Ndoa ya mama PHD na baba standard seven

Ndoa ya mama PHD na baba standard seven

Mmmhhh hiyo tofauti ni kubwa sana jamani kha hata kama................

Unless huyo jamaa anamkwanja mrefu sana wanawake sisi mmmmmhhhh
 
Inawezekana kama wanapendana.. na kama inawezekana huyo mwanaume ajiendeleze hata kwa english course na kozi nyingine usefull za kupanua ufahamu wake..madam mamsapu ana elimu nzuri anaweza msaidia
 
Inawezekana kama wanapendana.. na kama inawezekana huyo mwanaume ajiendeleze hata kwa english course na kozi nyingine usefull za kupanua ufahamu wake..madam mamsapu ana elimu nzuri anaweza msaidia

Lol...Zayon Dota bana:becky::becky:

Kwa nini Inglishi kozi?
 
Mapenzi ya kweli hayaangalii elimu, kama mwanamke ana busara elimu haimnyimi mume ampendae na kama mwanaume anajiamini kuwa anaweza ongoza familia na kuwa na maamuzi yenye busara hawezi acha kuposa eti mwanamke ana PHD, tena kwa mwanamke mwenye mapenzi na mumewe hata siku akiambia hana akili na mumewe hawezi hata kujibu zaidi ya kunyamaza., si unajua wanaume tunavyojidai umeishia darasa la 7 lakini unamtukana mkeo ana masters yake kuwa hana akili, kisa mwanaume..........I LOVE AFRICA.
 
Lol...Zayon Dota bana:becky::becky:

Kwa nini Inglishi kozi?

Kiinglish muhimu.. Unaweza onekana bonge la msomi kama ung'eng'e unakubali. Nina uhakika huyo kaka kama ana 35 kwa sasa itakuwa ngumu kuhimili mikiki ya shule lakn english course ni rahis na inaweza mpandisha chati.
Pia muangalie chances za kuolewa za huyo mdada ni slim ( Level of education na age).. suala la elimu ni part ndogo na linarekebishika given others factors are okay..anaweza muacha huyo badae akamtamani hata mvuta bange na huyu wa sasa afadhali..
 
Kama demu ana sura mbaya na katumika tumika sana itasaidia kuleta some sort of balance kwani kwa vyovyote vile na yeye atakuwa amepigika katika kutafuta husband so she wont let him go
 
NDIO MAANA MNADAI BADO MPOMPO SANA KWASABABU WITO WENU KUOANA UKO KIMWILI NA SIO KIROHO.
Matokeo yake:-
1.WATU KUTEMBEA NA WAKE NA WAUME ZA WENGINE.
2.UBAKAJI.
3.KUTOKUWA NA MSIMAMO KIMAPENZI.
USHAURI:-
1.MAKE YOUR OWN CHOICE SPIRITUALLY.
2.SATISFY YOUR HEART BY SUCH CHOICE THEN,
3.TRUST GOD THE ALMIGHT.
 
That's easier said than done.

Very true... Honestly,mi mwenyewe sitakuwa comfortabo kuwa na mwanaume ambaye atakuwa hajiamin mbele macho yangi sababu ya elimu niliyonayo. Wanaume hawa mara nyingi wanapenda ku-interprete hata maneno ambayo mkewe atasema kwa nia nzuri,just bcoz atahis mkewe anatoa wazo flan kwakuwa yeye hana elimu ya kutosha...its crazy yaaani.
 
Habari zenu wakuu. Naombeni mawazo yenu nimsaidie dada yangu maana yuko katika wakati mgumu wa kuamua.

Ni dada mwenye miaka 32, mtoto mmoja, elimu ya PHD. Amekutana na mwanaume, mfanya biashara wa kawaida tu, elimu std 7, anaemzidi kama miaka mitatu. Wanapendana na mwanaume amepropose anataka wafunge ndoa haraka iwezekanavyo. kinachomtatiza ndugu yangu ni kwamba anawasiwasi kuwa understanding capacity yao inaweza kuja kuwaletea shida huko baadae as wanaume wakioa wanawake wa aina hii kunakuwaga na inferiority complex fulani na mara nyingi hawachukulii vitu vingi kwa namna sawa. Kuna ambae ana uzoefu na jambo hili na wenye mawazo naomba tumsaidie ndugu yetu. natanguliza shukran

Mwambie asijaribu kufanya kitu kama hicho, PHD na std 7, thats too much, yani its like samaki na mwewe wafunge ndoa, wataishi wapi?

" If the interviewer asks u , what salary u expect, try answering by saying.' That is good question, what are u planning to pay ur best candidate ? "
 
hiyo ndoa haitadumu,tuache kuwadang'anya hao wana ndoa,yaani hapo kila atakalo hoji mke ni lazima mume/ndugu wa mume wa jumuishe na elimu ya mke,labda mke awe mpore na asihoji mambo yatakayoweza leta utofauti wa elimu.labda kama mume angekuwa na elimu kubwa hapo ndo ingedumu.
 
dada yako naye ana shida!
yaani kusoma koote huko kukutana na wanaume mablimbali kote huko kuanzia sekondari, vyuoni, dgree, masterz hadi na phd hakuona kabisaaaaa.....?????!!!!!
 
Habari zenu wakuu. Naombeni mawazo yenu nimsaidie dada yangu maana yuko katika wakati mgumu wa kuamua.

Ni dada mwenye miaka 32, mtoto mmoja, elimu ya PHD. Amekutana na mwanaume, mfanya biashara wa kawaida tu, elimu std 7, anaemzidi kama miaka mitatu. Wanapendana na mwanaume amepropose anataka wafunge ndoa haraka iwezekanavyo. kinachomtatiza ndugu yangu ni kwamba anawasiwasi kuwa understanding capacity yao inaweza kuja kuwaletea shida huko baadae as wanaume wakioa wanawake wa aina hii kunakuwaga na inferiority complex fulani na mara nyingi hawachukulii vitu vingi kwa namna sawa. Kuna ambae ana uzoefu na jambo hili na wenye mawazo naomba tumsaidie ndugu yetu. natanguliza shukran

kuwa na PhD manake ni ku-toa mchango wako ktk eneo fulani la taaluma. kuwa na pHD siyo kujua kila jambo. nina pHD ya kutoa ushauri, manake ni kuwa nimechangia maarifa yangu ktk eneo la kutoa ushauri- hii hainifanyi mimi niwe mlinzi bora, mchumi bora, mwalimu bora . wala hainifanyi niwe mume ninaefahamu na mwenye kukubalika kuliko wanaume wote wasio na pHD...
ushauri wangu ni kuwa ...
2.ikiwa Dada yako phD yake haihusiani na mambo ya ndoa , au biashara au aina ya biashara anayofanya huyo shemeji yako mtarajiwa hakuna tatizo kwani hakuna patakapo tokea mgongano wa kielimu ktk maisha yao ya ndoa- kama ikitokea ni mgongano wa kawaida ambao chanzo siyo tofauti ya elimu
1.Dada yako anaonekana kuwa na mawazo ya kuwa yeye ni mwenye kufahamu zaidi kuliko wale walio elimu darasa la saba- nimeshindwa kutumia msamiati hapa huenda ungeliona ninamtukana. mshauri afute hilo akilini mwake kwani litamsumbua si tu kwa huyo bwana bali pia akiwa ktk mawasiliano na wote wasio na phd.
hayo namba 2 na 1 ni kwaajili ya dada yako ... na hili hapa chini ni kwaajili yako wewe

Ninawasiwasi kuwa hii wasiwasi ya elimu ya huyo shemiji yetu mtarajiwa unayo wewe na si dada yako ndo aliyeonyesha hiyo wasiwasi. ikiwa wasiwasi ni yako wewe, basi jaribu kuongea nae wewe mwenyewe na akutoe huo wasiwasi wako
 
inawezekana lakini yahitaji kuheshimiana na kuchukuliana kwa hali ya juu,nature shud be applied ,huyo mume asiwe na inferiority complex na huyo mke asimdharau mumewe kwa namna yeyote, amuonyeshe anampenda na kumuheshimu even infront of pipo, kingine huyo mume lazima awe mtafutaji
 
Ukitaka kuoa oa mwanamke wa taipu yako,ambaye mnaendana kwa baadhi ya vitu, ajaribu aone mziki wake !!
Wakigombana tu atatukanwa kwa kiinglish hadi akome !!
 
Habari zenu wakuu. Naombeni mawazo yenu nimsaidie dada yangu maana yuko katika wakati mgumu wa kuamua.

Ni dada mwenye miaka 32, mtoto mmoja, elimu ya PHD. Amekutana na mwanaume, mfanya biashara wa kawaida tu, elimu std 7, anaemzidi kama miaka mitatu. Wanapendana na mwanaume amepropose anataka wafunge ndoa haraka iwezekanavyo. kinachomtatiza ndugu yangu ni kwamba anawasiwasi kuwa understanding capacity yao inaweza kuja kuwaletea shida huko baadae as wanaume wakioa wanawake wa aina hii kunakuwaga na inferiority complex fulani na mara nyingi hawachukulii vitu vingi kwa namna sawa. Kuna ambae ana uzoefu na jambo hili na wenye mawazo naomba tumsaidie ndugu yetu. natanguliza shukran

Kwa upande wangu naona watawezana maana huyo dada yako ni mzungu na huyo jamaa ni mwafrika tena Mtanzania.Nasema hivo kwa kuwa kwa Tanzania yetu na mlolongo wa elimu yetu hakuna tena nasema hakuna kabisa mtu anaeweza kupata Phd akiwa na miaka 32, I stand to be corrected forever
 
Back
Top Bottom