugwa nikapigiwa simu na wife kijana anaingiza hasara nimefunga.

Niliporejea home uzi ni ule ule anataka niachane nayo. Kweli nikaamua kuachana nayo kwani kodi ya pango iliisha na pia palifugwa wateja wangekuwa wametuhama zaidi hivyo nikilazimisha naweza tengeneza hasara na madeni
nikahitimisha kufunga Rasmi.

Niko zangu home najipanga kutafuta mishe ya kufanya wife ndiye mwenye kazi ndiye kila kitu kinacho husiana na hela. Manyanyaso yakaanzia hapa,
kelele, kupangiwa anachotaka.

Jumamosi ya ngao jamii kati ya Simba na Yanga niliomba Elfu mbili tu nikakae kwenye kibanda umiza niangalie mechi nilitolewa nje.

Siku hiyo nilishinda home kuna kazi nilikuwa nafanya. Nilichoka kweli,
basi nikajirudia zangu home saa 18:00 kujilalia saa tatu na nusu akawa anaingia. Alipofika akanyosha moja kwa moja kitandani. Nikauliza “wife hupiki?” maana njaa inauma. Akasema sipiki na sijakununulia chochote tutakula kesho. Kila nikimwongelesha kimya basi kuepusha shari nikakaa kimya nikalala japo usingizi wa tabu uchovu + njaa + mawazo

Kuanzia siku hiyo ni kununiwa hakuna kusemeshana. Nimewaza niuze nyumba nipate mtaji naona ugumu biashara zikigoma.

Wazo langu kwa sasa kwa sababu sina thamani kwake niondoke nikatafute maisha mbali ata miaka 10 ili nipate amani na faraja. Nahofia nitakufa bure na mawazo naye abaki na amani yake anilelee tu wanangu.
Nani alikwambia ndoa inaleta amani?
Mkiambiwa MSIOE HAMSIKII.

Sasa endeleeni kupigwa mijeredi.

#YNWA
 
Tatizo lenu mshaweka moyoni mwenu kuwa wanawake ndio kila kitu maishani mwenu. Na mtu yoyote akijua yeye ndio kila kitu kwako kwa nn asikiringie ....? Kwa Nini asikupeleke vile anataka.....?

Acheni ushamba ona Sasa Hadi mnataka kukimbia miji yenu

Mbona babu zenu waliwaweza Hawa viumbe nyie mnakwama wapi......?

Endeleeni kuwa entertain wawape show mbuzi nyie
 
Ukweli nimechoka nahitaji kusafiri mbali na nyumbani kwangu kila mtu aishi maisha yake maana tunakaa muda wote kama mtu na mke mwenza.

Ndoa yangu ina miaka 5 tuna watoto 2. Nilikuwa nafanya Biashara vizuri nikafanikiwa kujenga nyumba ya Familia na kumfungulia wife biashara naye ili asinitegemee kila kitu.

Bahati mbaya biashara yangu ikayumba nikawa nakomaa nayo ila yeye muda wote ni kunikatisha tamaa niachane nayo.
Nikapata dharura ya kusafiri kwanda mkoani kwa wazazi nikamwacha kijana.

Huku nyuma wife akamsonga songa kijana mwisho Biashara yangu ikafugwa nikapigiwa simu na wife kijana anaingiza hasara nimefunga.

Niliporejea home uzi ni ule ule anataka niachane nayo. Kweli nikaamua kuachana nayo kwani kodi ya pango iliisha na pia palifugwa wateja wangekuwa wametuhama zaidi hivyo nikilazimisha naweza tengeneza hasara na madeni
nikahitimisha kufunga Rasmi.

Niko zangu home najipanga kutafuta mishe ya kufanya wife ndiye mwenye kazi ndiye kila kitu kinacho husiana na hela. Manyanyaso yakaanzia hapa,
kelele, kupangiwa anachotaka.

Jumamosi ya ngao jamii kati ya Simba na Yanga niliomba Elfu mbili tu nikakae kwenye kibanda umiza niangalie mechi nilitolewa nje.

Siku hiyo nilishinda home kuna kazi nilikuwa nafanya. Nilichoka kweli,
basi nikajirudia zangu home saa 18:00 kujilalia saa tatu na nusu akawa anaingia. Alipofika akanyosha moja kwa moja kitandani. Nikauliza “wife hupiki?” maana njaa inauma. Akasema sipiki na sijakununulia chochote tutakula kesho. Kila nikimwongelesha kimya basi kuepusha shari nikakaa kimya nikalala japo usingizi wa tabu uchovu + njaa + mawazo

Kuanzia siku hiyo ni kununiwa hakuna kusemeshana. Nimewaza niuze nyumba nipate mtaji naona ugumu biashara zikigoma.

Wazo langu kwa sasa kwa sababu sina thamani kwake niondoke nikatafute maisha mbali ata miaka 10 ili nipate amani na faraja. Nahofia nitakufa bure na mawazo naye abaki na amani yake anilelee tu wanangu.
Ndo maana Najisemeaga siku Zote mke wangu mimi atabaki kuwa mama wa Nyumbani yaani Sitakubali eti afanye kazi au Nimfungulie biashara, yaani umempa mtaji mwenyewe leo hii anajiona Mwamba na Unakosa amani kwa Pesa yako Mwenyewe daaah, Inakera sana

Kwangu mi atabaki kuwa mama wa Nyumbani yaani hilo lazima lifanyika na sio kinyume chake, ***** walah
 
Mkuu njoo inbox tuyajenge! Pole sana ni changamoto ndogo sana hyo.
 
Back
Top Bottom